a.9784
Senior Member
- Feb 19, 2008
- 145
- 4
Kupitia vyombo vya habari vya Chanel ten na ITV jana tarehe 11 April,2008,wanawake wameomba uwakilishi bungeni uwe ni asilimia hamsini kwa hamsini.Agenda hii ni miongoni mwa malengo yaliyomo katika ilani ya uchaguzi ya CCm ya mwaka 2005.Malengo hayo ni kwamba katika uchaguzi wa mwaka 2010 kama bunge litakuwa na wabunge 330 then 165 wawe ni wabunge wa kiume na 165 wawe ni wabunge wa kike.
Katika kikao kilichofanyika jana pale Ubungo Plaza(Blue Pearl Hotel)Mjadala ulikua mzito juu ya mada hii ya 50 kwa 50.Mapendekezo yaliyotolewa ni kwamba katiba ifanyiwe marekebisho na ikumbukwe kwamba mwanamke mwenzao ambae ni Mary Nagu tena waziri wa sheria na katiba amekwisha bainisha kwamba Muda wakurekebisha katiba bado.Je,leo hii mama huyo yuko tayari kulamba matapishi yake kwa kuwaunga mkono wanawake wenzake?
Hii ni 2008,tumebakiwa na 2009 na 2010 ni uchaguzi mkuu.Hizi Day dreaming zitawezekana kweli kwa 2010 tuwe na uwakilishi wa 50/50?
Lakini jamani naomba tusiwe bayasi kwa hili.Hivi katiba imezuia wanawake wasifikie hiyo asilimia hamsini?Mimi nadhani katiba kwa hapa tunaipa lawama ambazo hazistaili kabisi.Hivi ikitokea mwaka 2010 wanawake bungeni wakawa ni asilimia 60 na wanaume asilimia 40 ni nini kitatokea.
Wadau naomba tulione hili na labda tujadili ni njia zipi zitumike katika kufikia lengo la akina mama hawa.