Uwanja sawa, lakini Bil. 2 hapana!

Mkuu umeandika mambo mengi mazuri lakini hujajibu hoja ya jamaa kwamba kimsingi je hiyo 2b ambayo si haba anaitoa kama mwanachama au shabiki wa kawaida au kama mwekezaji ? Nafikiri hoja iko hapo . Kwamba , kama anatoa 2b kuonesha mfano kwa wanachama , wapenzi , mashabiki na wadau wa soka kuchangia basi ni jambo jema sana ; lakini kama hiyo 2B itahesabiwa ktk zile 20B basi itakuwa si sawa . Atapaswa kuchangia kutokana na 49% ya hisa zake maana atakuwa mmiliki kwa 49% kwa hiyo lazima afanye kitu zaidi ya 2B .
 
Japokuwa mimi ni Simba dam dam ila hili nililipinga tangu mwanzo ila wakaishia kuniita mwana utopolo na wengine wakadiriki hata kuniuliza nateseka nikiwa wapi, ila huo ndio uhalisia hapa Mo anatupiga kama wana simba.
Unateseka ukiwa wapi

Mo sio wa kwanza kutupiga muache atupige tu ila la muhimu anayoyatamka ayafanyie kazi full stop....
 
Hongera kwa andiko zuri Sana....!!!!
Bahati mbaya au nzuri hauja eleza kuhusu muundo wa klabu ya Simba na namna ambavyo watapata hasara kupitia Mo kutoa Bilioni 2.
Simba sio Mali ya Wana Chama peke yao, bali ni kampuni.
Ili kujadili kuhusu klabu ya Simba ni lazima kufahamu mambo yafuatayo.
1.Simba Sport Club
2.Simba Holding company Limited
3.Mo Simba Company Limited
4.Simba Sports Club Company Limited

Ukifatilia Kuna Simba nne ambazo zipo kwenye miundo Tofauti Tofauti.
Simba ya kwanza...SIMBA SPORTS CLUB mwenyekiti ni Mangungu....!!
Hii ni club ya Simba ambayo ndio imeunda kampuni yao brella ambayo inaitwa SIMBA HOLDING COMPANY yenye hisa asilimia 51.
Simba nyingine ni MO SIMBA COMPANY LIMITED hii ni kampuni ya Mo ambayo imesajiliwa Brella ina asilimia 49.
Kampuni za SIMBA HOLDING COMPANY na MO SIMBA COMPANY LIMITED zimeungana na kutengeneza kampuni Moja ambayo inaitwa SIMBA SPORTS CLUB COMPANY LIMITED.
Kampuni hii ndio Ina endesha klabu ya Simba Kwa kupitia Bodi ya wakurugenzi ambayo imeajili C.E.O ambae ana endesha klabu katika shughuli za Kila siku kwa niaba yao.

Kimsingi Mali za Simba na Madeni ya Simba ni ya Mo Dewji pamoja na Wana Chama wa Simba, maana na yeye ni sehemu ya umiliki kupitia kampuni yake ya Mo Simba Company Limited.
Kwaiyo basi maendeleo,Mafanikio au hasara zina mgusa Mo Moja kwa Moja kwa maana ni muwekezaji ndnai ya Simba.

Ni rudi kwenye hoja yako ya Mo kutoa Bilioni 2 kwneye ujenzi kati ya kiasi Cha Bilioni 30 zinazo hitajika.
Jambo Moja la msingi kutambua ni kwamba hivi ndani ya klabu ya Simba Kuna mwana Chama ambae ameweza kuchangia kiasi Cha kuanzia Bilioni 1 na kupanda juu...?
Wewe imechukua jumla ya michango inayo hitajika nakuona Mo katoa pesa kidogo kuliko Wana Chama.
Bila kujua kumbe Wana Chama Hawa Wana changia kuanzia buku au elfu tano,elfu hamsini, laki, milioni na kuendelea.
Lakini Mo yeye mtu mmoja katoa Bilioni 2 lakini Wana Chama wao kwa umoja wao wana toa bilioni 28.
Hapa kimantiki Mo katoa nyingi kama mtu mmoja kulinganisha na mtu mmoja mmoja kwenye mchango wake.
Kwaiyo kama tugesema tutafute msimamizi wa mradi kwa kuangalia mchango wake yeye ndio ana stahili kuwa mwenyekiti wa mradi kwa pesa yake kuwa nyingi kuliko mwana Chama yoyote.
Wanachama wa simba inabidi wachangie 51% ya pesa zinazohitajika na Mo achangie 49% ya pesa,,,, kama Mo amechangia B2 kama mwanachama mwenye mapenzi na simba haimaanishi nafasi take kama mdhamini haipo na uwekezaji wake kwenye uwanja inabidi uwe more than 13 billions coz kwenye hesabu ya mapato yatakayotokana na uwanja hawataangalia alitoa shilingi ngapi Bali asilimia zake 49 zitazingatiwa.
 
Uwanja sawa, lakini Bilion mbili hapana!

Kwanza nina declare interest, mimi ni Yanga damu, na sijaandika haya kwa sababu mimi ni Yanga, Lah!
Miaka nenda miaka rudi masimango ya wadau wa Mpira kwa timu zetu mbili kubwa ni suala la uwanja, watu wanahoji kwa Club iliyoanzishwa mwaka 11 February 1935 mpaka leo kukodi uwanja wa mazoezi, hii hapana!

