Uwajibikaji na maamuzi tata ya serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uwajibikaji na maamuzi tata ya serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Obi, Dec 30, 2010.

 1. Obi

  Obi JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2010
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 376
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Serikali ya CCM imebobea katika kufanya maamuzi yasiyo na tija kwa Taifa tofauti na yale wanayoyahubiri. Ukisikia ikihimiza uwajibikaji na uchapakazi kwa bidii unaweza kuingia kwenye kosa la kiufundi kuamini kwamba ndivyo inavyotaka kuendesha mambo yake. Kwa muda mrefu maamuzi ya serikali ya awamu ya nne yamegubikwa na ghilba na chuki miongoni mwa watu wachapakazi na wapenda maendeleo na wale wasiopenda maendeleo ndani ya taifa hili. Kila anayeonekana kuchapa kazi kwa bidii huangaliwa kwa jicho la chuki na hatimaye ataundiwa mkakati wa kumwaangamiza. Nitatoa mifano michache.
  Mheshimiwa, Dr. John Magufuli. Hakuna ubishi kuwa huyu mheshimiwa ni mtu mchapa kazi na mpenda maendeleo. Utendaji kazi wa Waziri John Magufuli, ambaye katika utawala wa awamu ya tatu, akiwa naibu waziri wa ujenzi na hatimaye waziri kamili, kwa aina ya utendaji wake, ilikuwa ni kupoteza muda na rasilimali kuthubutu kumuondoa katika nafasi hiyo. Akiwa katika nafasi hiyo, Magufuli amejitofautisha kabisa na wote walioweka kuongoza wizara ya ujenzi kuanzia Basil Mramba; Andrew Chenge na baadaye Shukuru Kawambwa. Ingekuwa si ghilba za CCM kwa kuamua kupoteza muda wa mchapakazi kama Magufuli kwa miaka mitano, hakika leo tusengekuwa tunazungumza aina ya masongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
  Vilevile hakuna ubishi kuwa yaliyomkuta alikuwa spika wa Bunge Samwel Sitta kutoswa kwenye kinyang’anyiro cha uspika kwa kizingizio cha kutaka spika mwanamke ni kielelezo cha kusema “tunataka uwajibikaji” kumbe sivyo, ni chuki na gilba miongoni mwa wasiopenda maendeleo wa taifa hili. Sitta aliadhibiwa kwa sababu alionekana kulijenga Bunge lenye nguvu, lililokuwa linaiwajibisha serikali, lililokuwa linaifanya serikali ikose usingizi. Alijenga Bunge lililojaa wawakilishi wa wananchi na ambalo liliifanya serikali ikose usingizi kwa kusimamia uwajibikaji wa serikali kwa vitendo.
  Chuki hizo hizo zimemwangukia aliyekuwa mkurugenzi wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando. TBC chini ya Tido Mhando ilijiendesha kama chombo kilichojali uweledi katika fani ya habari. Hakuna ubishi kwamba Tido alirejeshwa nchini kwa wimbo ule ule wa watawala wetu kwamba wanataka wataalamu waliokimbilia nje kuja kushiriki katika ujenzi wa taifa letu hili change. Aliitikia wito akafanya kazi kwa bidii akiamini watalawa wapo pamoja nae katika kazi anayofanya, kumbe wapi kiama tia maji.
  Huu uwajibikaji unaohubiriwa na watalawa wa nchii hii upo wapi? Wataendeleza chuki na gilba zao mpaka lini kwa watu wachapa kazi na wapenda maendeleo kwa taifa letu?
   
 2. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2016
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,553
  Likes Received: 1,605
  Trophy Points: 280
  Obi

  ili nchi iwe na uwajibikaji na uzalendo inabidi kuwepo na utawala bora, usimamizi wa sheria, ukweli na uwazi ktk maamuzi na utendaji wenye ufanisi serikalini...

  lkn changamoto ni hawa wanasiasa kujihusisha ktk ufisadi na mikataba mibovu pasipo kujari utaifa....
   
 3. MKWEPA KODI

  MKWEPA KODI JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2016
  Joined: Nov 28, 2015
  Messages: 18,241
  Likes Received: 37,192
  Trophy Points: 280
  Maelezo yako ni mazuri sana, ila ongezea kidogo kwamba pamoja na mazuri yote ya samweli sitta alikuja kufanya kosa kubwa sana katika maisha yake na nchi kwa ujumla kwa kutuharibia katiba yetu
   
Loading...