Uwakilishi haramu watishia usalama wa utaifa letu.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uwakilishi haramu watishia usalama wa utaifa letu....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Aug 4, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Aug 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,724
  Likes Received: 415,856
  Trophy Points: 280
  Ukienda Bungeni sifa ya waheshimiwa pale Bungeni ni jimbo la uchaguzi walilojiandikisha na wala siyo mahali ambapo wanaishi.....matokeo yake asilimia zaidi ya tisini ya wabunge wetu ni wakaazi wa Dar-Es-Salaam lakini hujitia kuwakilisha majimbo lukuki mkoani...........................matatizo ya Dar ndiyo wanayoyafahamu na hivyo kuyapigia debe kwa nguvu zote yatatuliwe huku wakijigamba hata wapigakura wao wamewatumwa walisemee jiji la Dar...........................

  Jana nimeona vioja pale ambapo wabunge wameshupalia suala la JK na mtoto wake kupora UDA kupitia kampuni hewa......................na wateule wa JK kama Idid Simba..........wakiwa mstari wa mbele katika uporaji huo..................ni mambo muhimu kitaifa lakini wapigakura wa majimbo ambayo waheshimiwa hawa hujitia kuwa ndiko roho zao zilipo wanakero kibao lakini hazipewi kipaumbele kwa sababu haziwagusi waheshimiwa hawa moja kwa moja...........

  Teuzi za Raisi zinafanyika kwa usiri sana na wala hazina masilahi kwa taifa ila kwa yule anayezifanya kwa sababu viongozi wengi ndiyo wamekuwa mstari wa mbele katika kulipora taifa hili.........................

  tukidai katiba mpya ili kurekebisha kasoro hizi za kimfumo tunaitwa wachochezi na wenye wivu.....................kwa wale ambao hivi sasa ndiyo wanaolitumbua hili taifa.............................

  kwa hiyo Bunge hili na watendaji serikalini katika mfumo ambao siyo shirikishi na siyo wajibikaji nionavyo ndiyo tishio nambari moja la usalama wa utaifa wetu.......................................waonaje??????????????????
   
Loading...