Uwanja wa Julius Nyerere ni kama daladala – Wabunge

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,007
Uwanja wa Julius Nyerere ni kama daladala – Wabunge
Cassian Malima, Dodoma
Daily News; Saturday,August 23, 2008 @00:03

Wabunge jana walielekeza mashambulio kwa wanaosimamia chumba cha watu mashuhuri (VIP) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, kwamba wamesababisha kishuke hadhi na kuwa kama daladala kutokana na kuruhusu wasio na hadhi kuingia humo holela.

Kwa mujibu wa wabunge, licha ya VIP wa nchini, kero kubwa ni ya raia wa kigeni na hasa wenye ngozi nyeupe ambao wote wanadai kuwa ni VIP. "Sisi tumekuwa wakarimu mno, tunawapa hadhi ya VIP, kwao hawatupi," alisema Ramadhani Maneno (Chalinze-CCM), ambaye alilidokeza Bunge kwamba kuna wakati wageni wanaostahili husimama mle kama wako kwenye daladala.

Mwenzake, Daniel Nsanzugwanko (Kasulu Mashariki-CCM), alisema hali ilivyo kwenye chumba hicho cha VIP ni "vurugu tupu." Alisema wakati fulani alikerwa wakati akitoka safarini Ulaya aliposhuhudia wafanyakazi wa Kampuni ya Saskatel inayojihusisha na TTCL, wakiingia mle huku wakiwa wamevaa kaptula.

"Ati nao wakapita VIP. Wazungu wamefanya pale kuwa ni mahali pa kuvutia sigara, fanyeni ili pale pawe na heshima," alisema Nsanzugwanko. Kabla ya hoja hiyo kujibiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambaye hotuba yake ya bajeti ilikuwa ikijadiliwa, Spika aliingilia kati baada ya Nsanzugwanko kuzungumza na kusema chumba kile hakistahili kuwa VIP, bali kilijengwa ili kiwe Ofisi ya Meneja wa Uwanja.

"Mimi nilikuwa Waziri wa Ujenzi wakati uwanja ule unajengwa (miaka ya mwanzo ya 1980). Ile ilipaswa kuwa Ofisi ya Meneja wa Kiwanja. Cha muhimu kwa serikali kutoa fedha ili ijengwe (VIP) nyingine," alisema. Akiwajibu wabunge, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa alisema hatua zitachukuliwa kurekebisha hali hiyo. Alihoji; "Hivi jamani, kama Membe ni VIP na ndugu zake ni VIP? Alijibiwa "hapana" na hapo akaahidi kukaza kamba wasiostahili wasiingie katika chumba hicho.
 
Back
Top Bottom