Uwakilishi bungeni 50/50

a.9784

Senior Member
Feb 19, 2008
145
4
Kupitia vyombo vya habari vya Chanel ten na ITV jana tarehe 11 April,2008,wanawake wameomba uwakilishi bungeni uwe ni asilimia hamsini kwa hamsini.Agenda hii ni miongoni mwa malengo yaliyomo katika ilani ya uchaguzi ya CCm ya mwaka 2005.Malengo hayo ni kwamba katika uchaguzi wa mwaka 2010 kama bunge litakuwa na wabunge 330 then 165 wawe ni wabunge wa kiume na 165 wawe ni wabunge wa kike.

Katika kikao kilichofanyika jana pale Ubungo Plaza(Blue Pearl Hotel)Mjadala ulikua mzito juu ya mada hii ya 50 kwa 50.Mapendekezo yaliyotolewa ni kwamba katiba ifanyiwe marekebisho na ikumbukwe kwamba mwanamke mwenzao ambae ni Mary Nagu tena waziri wa sheria na katiba amekwisha bainisha kwamba Muda wakurekebisha katiba bado.Je,leo hii mama huyo yuko tayari kulamba matapishi yake kwa kuwaunga mkono wanawake wenzake?

Hii ni 2008,tumebakiwa na 2009 na 2010 ni uchaguzi mkuu.Hizi Day dreaming zitawezekana kweli kwa 2010 tuwe na uwakilishi wa 50/50?
Lakini jamani naomba tusiwe bayasi kwa hili.Hivi katiba imezuia wanawake wasifikie hiyo asilimia hamsini?Mimi nadhani katiba kwa hapa tunaipa lawama ambazo hazistaili kabisi.Hivi ikitokea mwaka 2010 wanawake bungeni wakawa ni asilimia 60 na wanaume asilimia 40 ni nini kitatokea.

Wadau naomba tulione hili na labda tujadili ni njia zipi zitumike katika kufikia lengo la akina mama hawa.
 
Kama Tanzania tunahitaji maendeleo kinacho hitajika siyo wanawake/wanaume bungeni kinachohitaji ni watu wenye mwelekeo wa kuleta/kuchangia maendeleo.

Lakini kama ni suala la siasa siasa tunaweza kuongeza.
 
mie nnaamini kila ukiengeza uwakilishi wa wanawake bungeni ndio unaporejesha nguvu za utendaji wa bunge nyuma.


ukweli wanawake walio serious na kazi ni wachache sana sasa kulazimisha tu kwa kuiga wenzetu itakuwa hatari sio mzaha.

kama wako serious waingie kwenye vyama vyao wapambane na hilo liko open sio kusubiri tuweke sheria halafu waingie kwa kuteuliwa.

haki ya nani bungeni kutazidi kutiana tu na sio utumishi wa wananchi
 
Kibaya zaidi, wanawake wanapopata nafasi hizo za ubwete wengi kama si wote wanabadilika ghafla na kufikia hata ku DIVORCE waume zao ambao wamekuwa nao katika shida na raha kwa muda mrefu wa maisha yao , mfano halisi waheshimiwa wawili wa viti maalumu wanaotoka mkoa mmoja na (S.S) wamekwisha kimbia waume zao wamejenga nyumba mpya na kuishi peke yao baada ya kuukwaa UHESHIMIWA anaebisha afatilie Inakatisha tamaa
 
Haya ni malengo ya wanawake ...... je, malengo ya nchi ni yapi? Ni wazi kwamba Tanzania inahitaji uwakilishi bora na sio uwiano wa uwakilishi huo. Sitajali bungeni (au uongozi kwa jumla) kukiwa na wanawake wengi zaidi ya wanaume as long as ni uwakishi bora.
Wanawake kutaka tu nusu ya uwakilishi bila kuangalia mahitaji ya nchi ni ubinafsi. Tafadhalini kina mama piganieni usawa katika fursa na si kupigania uwakilishi.
 
Lakini jamani naomba tusiwe bayasi kwa hili.Hivi katiba imezuia wanawake wasifikie hiyo asilimia hamsini?Mimi nadhani katiba kwa hapa tunaipa lawama ambazo hazistaili kabisi.Hivi ikitokea mwaka 2010 wanawake bungeni wakawa ni asilimia 60 na wanaume asilimia 40 ni nini kitatokea.





BUNGE LITAJAA UMBEA,MIPASHO,VIJEMBE NA HAPATAKUWA NA USITAHIMILIVU TUPU NA WANAWAKE wote wanaokimbilia DOM kwa biashara fulani itabadilika kuwa kwa vidume kwenda huko kupiga same business






Mnyonge mnyongeni ila sasaaaaaa,haki yakeeeeee MPENII jamaaa!!ebo
 
Hata wakiwa asilimia 80 tunachohitaji ni viongozi waadililifu, wachapakazi kutufikisha kwenye nchi itkayokuwa ya maziwa na asali
 
Tanzania need viongozi, hizi biashara za kusema tunataka wanawake % ngapi na wanaume naona hazina kichwa wala miguu.

We need viongozi and that is what i cares most
 
Tanzania need viongozi, hizi biashara za kusema tunataka wanawake % ngapi na wanaume naona hazina kichwa wala miguu.

We need viongozi and that is what i cares most
Ikiwa CCM wameweza kuwaweka waimbaji katika nEC unafikiri kwa mwendo huu wa Muungwana si watajazwa wasanii kibao yaani bado hawa MaMiss Tanzania .bado hawajasituka lakini karibu nao watakimbilia huko maana ndio biashara inayolipa kwa muda mfupi unakuwa milioneya au bilioneya na ukiukwaa uwaziri ndio umesharuka maisha ya kusua sua.
 
Hata wakiwa asilimia 80 tunachohitaji ni viongozi waadililifu, wachapakazi kutufikisha kwenye nchi itkayokuwa ya maziwa na asali

Nilitegemea JK angetufikisha huko lakini naona kama anatupeleka kwenye Vumbi na Shubiri. Maziwa na asali vipo kwa ajili ya wachache waliokamatia mpini (((((
 
Back
Top Bottom