Uwakita: Sasa tutajibu kila tamko la waislamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uwakita: Sasa tutajibu kila tamko la waislamu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 3, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Na Agnes Mwaijega

  UMOJA wa Wainjilisti wa Kikristo Tanzania (UWAKITA) umesema kutokana na vurugu ambazo waislamu wamekuwa wakiwafanyia katika mikutano yao
  watahakikisha wanajibu kila tamko ambalo litatolewa dhidi yao katika makongamano yao nchini.

  Hatua hiyo ilitangazwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa UWAVITA, Bw. Samson Bullegi alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu matukio mbalimbali, aliyosema waislamu wamekuwa wakiwafanyia wakristo nchini.

  "Kuanzia sasa UWAKITA utajibu kila tamko litakalotolewa na waislamu kupitia ama redioni,chombo kingine cha habari au makongamano kwa stahili ile ile watakayoitumia wao, lakini kwa busara," alisema Bw. Bullegi.

  Vile vile umoja huo umeitaka serikali kuwaachia huru wakristo, wachungaji na wainjilisti ambao wamewekwa katika mahabusu ya Polisi Mto wa Mbu kutokana na vurugu zilizofanywa na waislamu Monduli, Arusha kwa madai kwamba hawana hatia yoyote.

  Pia wamelaani kitendo cha Jeshi la Polisi kutokuchukua hatua zinazotakiwa dhidi ya vurugu zinazofanywa na waislamu katika mikoa tofauti pamoja na makongamano ambayo yanawadhalilisha viongozi wa kikristo nchini.

  Hata hivyo, UWAVITA ilisema haina imani tena na Wizara ya Mambo ya Ndani hususan Jeshi la Polisi, hususan muundo wake, kwa kuwa serikali imekuwa haitoi kauli yoyote ya kukemea vitendo hivyo wala kuwachukulia hatua wahusika ambao ni waislamu.

  Bw.Bullegi alitoa mfano wa baadhi ya matukio ya vurugu ambayo yalifanywa na waislamu kwamba ni pamoja na kuvamia kanisa la Anglikana la Nguruka mwaka 2008, AGT Kyala na kufanya uharibifu mwaka 2007, Kimara Baruti mwaka 2003 na Faith Mission lililopo wilayani Chato.

  "Wakristo tumekuwa wavumilivu sana kwa muda mrefu kila waislamu wanapofanya vurugu katika mikutano yetu, sasa hivi tumechoka.

  "Mbaya zaidi hata Jeshi la Polisi ambalo linatoa kibali cha kufanya mikutano hiyo halioneshi ushirikiano katika kipindi chote ambacho waislamu wamekuwa wakifanya vurugu hizo kwenye mikutano ya wakristo," alisema.

  Aliongeza kwamba wanapata wasiwasi wanapoona kwamba matukio hayo bado yanaendelea bila Jeshi la Polisi kuingilia kati.

  Alisema kutokana na uharibifu uliofanywa katika mji mdogo wa Mto wa mbu Februari 26 mwaka huu kimewasikitisha na kuwasukuma kuzungumzia juu ya suala hilo, na hivyo kuitaka serikali kulipa mali zilizoharibiwa.
   
 2. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Uislam ni JINO kwa JINO. Ukristo ni ADUI YAKO MPENDE. Kwa mantiki hii, (it is just a common sense) sishangai naposikia kwamba waislam wamevamia mkutano wa injili na kufanya vurugu. Nitakachoshangaa ni kusikia wakristo wamevamia mkutano wa waislam na kufanya vurugu. Nikisia hivyo, nitapata wasiwasi kama hao kweli ni wakristo.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...