Fahami Matsawili
Senior Member
- Mar 8, 2018
- 172
- 153
Rais wetu Mh. John Pombe Magufuli anaposema Tanzania ni nchi tajiri ila kuna watu wachache walituchezea inawezekana wachache ndio wanamuelewa.
Tanzania ni nchi iliyojaliwa vyanzo vingi vya uvuvi bahari, ziwa, mito na mabwawa lakini kutoka na uvuvi haramu ulioshamili huko nyuma sekta ya uvuvi ilichangia kiasi kidogo kwenye Pato la Taifa lakini kwa jitihada za waziri wetu wa uvuvi Mhe Luhaga Mpina, atunda yameanza kuonekana kwa sasa.
Mchango wa sekta ya Uvuvi katika uchumi wa nchi yetu hasa Ziwa Victoria.
1. Ziwa Victoria limegawanyika katika nchi tatu; Tanzania, Kenya na Uganda.
Upande wa Tanzania ziwa lina ukubwa wa Maji Asilimia ya 49% ya ziwa lote, Nchini Uganda ziwa lina ukubwa wa asilimia ya 45% ya ziwa lote na Nchini Kenya ziwa lina ukubwa wa Asilimia 6% ya ziwa lote.
2. Ziwa Victoria linakadiriwa kuwa na aina zaidi ya 500 za samaki japo tafiti zinasema kwamba 40% ya aina zote za Samaki zilikuwa mbioni kutoweka kabisa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kibinadamu na zile za asili.
4. Shirika la Chakula Duniani (FAO) linakisia kuwa zaidi ya watu 280,000 wanaajiriwa na shughuli za uvuvi zikiwamo wavuvi, waanika samaki, wakaanga samaki, wanunuzi na wachuuzi wa samaki, watengeneza nyavu, wajenzi wa mitumbwi, wafanya matengenezo ya mitumbwi na wachuuzi wa samaki.
5. Wanunuzi Ulaya wanataka minofu mikubwa na siyo ya samaki wadogo au samaki wanaovuliwa kwa njia haramu kama sumu, mabomu n.k. Hivyo soko la samaki lilianguka vibaya huko na kutegemea zaidi soko la Afrika ambalo halikuwa bora kulinganisha na soko la samaki kwa nchi za Asia na Ulaya.
6. Ziwa hili lina zaidi ya visiwa 100 ambavyo hukaliwa na watu na vingine havikaliwi na watu.
7. Ziwa hili ni la kwanza kwa ukubwa barani Afrika na la pili kwa eneo lenye maji baridi duniani baada ya Ziwa Superior la Marekani, lakini pia ni la tatu kwa ukubwa katika maziwa yote duniani
8. Shughuli kuu zifanyikazo katika ziwa hili ni Uvuvi, Usafirishaji, Utalii, Uvunaji wa maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali n.k.
9. “Jumla ya thamani ya biashara ya mazao ya samaki kwa mwaka mmoja kwa Ziwa Victoria katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda inakadiriwa kuwa Shilingi Trilioni 6 wakati Tanzania inapata Shilingi Trilioni 1.6 wakati inamiliki eneo kubwa la ziwa ilhali Uganda na Kenya zinazomiliki eneo dogo zinapata Shilingi Trilioni 4.4 tafsiri yake ni kwamba bado hatujanufaika vya kutosha na Ziwa Victoria”
10. Serikali yetu ya awamu ya Tano chini ya Rais wetu John Pombe Magufuli ilipozindua Operation ya kuzuia Uvuvi haramu wengi walidhani Wavuvi wanaonewa lakini Juzi, Jana na leo nimepita sokoni, beach kuzungumza na Wavuvi, wachuuzi wa samaki na wauzaji wadogo wa samaki ili kujua hali ipoje kabla ya operation baada ya operation ya kuzuia Uvuvi haramu na kuhimiza Uvuvi rafiki ziwa Victoria.
Ushuhuda kutoka kwa wauzaji wa samaki na wachuuzi pamoja na Wavuvi wanasema samaki wanapatikana kwa wingi na wakubwa na bei nzuri wanampongeza Rais wetu John Pombe Magufuli na Waziri wetu wa Uvuvi mhe Luhaga Mpina kwa kazi kubwa waliyofanya kupambana na Wavuvi haram ambao walisababisa samaki kutoweka ziwani na kupatikana kwa Shida na shughuli nyingi za kiuchumi kusimamia kutokana na samaki kupatikana kwa Shida.
Hivyo nategemea mapato yanayotokana na shughuli za kibiashara ndani ya ziwa Victoria kwa mwaka yataongezeka kutoka Wastani wa shilingi Trilioni 1.6 angalau hadi shilingi Trilioni 3.5 kwa mwaka kutoka ziwa Victoria tu kama matunda ya juhudi za serikali yetu ya awamu ya Tano katika kudhibiti Uvuvi haram nchini.
Sekta binafsi imeanza kuinuka na kufufua viwanda vya samaki vilivyosimama kutokana na uhaba wa samaki uliosababishwa na Uvuvi haramu sasa Uvuvi haramu Tanzania umeenda kubaki historia..
Kiwanda cha samaki Prime Catch cha Musoma, Supreme Perch, Tanperch...
Lakini serikali yetu imefuta Ushuru wa Ongezeko la thamani (VAT ) kwa zana za Uvuvi ili zipatikane kwa urahisi na kwa bei nafuu.
Kama injini za kupachika, nyavu za Uvuvi, na vifungashio n.k
Hazi ndio Jitihada za serikali yetu ya awamu ya Tano chini ya Rais wetu John Pombe Magufuli kuhakikisha Uvuvi haramu unabaki historia na nchi yetu inanufaika ipasavyo kiuchumi na sekta ya Uvuvi...
Fahami Matsawili.
Sent using Jamii Forums mobile app