Uwajibikaji wa Mbunge kwa Wapiga Kura: Nini kifanyike kuleta ufanisi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uwajibikaji wa Mbunge kwa Wapiga Kura: Nini kifanyike kuleta ufanisi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MsandoAlberto, Apr 27, 2011.

 1. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakati najadiliana na FJM kwenye thread nyingine nimejikuta nikijiuliza je Mbunge anawajibika vipi kwa wapiga kura wake? Ni uwajibikaji wa aina gani pale ambapo Mbunge anawajibishwa kwa kutochaguliwa tena? Mwananchi anakuwa amepoteza nafasi ya muhimu ya kuhoji mambo mengi wakati Mbunge huyo akiendelea kuboronga na kufanya yale ambayo hajatumwa na wananchi au kuendeleza yale ambayo chama chake kinataka.

  Ni mambo gani yafanyike au utaratibu gani uwekwe wa kuwahoji na kuwawajibisha wabunge ambao wanashindwa kutekeleza wajibu wao? Je ni wapi Mbunge anakuta kipimo cha ufanisi wa kazi yake?

  Hali ya sasa ni kusubiri Mkutano wa hadhara kumuuliza Mbunge maswali. Maswali ambayo mara nyingi unakuta hayamuhusu Mbunge badala yake ni wajibu wa serikali ambao haujatekelezwa. Majibu anayotoa Mbunge hayaridhishi. Pia Mbunge anatumia hadaa kuwalaghai wananchi Kwa mfano, atatoa zawadi za madawati, atasaidia kwaya, atatoa laki kwa kina mama, elfu hamsini kikundi cha vijana, madaftari kwa wasioona, walkman kwa viziwi. Pia atatoa msaada wa kompyuta moja kwa wanafunzi mia nne!!

  Je anawajibika vipi? Ni chombo gani kinaweza kumwajibisha Mbunge anayeshindwa kutekeleza wajibu wake? Nini kifanyike?

  Mawazo yenu yatasaidia kuanzisha mjadala mpana zaidi ili tuweze kubadili hali ya ungozi ndani ya nchi yetu. Mbunge akiwajibishwa lazima atamuwajibisha waziri na serikali kwa ujumla. Wakiendelea kuendekezwa wataendeleza porojo na usanii.

  Angalizo, katika hili hakuna cha CCM, CUF wala CHADEMA, TLP au NCCR. Ni wote. Wote lazima wawajibike kwa hiyo tuchangie bila ushabiki wala ufuasi wa vyama.
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Cardinal rule - Wabunge ni wawakilishi wa wananchi na wanawajibika kwa wananchi hivyo lazima record ya utendaji wa kila mbunge –ndani ya bunge ujulikane kwa wapiga kura wake.

  Kila mbunge lazima awekewe voting recording yake bungeni kwenye mambo yote ya msingi. Hii itampa mwananchi picha halisi dhidi ya mbunge wake na muhimu zaidi itamfanya mwananchi kutathmini kama mbunge wake anafanya maamuzi kwa msukumo wa ki-itikadi yaani chama anachotoka au/na kwa kuzingatia maslahi ya wapiga kura wake.

  Nchi kama Marekani na Uengereza kuna wakati mbunge au wabunge toka chama tawala (vice versa) wanakwenda kinyume na chama chao mara pale wanapoona kuwa hoja fulani haikubaliki kwa wapiga wake (jimboni kwake). Wengi hufanya hata a quick poll au wanapiga simu wa baadhi ya wapiga kura ili kusoma upepo unavuma vipi (just to be sure) maana akienda kinyume na matarajio ya wapiga kura wake basi atakuwa na kibarua kigumu sana kuelezea maamuzi yake.

  Nitoe mfano. Katika Bunge lililopita hivi majuzi (April session) tuliona mjadala mkali kati ya wabunge wa upinzani wakiongozwa na Mh. Tundu Lissu kwa upande mmoja na wale wa wabunge wa CCM wakiongozwa na mwanasheria wa Serikali na Mh Waziri Celina Kombani. Hii ilikuwa kuhusu uwepo wa wakuu wa Mikoa na Wilaya kwenye kamati za kusumamia nidhati katika utendaji wa Mahakama za Mikoa na Wilaya. Na hoja ya Mh. Lissu ilikuwa ni kulinda uhuru wa Mahakama – mmoja wa mhimili mkuu wa dola kama ilivyo kwenye katiba. Hata hivyo, wote tuliona wabunge wote wa CCM waliokuwa ndani (na waliongia) walipiga kura kumuunga mkono Waziri Celina Kombani wakati wale wa Upinzani waliunga mkono marekebisho ya Lissu.

  Sasa, tukurudi kwa wananchi jambo la kumuuliza hapa ni je Mbunge wako anaelewa na kuamini kwenye dhama ya ‘separation of powers'? Na alipigaje kura kwenye huu mswada? Kwamba alisema NDIYO wanasiasa wafuatilie utendaji wa mahakama? au alisema HAPANA – mahakama ipewe uhuru wake kama ilivyo kwenye katiba? Hivyo hivyo wabunge wanaweza kuhojiwa kuhusu mambo mengine ili kupata misimamo yao mfano maazimio ya tume ya Mwakyembe n.k.

