UWAJIBIKAJI: Kuna visima vingapi vimejengwa na CHADEMA kwa mahela ya Sabodo?

Avanti

JF-Expert Member
Aug 24, 2010
1,209
239
Angewahoji wenzake Mh. Zitto hili sijui ingekuwaje?

Anyway hebu tujibuni basi viongozi wetu, kuna visima vingapi? Vipo wapi?

Je, miradi yetu mingine(kama ofisi ya pale Mwenge) aliyotusaidia tuifanikishe imefikia wapi?

Jana wakati napost wengi wetu tulikuwa kwenye shamrashamra za sherehe za Uhuru. Labda leo Kurugenzi yetu ya Habari itajibu maswali haya!

============
SIMILAR CASES:

April 8, 2015

Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) kilipokea jumla ya shilingi za kitanzania billion 2. 5 kama msaada wa ujenzi na uchimbaji wa visima 700.

Pesa hizo zilitolewa na mfanyabiashara Mustapha Sabodo a ajili ya majimbo 25 yanayoshikiliwa na wabunge wa chama hicho mwaka 2011 mwezi November.

Maswali yangu kwa wabunge wa CHADEMA na viongozi wetu ni haya machache tu

1. Viko wapi hivyo visima 700 vyenye thamani ya shilling billion 2.5 katika majimbo yetu 25 ya uchaguzi?

2. Mimi mbunge wangu ni mhe. Mnyika ningependa kujua visima hivyo vipo eneo gani haswa ukizingatia sisi wakazi wa ubungo tuna shida ya maji?

3. Wabunge wa CHADEMA tuleteeni idadi ya visima hivyo katika majimbo yenu na sehemu vilipochimbwa wananchi tufhamu

4. Kama hamna hivyo visima pesa hizo zilitumika katika eneo gani na mtuletee mchanganuao.

Tafadhali, nisitwe msaliti nataka kujua kwa sasabu jana tulikuwa na diwani wetu huku ubungo kilungule akashindwa kujibu hilo swali akataka aulizwe mbunge na viongozi wa kitaifa

October 11, 2016:

Aliyekua mfadhili wa Chama, Mzee Sabodo alishawahi toa msaada wa mamilioni ya fedha kwa CHADEMA kusaidia jitihada za upatikanaji wa maji kwa uchimbaji wa visima katika majimbo yanayoongozwa na wabunge watokanao na chama hicho!

Kama mdau wa maendeleo ningependa kupata mrejesho toka kwa wapenda maendeleo wenzangu, kama kuna dalili zozote za matumizi sahihi ya fedha zilizotolewa kwa shughuli husika!

Napata mashaka kama kuna lolote limefanyika mpaka sasa! Kama lipo basi tungependa kuona tu visima vichache vilivyotokana na fedha zilizotolewa!
 
Kama ukipata majibu hapa ntafikiria vinginevyo kuhusu chama hiki!!!!!!!!!
Kwa sasa fikra yangu ni kuwa hawako makini na sio watendaji wa ki hivyo!!!!


Ni kama mkulima aliyepata mavuno mengi sasa pa kuyaweka shida na mkakati wa kuyafikisha sokoni unasuasua!!!!
 
Visima 1236.

Swali jingine lipo au tufunge thread?

hivi ulivyoandika hata mtoto wangu anaweza.
nitafuatilia huu uzi hadi mwisho kama hamna majibu leo nitajua Tanzania upinzani umekufa rasimi.
Kwanza dr slaa alituahidi kuwa majimbo ya upinzani yatakuwa ya mfano,hilo sijaliona hadi leo
 
hivi ulivyoandika hata mtoto wangu anaweza.
nitafuatilia huu uzi hadi mwisho kama hamna majibu leo nitajua Tanzania upinzani umekufa rasimi.
Kwanza dr slaa alituahidi kuwa majimbo ya upinzani yatakuwa ya mfano,hilo sijaliona hadi leo

Tena Manispaa ya Kigoma madiwani wala rushwa ni wa chama changu CDM! Huwa inaniumiza sana!
 
Umendika nini sasa?

1. Nani anajukumu la kukusanya kodi ......

2. Kwanini tunalipa kodi.......

3. Nani anamiliki mechanism/machinery katika kusimamia maendeleo kwa mujibu wa fedha zilizokusanywa

4. Baada ya uchaguzi utekelezaji unaofanyika ni wa sera za chama cha upinzani au chama tawala.

Ukinijibu haya nitakupa majibu ya swali lako.
 
Thubutu nani wa kujenga visima hapo, ok kwa idadi hiyo mliyotupa tunakubali je location wapi vipo.
 
Balali

Kwa hiyo mmelamba vihela mnataka kusema mliviwasilisha kwa wasimamia maendeleo? Mbona picha zilionesha viongozi wa CDM wakizipokea na hawakuoneshwa wakiziwasilisha kwa watekelezaji wa shghuli za maendeleo (kwenye halmashauri husika n.k).

Pili kuhusu utekelezajiwa sera kuna halamshauri zinazoongozwa na upinzani, mfano halmashauri ya manispaa ya Kigoma, hii inaongozwa na kusimamiwa na CDM, kwa nini nao wanaonekana ni wala rushwa tu?
 
mkuu Avanti huu uzi hatuwezi kupata majibu.wameshaanza kuogopa na pengine watakuita gamba au kijana wa zito
 
Last edited by a moderator:
Dogo umeambiwa Sabodo ndio serikali? Hili lakujenga visima waulize waliotawala zaidi ya miaka 50 wamejenga vingapi full stop!

Pesa ilitoka kwa ajili ya visima na waliochukua walijua haya unayoongea ila wakaamua kuchukua hatua stahiki!!!!!!

Unafuatiliwa utekelezaji wa azma yao njema kabisa!!!!!

Halafu ukiongea weka mikono bana unarusha sana mate
 
mkuu Avanti huu uzi hatuwezi kupata majibu.wameshaanza kuogopa na pengine watakuita gamba au kijana wa zito

...,Ha a a ha a nyie Jamaa mbona mnapga za Chembe tu? Inamaana hamuon sehem nyngne Jaman? Kuwen na huruma japo kdogo!
 
Last edited by a moderator:
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom