Polisi ndio uwafanyia vurugu wapinzani kwa kutii maagizo ya wanasiasa makanjanja kina bashite
Baada ya Bashite kuondoka hutakaa uone uonevu kwa wapinzani, its obvious JIWE hakuwahi kumtuma alokuwa anafanya.
saa hii atakuwa gym kupunguza ipsi
 
PICHA KUTOKA JNIA

======

UPDATES;

1105HRS: Hapa uwanjani pametulia, hakuna fujo wala dalili za fujo, Wanachama wachache wa CHADEMA wanaonekana wakipita pita huku na kule. Bado sijabahatika kuona gari la Polisi Wala Gari la CHADEMA.
View attachment 1518414
View attachment 1518413
Ratiba inaonesha muda wa ndege kufika ni saa saba na dakika Ishirini. Angalia kwenye chati
View attachment 1518416
1121hrs: Saa moja iliyoisha Tundu Lissu ndo amepanda ndege ya Ethiopian Airlines ET 805 kutoka Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Bole Addis Ababa kuja hapa Dar Julius Kambarage Nyerere International Airport.

Safari inatazamiwa kuchukua masaa yasiyozidi Matatu kufika hapa tulipo.
View attachment 1518415
1140hrs: Mwenyekiti Mkoa wa Iringa CHADEMA William Mungai, aliyekuwa Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche na aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Joseph Mbilinyi(Sugu) Wakiwa Wamefika hapa Uwanja wa ndege kumpokea Lissu
View attachment 1518417
1156HRS: Kutoka kushoto: Hekima Mwasipu, Wakili wa Chadema, Sugu, Catherine Ruge(Simba Jike) Viti Maalum Mara na Mgombea wa Jimbo la Segerea CHADEMA
View attachment 1518418
1230hrs: Polisi Magari Mawili ya Polisi wameshusha Wanausalama wa kulinda amani wapatao kama 30 nje ya Viunga vya Uwanja wa ndege. Wamekaa mstari kama Gwaride na wanapewa Maelekezo. Wameshusha njia Panda ya kuelekea Uwanja wandege. Kuna askari wanne walikuwepo tangu asubuhi Wakihoji kila anaye ingia.

Bodaboda kama 50 wapo hapo Askari Polisi Walipo, nadhani Wamekataliwa kuingia. Vilevile Magari ya CHADEMA maarufu kama Magari ya M4C, Yapo sehemu hiyo ya njiapanda yakizunguka huku na kule. Magari ya CHADEMA yapo Matano yamejaa watu waliovalia nguo za CHADEMA.

Polisi ukijielezea unapoelekea ndo Wanaruhusu. Lalikini kuna baadhi ya Wafanyakazi(Walinzi wa Uwanja, sio Polisi) ndo wanakataza watu kuingia.
View attachment 1518419View attachment 1518420
1240: Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wameweza kupenya na kuongia ndani sehemu ya kusubiria Wageni
View attachment 1518423View attachment 1518422View attachment 1518421
View attachment 1518424
View attachment 1518425
1300hrs: Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA wameruhusiwa kuingia. Wengine wapo nje ya Uwanja wanaimba nyimbo.
View attachment 1518426
Polisi Tanzania Wamewaruhusu Wanachama wote wa CHADEMA na Wafuasi wa Tundu Lissu. Muda wowote ndege itawasili

View attachment 1518431

View attachment 1518432

MATAGA jana wamelala na viatu , na shombo za samaki, imewau kweli kweli, hawana utu na ubinadamu, wanatama Lissu afe hata sasa hivi; ila Mungu amejitukuza.
 
Leo ccm na serikali yake hawatakiwi kabisa kuhamasisha watu km walivohangaika siku tatu zilizopita kwenda kuaga mwili wa mkapa maana watz wataenda wenyewe kumsindikiza Nabii Tundu LISSU......
 
Ccm Ina viongozi wasio na akili kabisa. wananunua wabunge na madiwani alafu hawawezi kuwanunua watz??

CHADEMA ni mpango wa Mungu na ni chama cha mioyo ya watz wkt ccm ni chama Cha mioyo ya polisi, tume ya uchaguzi na msajili wa vyama......PERIOD
 
An alternative apology. Hakuna kitu kama hicho. Ujasiri wa Lissu hata wao wameshikwa na butwaa
Ina maana huo umati uilikuwa na nguvu kuliko maandamano yeyote ya Chadema yalowahi kutokea nchi hii au kuliko mambo yeyote ambayo polisi washawahi kuyaingilia au ni kujifanya tu kuwa huwajui wa Tanzania?

Watu tunashukuru jamaa hawakuingilia na hilo lilishauriwa muda mrefu kabisa polisi kukaa mbali,bado hakuna mwanachadema ambae alikuwa na ubavu wa juzuia polisi kama wangeamua kuchukua maamuzi tuloyazoe.

Hii ndio hasara ya kuwa mpinzani hewa,ukiachwa unasema umeogpwa,ukipigwa unasema umeonea,lazima tubadilike siasa si upepo wala kivuli.
 
Mkuu uzi wa reference niliokupa una maelezo ya nani kamtekeleza mwenzake.

Sasa unaponiuliza maswali ambayo yako wazi kwenye sehemu niliyokupa tunakuwa hatupigi hatua mbele.

Tafadhali rejea kwenye reference ile wametajwa.
Tuliowapa mamlaka nao hatuoni kuvaa hata barakoa na huwa wapo kwenye mikusanyiko, mpaka juzi Dodoma akawa anasema kwani wao hawaogopi kufa. Ndiyo maana nikauliza aliyemtelekeza mwenzie nani?
 
Ushauri mzuri ila CHADEMA ni wastaarabu sana, mambo waliyofanyiwa na viongozi wa CCM kama wangekuwa na traces za ukorofi lazima wangefanya vurugu kama za wapigania uhuru wa Afrika ya kusini.
Mkuu 'Chesty', sema CHADEMA walitumia akili kubwa kuepuka vishawishi vya kufanya mambo ambayo yangewasababishia kufutwa kabisa.

Mengi ya waliyofanyiwa ilikuwa ni mitego ya kichokozi, ili waingie kichwa kichwa na wamalizwe.

Wanastahili pongezi kwa kuiepa mitego yote ile. Sasa wajipange kwa ushindani halisi kuwavuta wananchi upande wao.
 
Back
Top Bottom