Kwa hili bila kumung'unya maneno, nasema kongole kwa wana Simba kama kweli mna dhamira ya dhati ya kuujenga uwanja wenu.
Japo sijui hiyo bajeti ya Bilion thelathini mmeipataje na kujiwekea lengo ilhali hata michoro hamna.

Lakini anyways, hiyo sio ishu kwangu, inawezekana mmeamua kufanya Siri japo najua hamna kitu kama hicho. Kwenye hayo mambo ya umma hakunaga siri coz mwisho wa siku lazima utangaze tenda ili kuipata kampuni ya kuifanya hiyo kazi ambayo ndio itakupa andiko la gharama halisi za ujenzi.

Lakini Kuna ukakasi mkubwa, kiongozi ameamsha kampeni hiyo akiahidi kuchangia Bil. 2, hii kwangu naweka BIG NO.
Kwanza nikuhakikishieni, kimahesabu Inawezekana kabisa kuuujenga uwanja wa Mpira wenye viwango vyovyote kwa michango, asikudanganye mtu eti haliwezekani, akabeza, muache abeze, kwani hata uwanja wa taifa si umejengwa na michango yetu hiyo hiyo iliyobadilishwa tu Jina ikaitwa KODI.

Hesabu rahisi tu, kwani wanachama Milioni nne wa Simba wakilipa Ada Yao ya uanachama kwa mwaka si inapatikana Bilion 48?, tena inavuka na lengo, kwa hili Simba mnaweza msikatishwe tamaa, na hata Yanga wakiamua wataweza, ni suala la kuamua tu!

Sasa nirudi kwenye hoja yangu ya msingi, bwana mkubwa yeye ameahidi kutoa Bilioni mbili, si haba, ni fedha pia na inaweza kuwa msaada mkubwa sana kwenye kampeni ya uhamasishaji uchangiaji!

Lakini shida yangu ni moja tu, hivi kimahesabu hizo Bilioni Mbili si asilimia 7.5 tu ya Bilioni 30?
Yes,sijabahatisha bhana, ni asilimia saba unusu tu.

Sasa kama ni hivyo, watu wa Simba msiogope kuhoji, mimi nakuonesheni njia ya kuanzia kuhoji, huyo Tajiri si inadaiwa amenunua hisa zile 49%?

Sasa kama mlikuwa hamjui ni kwamba kila asset itakayosajiliwa kwa Jina la Simba sports Club asilimia 49% itakuwa ni ya bwana mkubwa, bila kujali hiyo Mali imepatikanaje.

Hii ndio kusema kwamba, hata huo uwanja kama hati yake inasoma au itasoma Jina la Simba SPORTS club, Shea yenu WANA simba ni ile asilimia 51% na 49% inayobaki ni Mali ya bwana mkubwa.

Maana yangu ni kwamba kwa bwana mkubwa kuchangia Bil 2 ya uwanja maana yake amechangia asilimia 7.5 tu lakini kwenye hati za umiliki atachukua 49%,sijui mnanielewa!??
Si juzi mmetangaza mmeingia kwenye mfumo wa hisa na yeye amelipa Bil. 20?

Yaani maana yake zaidi ni kwamba zile 41.5% za umiliki wake katika uwanja zote atanunuliwa na wanachama na wapenzi WA simba,hii haiko sawa bhana, Sasa hapa ndio wale jamaa wa FCC inabidi watumiwe kuhoji kwa sababu tunazungumzia umiliki wa hisa, tunazungumzia biashara hapa ambao mwisho wa mwaka watu inabidi wakae mezani kugawana kilichopatilana na kila mtu atapata kulingana na uwiano wa umiliki wake wa HISA.

LAKINI nisiwakatisheni tamaa, mna hiyari aidha mumnunulie Tajiri wenu hizo Shea 41.5% au mmwambie ukweli bila kumuogopa kwamba huo anaoita mchango si mchango ni fedha za manunuzi ya hisa zake kwenye umiliki wa uwanja wenu, kwa hivyo kiuhalisia wamambo kama ni kuchangia basi achangie hizo asilimia zote 49% ambazo makaratasi ya mahesabu yatamtambua yeye kama mmiliki bila kujali kwamba waliochanga ni mashabiki na wanachama ambao Ada Yao ya mwaka hulipa kwa mbinde na kujinyima, na wakati mwingine hata pesa ya kiingilio kwenye mechi inawashinda.
Ukiamua kutokuelewa shauri zako, na ukibisha ukweli huu we bisha tu!

Daima mbele nyuma mwiko!
Hawawezi kukuelewa,inatakiwa wafanye tathmin ya gharama za ujenzi halafu tajiri yao alipe 49%wanachama watoe jumla 51%.Acha wapigwe kwa chupa ya mirinda.
 
Halafu uamuzi wa kujenga uwanja ulikuja baadaye ya CO kuhimizwa afuate taratibu ambazo alitaka kuzinajisi,ina maana kwenye uwanja wao hakutakuwa na taratibu na kanu
 
Back
Top Bottom