Uwanja wa Majaliwa | Vodacom Premier League (VPL) Namungo FC dhidi ya Yanga SC

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Ligi Kuu Tanzania, Vodacom Premier League (VPL) kuendelea kupigwa leo March 15, 2020 ambapo wenyeji wa mchezo Namungo FC wanapepetana na Yanga SC, kwenye uwanja wa Majaliwa, (Majaliwa Stadium) Ruangwa mkoani Lindi

Kipute hicho kinatarajiwa kuwa kigumu na kikali kwa pande zote kutokana kila mmoja kuhitaji alama tatu muhimu, ambapo Namungo FC wakiwa nafasi ya 4 kwa alama 49 kwa michezo 27, wanahitaji alama tatu ili kuweza kuishusha Yanga SC iliyoshika nafasi ya 3 kwa alama 50 kwa michezo 26 ambayo inataka kusogea zaidi nafasi ya juu ya msimamo wa ligi.

Katika mchezo huo Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa ametoa hamasa kwa wakazi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi ili kuipa nguvu Namungo FC huku akieleza namna alivyopambana hadi timu hiyo kupanda daraja na kuwa tishio VPL

"Kesho (yaani leo) nataka kuparua parua mtu mzima", amesema Majaliwa.

Naye kocha wa Namungo FC, Hitimana Thiery amesema mchezo utakuwa mgumu, lakini kutokana kuwa katika Uwanja wa nyumbani amejiandaa kushinda.

Kwa upande wake Kocha wa Yanga SC Luc Eymael amesema kuwa amekwenda na wachezaji wachache lakini ana imani ya kufanya vizuri na kusonga mbele.

Hata hivyo kocha Eymael ameonyesha kusikitishwa kwake kitendo cha baadhi ya wachezaji kutosafiri na timu, akisema wachezaji wamekosa weledi na hakubaliani nao kwani nikuvunjia heshima klabu kubwa kama Yanga huku akiwatuhumu baadhi ya wachezaji kuchagua mechi.

Kumbuka mtanange ni kuanzia saa 10: 00 jioni. USIKOSE UKAAMBIWA

Reporter, Ghazwat

==================

Update;

Klabu ya Namungo FC, wametoka sare ya kufungana bao moja kwa moja na Yanga.

Yanga ndo waliokuwa wa kwanza kupata bao mapema kabisa dakika ya 05, likifungwa na Tariq Seif, bao ambalo lililodumu hadi mapumziko

Kipindi cha pili, kilianza kwa kasi kwa pande zote, lakini Namungo FC, waliweza kusawazisha kupitia kwa Bigirimana Blaise kunako dakika ya 62 za mchezo.

VPL, FT; Namungo FC 1-1 Yanga SC

FB_IMG_1584249370833.jpeg
 
Shida nini hao wachezaji hawapo

Sent using Jamii Forums mobile app
Niyonzima kocha Eymael amesema amesimamishwa, lakini taarifa za hivi punde wanadai ana kadi tatu za njano.

Yondan ana ruhusa ya mwalimu kushughulikia familia yake, na Molinga ameomba ruhusa kwani mkewe ni mgonjwa.

Lamine, Mo Banka, Adeyum wanadaiwa kuwa wagonjwa, kwa mujibu wa Official page ya Yanga SC
 
Ligi Kuu Tanzania, Vodacom Premier League (VPL) kuendelea kupigwa leo March 15, 2020 ambapo wenyeji wa mchezo Namungo FC wanapepetana na Yanga SC, kwenye uwanja wa Majaliwa, (Majaliwa Stadium) Ruangwa mkoani Lindi

Kipute hicho kinatarajiwa kuwa kigumu na kikali kwa pande zote kutokana kila mmoja kuhitaji alama tatu muhimu, ambapo Namungo FC wakiwa nafasi ya 4 kwa alama 49 kwa michezo 27, wanahitaji alama tatu ili kuweza kuishusha Yanga SC iliyoshika nafasi ya 3 kwa alama 50 kwa michezo 26 ambayo inataka kusogea zaidi nafasi ya juu ya msimamo wa ligi.

Katika mchezo huo Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa ametoa hamasa kwa wakazi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi ili kuipa nguvu Namungo FC huku akieleza namna alivyopambana hadi timu hiyo kupanda daraja na kuwa tishio VPL

"Kesho nataka kuparua parua mtu mzima", amesema Majaliwa.

Naye kocha wa Namungo FC, Hitimana Thiery amesema mchezo utakuwa mgumu, lakini kutokana kuwa katika Uwanja wa nyumbani amejiandaa kushinda.

Kwa upande wake Kocha wa Yanga SC Luc Eymael amesema kuwa amekwenda na wachezaji wachache lakini ana imani ya kufanya vizuri na kusonga mbele.

Hata hivyo kocha Eymael ameonyesha kusikitishwa kwake kitendo cha baadhi ya wachezaji kutosafiri na timu, akisema wachezaji wamekosa weledi na hakubaliani nao kwani nikuvunjia heshima klabu kubwa kama Yanga huku akiwatuhumu baadhi ya wachezaji kuchagua mechi.

Kumbuka mtanange ni kuanzia saa 10: 00 jioni. USIKOSE UKAAMBIWAView attachment 1388878
Aparure uwanjani maana tunamjua yeye ni Mikia lialia.
Isiwe kacheza na marefa kama senior adviser wenu.
 
Back
Top Bottom