Uwajibikaji wa Taasisi na Mashirika ya Umma.

Mwadunda

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,027
1,707
Katika awamu ya tano kuna dhana imejengeka kuhusu ustawi wa uwajibikaji wa Serikali, ila kiukweli hakuna ustawi wa aina yeyote hasa katika swala la huduma kwa wateja, yaani unaingia ofisini kuhitaji huduma fulani ila lugha na muda wa kupata hiyo huduma ni changamoto sana nadhani kwa mwananchi wa kawaida tatizo linakua kubwa zaidi.
Taasisi zinazogusa maisha ya jamii kila siku taasisi za afya ikujumuisha zahanati, vituo vya afya na hospitali, TANESCO, Halmashauri zote, usafirishaji hapa ni Traffic Police na SUMATRA/LATRA, ardhi na nyinginezo nyingi.
Watumishi wa umma na mashirika ya umma tambueni hizo nyadhfa mmepewe na Mungu hivyo tumikieni jamii zenu kwa upendo mkifuata sheria, kanuni na taratibu mlizopewa na msijione mmefika na kuanza kuota mapembe kufanya kazi jeuri sio sawa.
Natamani sometimes tungeishi kama Marekani, South Africa au Northern Korea ukizingua unazinguliwa fasta.
 
Back
Top Bottom