Uwajibikaji wa Kiongozi Kwa Mwananchi

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Nimewahi kuandika hatua kadhaa juu ya utekelezaji wa kazi kwa viongozi wetu, hasa waliotokana na UKAWA hususan ni Chadema, hawa ni wenyeviti wa serikali za mitaa/Vijiji, Madiwani, na wabunge.

Nilichokiangalia zaidi ni namna bora ya utekelezaji wa shughuli zao, kuwa na baseline data, kupanga mpango mkakati wa muda mrefu ,kupanga mpango kazi na mpango wa utekelezaji.

Leo katika kuendeleza maoni, mjadala na Mada hiyo. ..nitaongelea zile halmashauri za wilaya na manispaa zinazoongozwa na Ukawa, hususan ni Dar es salaam ambapo ni moja ya jiji lenye changamoto nyingi.

Mada hii ya namna bora ya utendaji kazi kwa viongozi wetu nitaihusianisha na mpango wa uwezeshaji wananchi kiuchumi, ambapo kwayo ni pamoja na kuwawezesha vijana kujiajiri, kwani inafahamika wazi nchi yetu ina tatizo kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana waliomaliza elimu ya msingi, sekondari na elimu ya juu.

Nawaomba sasa maeneo ukawa inapoongoza halmashauri basi ni muda wa kuitafsiri kwa vitendo Ilani ya uchaguzi ya UKAWA ,ni muda wa kuyatenda sasa kwa vitendo.

Kwa kurejea program ya kuwawezesha wananchi kiuchumi, ningependa kuwazungumzia zaidi wananchi waliojiajiri katika sekta Isiyo rasmi ambao ndio wengi sana mijini.
Umuhimu wa sekta inayojumuisha wajasiriamali mali wadogo na wakati wanaongozwa na sera yaani Small and Medium Enterprise Policy ya mwaka 2003(SME policy 2003) ni pamoja na kutoa mchango mkubwa katika pato la taifa, Kuongeza thamani ya mazao, Ina nafasi kubwa ktk kutoa ajira, huchangia kupunguza umasikini nk

Lakini pamoja na umuhimu huo kumekuwa na tatizo kubwa maeneo ya mijini, mfano mkubwa ni jinsi wamachinga ambavyo wamekuwa wakihangaika, makundi mengine ya vijana wa seremala, gereji, mama/baba lishe nk
Hawa wote ni kundi lililo ktk Sekta Isiyo rasmi ya ajira. Tumeona jinsi wamamchinga walivyokuwa wakifukuzwa, kukamatwa, kupigwa mabomu, nao kujibu mashambulizi, tumeona jinsi mama/baba lishe walivyokuwa wanakamatwa na migambo wa Jiji, tumeona jinsi vibanda mbalimbali vilivyobomolewa na mgambo wa Jiji, tumeona jinsi maeneo ya makundi ya vijana wa magereji na seremala walivyobomolewa na kufukuzwa kwenye maeneo mbali mbali nchini hususan jiji la Dar es salaam.

Ongezeko la vijana wengi maeneo ya mijini (Rural-Urban Migration) limesababishwa na vijana wengi kukimbilia mijini kutoka vijijini kwa kusaka fursa, kusaka ajira, hii ni kwa sababu ajira inayopatikana vijijini ambayo ni kilimo imekuwa ngumu kutokana na mvua zisizo za uhakika, huduma zingine duni vijijini zinasabisha vijana kuhamia mijini. ...nilitarajia Sera ya mipango miji (Urban planning policy) ingeweza kuwa suluhisho kwa vijana wanaoamua kutafuta fursa mijini, nilitegemea policy implication iwe to support job creation agenda lakini imekuwa kinyume chake.

Hivyo natarajia manispaa tunazoziongoza hasa Dar es salaam, Mbeya, Arusha tutekeleze mpango wa kuwawezesha wananchi kiuchumi ambapo mpango huu utazalisha ajira, utaongeza kipato, utapunguza umasikini ,utachangia pato la taifa, Endapo tu manispaa kwenye full council tutaweka maamuzi na kuyasimamia mabadiliko hayo kwa msingi kwamba sekta hii isiyo rasmi sio shughuli haramu (Non Illegal sector )

Manispaa ziko chini ya TAMISEMI, hivyo basi tushirikishe wizara mbali mbali kuhakikisha tunawasaidia makundi ya wananchi yaliyoko kwenye sekta Isiyo rasmi, ambayo ni kundi kubwa sana.

Mfano natarajia madiwani wetu hawaji na utaratibu uliokuwa ukitumiwa na ccm wa kuwaona wamamchinga ni haramu, (Illegal business,ila tu kipindi cha uchaguzi. Sitarajii kuona mgambo akivamia masufuria ya mama/Baba lishe na kuyataifisha (Stock confiscation),Sitarajii vijana wataachwa scattered bila muongozo na kuwahamisha kujiunga pamoja na kutenga economic groups.

Natarajia madiwani watawabana mipango miji, watumie taaluma zao na jukumu lao la kupanga miji ili

1.suluhu endelevu (Sustainable solution) juu ya tatizo la maeneo ya kufanyia biashara ipatikane, na hii itasaidia kuondoa tatizo la wajasiriamali kukosa maeneo ya kuendeshea shughuli zao
●Lengo ni kumaliza tatizo la bomoa bomoa linaloathiri sekta Isiyo rasmi (curb lack of business premises subject to demolition) linaloendeshwa na manispaa zetu
●Kuondoa tatizo la kutokutambilika na mamlaka za miji (Curb the problem of Recognition in local planning)
●Kutaondoa tatizo kupoteza mitaji yao kwa kukosa maeneo ya kufanyia shughuli zao au wanapokuwa jela au mahabusu
●Kuwafanya watambulike kwa kupata leseni na hivyo kulipa kodi ambayo itaongezeka mapato ya serikali.

2 . Natarajia wananchi watakaokuwa wamehamasishwa kujiunga kwenye vikundi watasaidiwa kupata mikopo yenye masharti nafuu, kiwango nafuu cha Riba (favorable interest charge) ambapo imekuwa kikwazo kwa wajasiriamali na wengine wanaotaka kuanzisha shughuli ya kiuchumi.

3 . Natarajia kuona tatizo la ukosefu wa ujuzi (skills) kwa wajasiriamali mali linashughulikiwa, kwa kuwa link na Wizara ya elimu na ufundi kupitia associated agency ambae ni VETA,
●Pia wizara ya viwanda na biashara kupitia associated agency wake ambae ni SIDO, nako watapata skills mbali mbali

4 . Natarajia tatizo la upatikanaji wa leseni na vibali vya mazao ya misitu hususan ni Mbao kwa ajili ya vijana wanaojishugulisha na useremala linafanyiwa kazi haraka ili serikali ikianza kununua madawati ya mashuleni, na kwa kupitia Pruvate Public Partnership (PPP) basi wanufaike.

Kwa leo naishia hapa tukutane next time
Niwatakie kazi njema ya kuwatumikia wananchi

Kwilasa E.
 
Back
Top Bottom