Uwajibikaji wa pamoja, unajenga au unaua demokrasia ndani ya chama? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uwajibikaji wa pamoja, unajenga au unaua demokrasia ndani ya chama?

Discussion in 'International Forum' started by MAMMAMIA, Apr 11, 2012.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mpenzi wa siasa, pengine bado ni shabiki tu, lakini kila nikiona dhana ya uwajibikaji wa pamoja katika chama, huwa ninaiogopa siasa. Pengine bado siielewi vyema dhana hiyo, lakini kwa ufahamu wangu ni kuwa chama kinatakiwa kiwe na kauli moja, asitokee mwanachama wa kupinga kauli au maamuzi hayo. Je kufanya hivyo sio ndio kuganda kule kule kwa "Zidumu fikra za mwenyekiti?"
  Ninaposema ninaiogopa dhana ya "uwajibikaji wa pamoja," hofu yangu ni kulazimishwa kuyasaliti mawazo yangu au kukubali kile nisichokiamini.

  Nimeona mifano ya watu wanaosemwa, kushutumiwa, kuadhibiwa na hata kufukuzwa ndani ya vyama vyao kwa kutokubaliana na maamuzi ya wengi. Wakiwa bungeni au kwenye mikutano yao ya vyama, ikiwa chama kimeamua kuwa na msimamo fulani, lazima wanachama wote watii msimao huo, atakayepinga anapachikwa majina kibao - msaliti, mwenye njama za kuua chama, anatumiwa na vyama vyengine n.k.

  Sasa ikiwa kwa mfano, ndani ya chama/kamati/kikundi... kuna wanachama 100, wamepiga kura kuunga mkono hoja, wanachama 99 wakakubali na mmoja akakataa, hiyo asilimia 99 (na hata kama ingekuwa asilimia 50.1), haitoshi kuyafanya maamuzi ya chama kuwa ni sahihi bila ya kumsulubu huyu mmoja aliyekataa? Kuna ubaya gani kwa huyu mmoja, hata akatangaza hadharani kuwa "Chama changu kimeamua na ninaheshimu maamuzi hayo lakini mimi sikukubaliani nayo?" Na anaposema hakubaliani, hana maana ya kudharau au kulazimisha msimamo wake, la, bali ama kwa sababu ya kuwa hakubali kweli, kwa ukaidi wake au kwa kutaka kutumia tu haki yake ya kidemokrasia.

  Wakuu, naomba mnifahamishe dhana nzima ya uwajibikaji wa pamoja na uhusiano, tafauti na athari zake kwa demokrasia.
   
 2. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  MODS, tafadhali naomba muihamishe hii mada hapa muipeleke jukwaa husika.
   
Loading...