  Hili likitiliwa maanani, nina uhakika litapunguza sana hii tabia ya ‘naunga mkono hoja mia kwa mia' na hata UMAMLUKI Utakoma maana wabunge (wote bila kujali chama) watajuwa wanawajibika kwanza kwa wanachi ndio mambo ya chama yanafuata. Na linapokuja swala zima la chama, mara pale wananchi watapokuwa na nyenzo hii ya kuhoji wabunge wao basi vyama vitalizimika kutengeneza hoja ambazo hata zikiuungwa na mkono na wabunge wao basi hazitawaletea shida. Hivi ndivyo nchi za wenzetu wameweza kuwawajibisha wabunge wao – ni kwa kuhakikisha kuwa wanafualia maamuzi, msimamo na vote ya wabunge wao wakati wakiwa bungeni. Pollig/survey business zinapata kazi sana maana hakuna chama/kiongozi anataka kubahatisha juu ya public reaction kwenye mambo fulani fulani.

  Najua wabunge wengi ni wa viti maalum kwa hiyo wanaweza kujiona kama hawana wa kuwahoji. Lakini tukumbuke wabunge wa viti maalum wanawakilisha vikundi/taasisi fulani. Mfano. Wako walipata viti maalum –NGOs, Vijana, Vyama vya wafanyakazi n.k. Kwangu mimi hayo ndiyo majimbo ya hao waheshimiwa kwa hiyo wahojiwe huko. Infact hawa ndio watakuwa na wakati mgumu maana watapamba na wanaharati.

  Mchango wa JF kwenye hili ni muhimu sana ukizingatia kuwa si wote wanaweza kupata record za utendaji wa wabunge wao kirahisi. JF wanaweza kuweka ukurasa maalum (special page) ya bunge ambayo kwenye kila mswaada muhimu basi michango na upigaji kura uwekwe (KWA MAJINA – FULANI KAPIGAJE KURA KWENYE a, b c...). Sina shaka kuwa humu JF kuna wanahabari wazalendo ambao wanaweza wakawa wanatoka ‘periodical' record kuhusu hawa waheshimiwa.

  Vyama vya siasa navyo kupitia mitandao yao (website) wanaweza kutoa results ya maaumuzi, michango na voting ya kila mbunge wake (kwa majina). Kwa kufafanua ni kwamba mfano, CCM wangeweza kutoa list ya wabunge wao wote namba walivyopiga kura kwenye miswada bungeni, CDM nao wakafanya hivyo. etc

  Naomba niishie hapo kwa leo.
   
 3. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  FJM, thank you very much kamanda. These thoughts is what we need. The funny thing is one will receive limited input when it comes to issues such as this. Lots of comments will be posted on trivial issues such as kujivua gamba etc.

  Ni muhimu sana kuamua jinsi ya kuwawajibisa wabunge ili waweze kutekeleza wajibu wao. Kuwepo na sheria inayomlazimisha Mbunge kutoa taarifa ya utendaji wake kwa wananchi.
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145

  Msando tuhamasishane humu Jamvini walau ifikapo July basi mwenendo wa bunge ufuatiliwe kwa mtindo huo. Nina idea nyingine ya namna ya kusambasa habari nitaiweka hapa kwa muda muafaka. Cha muhimu tusiruhusu tena wabunge ku-abdicate thier role ya kusimamia serikali na kutunga sheria kwa manufaa ya vizazi hivi na vijavyo. Watu wanalala bungeni. aibu gani hii?
   
 5. Scolari

  Scolari JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2011
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 273
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Msando,

  Umeibua hoja muhimu sana.

  Kwanza, kuna haja ya wananchi kufahamu kwa upana majukumu ya mbunge. Kwani wanaweza kuhoji suala ambalo halipo katika majukumu ya mbunge na kuacha kuhoji lile ambalo linapaswa kuomba kabisa.

  Baada ya kufahamu majukumu hayo, wanapaswa kukumbuka ahadi ambazo kiongozi huyo alizitoa ili wazihoji.

  Wanapaswa kuangalia ushiriki wake katika vikao vya bunge na halmashauri.

  Njia nyingine zinaweza kutengenezwa kupima utendaji.

  Nimeona katika facebook: kuna vijana wameanzisha jukwaa la Mbunge wako kafanya nini: Login | Facebook ni moja ya majukwaa ya kutoa taarifa katika utekelezaji na kuhakiki utendaji.

  Tunapaswa kubuni njia nyingi zaidi na zaidi. Pia kuhamasisha wananchi kuhoji na kufatilia utendaji huo.
   
 6. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mkuu Msando inabidi wapiga kura waandae Job description na waingie mkataba na mbunge wao wa jinsi ya kuisimamia na kuitekeleza
   
 7. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hmethod, ni kweli. Kwa utaratibu tulio nao Mbunge ndie anayepanga nini atafanya. Anaahidi wakati wa kampeni na mara baada ya hapo anaacha yale aliyoahidi anafanya yake.

  Job description itasaidia. Wakati wa kutoa shukrani inabidi iwe kipindi cha wananchi na Mbunge kukubaliana job description!
   
Loading...