Uwajibikaji: Kituo cha Daladala Simu 2000 mnatia aibu

Blandes

JF-Expert Member
Sep 17, 2011
401
228
Kituo ni kichafu sana magonjwa nje nje , Viongozi chukua hatua muone shida ni wapi ipo

IMG_20210811_173532_233.jpg
IMG_20210811_173603_724.jpg
 
Mradi wowote ukisimamiwa na Mtanzania ni sawa hakuna usimamizi kabisa. Wasimamizi na watumiaji wote akili zao ni grade moja. Achana na Simu2000 nenda Uwanja wa Benjamin Mkapa huu unaonadiwa kuwa bora Afrika Mashariki na Kati. Tazama vyoo vya ule uwanja ni aibu sana.

Mechi ya Simba na Yanga raia wanakojoa mpaka maeneo ambayo si rasmi kwa kukojoa. Hakuna maji vyooni, maji yapo kwenye vyoo vyao tu huku kwa mashabiki ni uchafu mtupu. Siku Magufuli anaenda pale ndipo wakajifanya kusafisha vyoo na kuweka miundombinu mipya ila kwa VIP tu.

Kila siku wanakusanya pesa kwa ajili ya uwanja sijui wanaamini uwanja ni pitch!

Mimi nina imani kubwa kuwa "Mtanzania ndiye binadamu mwenye uelewa mdogo sana wa kufikiri"
 
Ile mitaro ya barabarani inatoa harufu mbaya sana afu unakuta mama lishe anauza chakula hapo hapo.
 
... vimiradi kama hivyo wanapeana CCM wenyewe kwa wenyewe unategemea nini? Magamba hawajawahi kuwa smart kwa lolote.
 
Ushawahi kuingia ofisi za CCM? Acha hayo sijui Makao Makuu nenda huko mikoani, utadhani hawajawahi kuiibiia nchi hii
 
Kuna siku nilipigiwa simu ya kwenda kwenye semina wakati nipo pale, bahati mbaya nilivaa pensi. Ikabidi ninunue nguo nikaenda kubadilishia kule, kufika vyoo vimefurika halafu jamaa wanapokea hela tu kama hawana akili nzuri.
Mbona nilighairi!
 
Kuna siku nilipigiwa simu ya kwenda kwenye semina wakati nipo pale, bahati mbaya nilivaa pensi. Ikabidi ninunue nguo nikaenda kubadilishia kule, kufika vyoo vimefurika halafu jamaa wanapokea hela tu kama hawana akili nzuri.
Mbona nilighairi!
Aibu sana
 
Back
Top Bottom