BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,098
Sioni sababu yoyote ya muhimu ya kuuendesha Uwanja wetu wa Kimataifa kwa ubia na kampuni toka China.
Posted Date::4/28/2008
Uwanja wa ndege kukodishwa Wachina
*Ni ule wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar
*Kuendeshwa kwa ubia na Kampuni ya Sonangol
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi
KATIKA moja ya maamuzi mazito ambayo yanatarajiwa kufanywa tangu kuanza mageuzi ya Sera za Uchumi, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere sasa utaendeshwa kwa ubia.
Uchunguzi huo wa Mwananchi umebaini kwamba, serikali iko katika mazungumzo kwa muda mrefu kati yake na Kampuni ya China Sonangol ili iweze kukabidhiwa jukumu la kuuendesha uwanja huo kwa ubia.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo, China Sonangol inatarajiwa kufanya magaeuzi makubwa katika uwanja huo, ikiwa ni pamoja na kujenga eneo jipya la kutua ndege ambalo litafahamika kama 'Terminal Three'.
Uwanja huo kwa sasa una sehemu mbili (Terminal One na Two), ambazo hutumika kwa ajili ya ndege hutua na kuondoka.
Katika mpango huo, Mwananchi imezidi kubaini kwamba, China Sonangol pia itakarabati katika kiwango cha juu eneo la Terminal One na Two, kutoka hali ya sasa.
Uchunguzi huo pia umebaini kampuni hiyo iwapo itakubaliwa katika mazungumzo yanayoendelea, itajenga Chumba kipya cha Wageni Maarufu (VIP) kutokana na kilichopo sasa kuwa kidogo na ambacho hakiendani na wakati.
Naibu Waziri wa Miundombinu, Dk Makongoro Mahanga na Katibu Mkuu Omari Chambo, wote walipoulizwa walisema kwa kifupi hayo ni mazungumzo tu.
Dk Mahanga alisema hadi sasa hakuna makubaliano ambayo yamefikiwa katika suala hilo, kwani kilichopo ni mazungumzo.
Hata hivyo, Dk Mahanga ingawa hakukataa wala kuthibitisha kama kampuni hiyo itakubaliwa, alisisitiza kwamba uamuzi kama huo hata ukifanyika si mgeni kwani nchi nyingi duniani huendesha viwanja vya ndege kwa ubia.
"Sitaki kuzungumzia kitu ambacho hakipo kwani hayo ni mazungumzo tu, lakini hata kwa mfano mpango huo wa ubia si mpya kuna nchi nyingi duniani zinaendesha viwanja vya ndege kwa ubia," alisisitiza kwa kifupi.
Kwa upande wake Chambo, alisema suala hilo linaweza kupotoshwa, lakini akaahidi kutoa taarifa zaidi kwa gazeti hili.
"Msianze kupotosha jambo zuri likawa baya, nitafute nikupe taarifa zaidi kuhusu hilo," alisisitiza.
Wakati Dk Mahanga na Chambo, wakikataa kuzungumzia hilo kwa undani, uchunguzi huo umebaini zaidi kwamba China Sonangol, ndiyo ambayo pia iko katika mpango wa kuisaidia ATC kivifaa na kuboresha usafiri wa ndege kutoka nchini hadi Beijing.
Kwa mujibu wa uchunguzi huo wa kina, Rais Jakaya Kikwete akiwa katika ziara yake nchini China wiki mbili zilizopita, suala hilo lilitiliwa mkazo zaidi.
Ziara hiyo ya Rais pia aliandamana na aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge.
Mwananchi imebaini kwamba, eneo ambalo linaangaliwa kujengwa VIP mpya ni karibu na Dahaco.
Katika uchunguzi wake huo, Mwananchi imebaini kwamba ubia huo utakuwa katika kiasi ambacho kinaweza kuwa asilimia 50 kwa 50, ingawa mjadala kuhusu hilo bado.
Uwezekano huo unatokana na Kampuni hiyo ya Kichina kutarajiwa kutoa kiasi kikubwa cha fedha za uwekezaji, ambazo zitafanya nayo iwe na nguvu kubwa katika maamuzi ndani ya menejimenti.
Taarifa hizo za kiuchunguzi zinaonyesha kwamba, tayari Kampuni ya China Sonangol, imeonyesha nia ya kukubali kulipia deni la kati ya Sh 9 hadi 10 bilioni, kutoka kwa wananchi wa eneo la Kipawa lililo karibu na uwanja huo wanaodai fedha za kuhamishwa kwa ajili ya kupisha upanuzi huo.
Hata hivyo, suala hilo liko katika hatua za mwanzo na inaelezwa kwamba, bado halijafakikishwa katika Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kujadiliwa na kutolewa maamuzi na wala kujadiliwa na Kamati ya Bunge ya Miundombinu.
Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Mohamed Misanga, alisema hana taarifa yoyote kuhusiana na suala hilo na anachojua ni kwamba, uwanja huo unaendeshwa kama kawaida wala hajui mpango wa ubia.
"Kamati haina hiyo taarifa, ninachoamini na kuendelea kuamini ni kwamba, uwanja unaendeshwa kama kawaida," alisisitiza Misanga.
Iwapo uwanja huo utaendeshwa kwa ubia itakuwa ni moja ya hatua kubwa kutokana na unyeti wake kwa usalama wa nchi, kwani ni moja ya eneo muhimu kwa maadui wa ndani na nje kuweza kuihujumu nchi.