Uwanja wa Jamhuri, Morogoro | Vodacom Premier League VPL : Mtibwa Sugar 0 - 3 Simba SC

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Mechi kali ya Patashika ya ligi kuu Tanzania bara kupigwa leo February 11, 2020 kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro, ambapo Wakata Miwa, Wana Tamu Tamu, Mtibwa Sugar wanamkabili Mfalme wa Nyika, Mnyama Mkali, Simba SC.

Mechi kali ya hamsha hamsha yenye kusisimua pamoja na burudani ndani ya uwanja kwa muda wote wa dakika 90 za mchezo, hivyo timu hizi zinakutana ikiwa kila moja kuwa na kumbukumbu ya kupoteza michezo yao iliyopita ambapo Simba walipoteza dhidi ya JKT Tanzania 1-0 huku Mtibwa Sugar wakilala kwa Lipuli FC bakora 1-0.

Kocha wa Simba, Sven Vanderbroeck amesema, amejiandaa kikamilifu pamoja na kufanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwa vitendo uwanjani ili kuepuka makosa yaliyopita hivyo iwe hali ya uwanja, mvua au waamuzi wa mchezo haipaswi kuwa sababu, ni ushindi pekee tunawahitaji na wana kazi ya kuhakikisha hilo.

Kocha Zuberi Katwila amesema mchezo unategemewa kuwa mgumu na wa ushindani na kwa upande wao matokeo mabaya yaliyopita kwa mechi tatu mfululizo hayana nafasi ya kuwafanya wasiibuke na ushindi dhidi ya Simba SC.

Kumbuka mchezo kuanzia saa 10: 00 jioni, Usikose Ukaambiwa.

••••Ghazwat•••••Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana


IMG_20200211_152718_917.jpeg
IMG_20200211_152702_293.jpeg

UPDATE
Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba imeendelea kujikita kileleni baada ya kuichapa Mtibwa Sugar kwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Katika mchezo huo Simba ilipata mabao yake kupitia nahodha John Bocco, beki Mohamed Hussein na kiungo Hassan Dilunga.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 53, kifuatiwa na Azam (44) Yanga (37) kabla ya mechi yake dhidi ya Mbao na Namungo ikiwa ya nne na pointi 36
 
Wakati wowote mpira utaaza Uwanja wa Jamhuri VPL

Naaaaaaaaaaam mpira umeanza dakika 90 za jasho na damu kusaka alama tatu muhimub

Mtibwa Sugar 0-0 Simba SC
 
05' Mchezo umeanza kwa kasi huku Simba wakimjaribu golikipa wa Mtibwa Sugar Kado kwa shuti ambalo alidaka

Huku Mtibwa wajibu shambulizi na kujipatia kona ambayo haikuzaa bao
 
10' na 12' mashambulizi kuelekea lango la Mtibwa Sugar, almanusura Kagere aandike bao, baada ya kukosa kuunganisha krosi.

Mtibwa Sugar 0-0 Simba SC
 
21' ilikuwa hekaheka lango la Simba, lakini golikipa Manula anapangua hatari ile na kuwa kona...Daah ilikuwa hatari kwakweli

Inapigwaaaaaa Kona inaokolewa na Simba na wanamiliki sasa mpira
 
Back
Top Bottom