Uwajibikaji wa Vyombo vya habari wa Tanzania Media Fund Mlimani City

Meneja Mtendaji wa TMF, Ernest Sungura anamkaribisha Naibu Waziri kwenda kukata utepe kwa ajili ya kufungua maonesho hayo ya picha kutoka FTMT
 
Naibu Waziri anaanza kwa kutoa hotuba fupi kwa ajili wageni, anamkaribisha Ernest Sungura kwenye ulingo wa siasa kwa kuwa anaamini anaweza kuwa mwanasiasa mzuri. Kila jema Ernest
 
Dk Fenella Mukangara anasema kwamba serikali haitarajii TMF kuwa chanzo cha uchochezi na uvunjifu wa amani, kwa maana ya kuwafadhiri waandishi kwa habari ambazo zina mrengo wa namna hiyo. Anasema mfuko huu hauwezi kuwa na tija ikiwa utashindwa kutumiwa na waandishi ambao wana weredi na wenye uwezo wa kufanya kazi kwa nia ya kuchochea maendeleo ya Tanzania na watu wake
 
Dk. Fenella anasema serikali inapenda kuona mfuko unatoa nafasi kwa waandishi kuwa na mafunzo ya muda mrefu ili kuwa na waandishi bora. Anasema pia waandishi hao ni vyema pia wakasaidiwa vifaa kama kompyuta, moderm na vifaa vingine muhimu kwa ajili ya kufanya zao kwa ufasaha zaidi
 
Dk. Fenella: Sio kila habari ni habari, habari inayotoka kwa ajili ya uchochezi na uzushi, siyo habari nzuri kwa nchi yetu. Pamoja na TMF kuandika habari nyingi maeneo ya vijijini, lakini kisitumike vibaya. TMF ikitumika vyema, ni chanzo kikubwa sana ncha kusukuma uchumi na maendeleo ya nchi katika kufikia malengo ya Milenia, Mkukuta na maeneo mengine ya kusukuma mbele maendeleo ya Tanzania na watu wake
 
Dk Fenella: Serikali inaamini kuwa mfuko huo ukitumia vyema utaleta maendeleo makubwa siyo vijijini tu, bali nchi nzima. Katika kufanya kazi zake,
 
Dk Fenella: Mfuko unatarajiwa na serikali kuwa utajikita zaidi huko vijijini na kuwapa sauti wale wasiokuwa na sauti kusikika na hatimaye changamoto zao kusikika na kupewa nafasi ya kuwezeshwa.
 
Mgeni rasmi amemaliza hotuba na sasa anakata utepe kuruhusu kuanza kwa maonesho ya picha.
 
Back
Top Bottom