Uvuvi haramu kwa serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais wetu John Pombe Magufuli utabaki historia ziwa Victoria

Rais wetu Mhe John Pombe Magufuli amejitahidi kuhakikisha rasirimali za Watanzania zinalindwa kwa ulinzi mkali madini, misitu, wanyama, Uvuvi, Hifadhi n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
Punguza kujikomba mkuu.
Yaani unajionyesha uduni sana.

Najua maneno haya hutayapenda, lakini ukweli ni kwamba umejionyesha kuwa kuna kitu unakipigania kwa hao unaowalilia.

Yaani hata huna 'sophistication' ya jinsi ya kueleza kitu bila ya kujionyesha unataka utazamwe?

Imenibidi niwe muwazi kwako, kwa sababu nilikuona toka huko mwanzo wa mada yako.
 
Kuhusu jirani kununua mazao na kupeleka nje, hizo ni juhudi kwao, sisi kama watanzania tunapaswa nasi tuwaze mbele kwa kuanza kuweka label na kutafuta wanunuzi nje ya nchi
Sielewi lengo lako ni nini hapa katika mistari hii miwili.

"Kuhusu jirani kununua mazao na kupeleka nje, hizo ni juhudi kwao" - Sioni tatizo kama sheria za nchi yetu zinaruhusu kufanya hivyo na hasa kama mkulima ananufaika na mipango hiyo. Jambo mhimu hapa ni kuwepo na taratibu zinazoeleweka wakati shughuli hizo zikifanyika.
Lakini sioni uwezekano wa kubandika 'lebo' kwenye mali isiyokuwa zao la nchi hiyo ionyeshwe kuwa ni ya nchi hiyo. Hata mlaji akilijua hilo hatapendezwa.

Kuhusu "soko la nje" - inalazimu pia ujuwe kwamba mengi ya mashirika yanayouza bidhaa hizo nje kutokea nchini humo siyo ya nchini. Ni mashirika ya uwekezaji toka nje, kama Barrick anavyouza dhahabu yetu huko nje..

Ninalokubaliana na wewe, ni kuwepo na msukumo kwa sisi waTanzania nasi tujitahidi kuanzisha biashara kama hizo za kuuza mazao yetu nje sisi wenyewe. Ndio maana nasisitizia elimu iwe kipaumbele chetu cha kudumu ili watu wetu wawe na ufahamu wa kuyafanya haya mambo.
 
Umeona hapo ndio utajua walipinga kwa hila sio nia njema walikuwa nayo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama hujawahi kuvua samaki ziwani Rwelu; hujui jinsi uvuviwa asili ulivyokuwa ukifanyika huko nyuma hadi 2004; wala hujui aina (spicies) lukuki za samaki waliokuwa humo ziwa Nyanza kabla ya 1980s, na sabau za kutoweka kwa samaki hao ukilinganisha na livehoods za wananchi wa Ziwa Magharibi huwezi kuja hapa kuhubiri siasa za uvuvi haramu. Fahami Matsawili, this is one of your very empty politics!
 
Punguza kujikomba mkuu.
Yaani unajionyesha uduni sana.

Najua maneno haya hutayapenda, lakini ukweli ni kwamba umejionyesha kuwa kuna kitu unakipigania kwa hao unaowalilia.

Yaani hata huna 'sophistication' ya jinsi ya kueleza kitu bila ya kujionyesha unataka utazamwe?

Imenibidi niwe muwazi kwako, kwa sababu nilikuona toka huko mwanzo wa mada yako.
Toa hoja Ndugu mimi nisikuumize kichwa hoja hujibiwa kwa hoja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tueleze juu ya Rushwa inayoendeshwa na maafisa uvuvi na polizi ktk eneo hili. Tueleze pia michango iliyosemekana kutolewa na wavuvi ili kuwaona viongozi wa wizara. Nahisi kumekuwa na rushwa za kutosha.

Kwa upande wa rasrimali za uvuvi, hapo kuna sayansi tunayotaka utueleze. Lengo ni kupata minofu ya kuuza Ulaya au kulinda rasrimali za ziwa. Je, hao wakubwa wenye minofu watakapokuwa wengi, samaki wengine kama sato hali yao itakuwaje maana samaki wakubwa unaojivunia ni sangara ambao wanakula samaki wa aina nyingine. Unayo taarifa yoyote ya kisayansi au unapiga siasa? Kama hujui, naomba tu uandike kwamba hujui!
Sijaelewa Ulitaka kumaanisha nini Ndugu yangu. Aliyeelewa Tafadhari anisaidie!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijaelewa Ulitaka kumaanisha nini Ndugu yangu. Aliyeelewa Tafadhari anisaidie!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
Utaelewa tu! Umeanza kimakosa kuamini uvuvi ni ziwa Victoria tu!
Hebu jikaze tujadiliane kama una utaalamu maana ulichoandika ni siasa isiyo na ushahidi, hadi unakosea eneo la ziwa chini ya mamlaka ya TZ. Sifa kwa waziri, labda umeanza kampeni tu! Vipi uvuvi wa kutumia solar lamps unaendelea au hapana? Au waziri anatakiwa atemebelee tena mwanza ili akutane na watu mashuhuri? Vumilia.

Umeanza na kichwa cha thrd kinachosema uvuvi haramu utabaki ni historia. Una uhakika hakuna uvuvi haramau leo hii? Eneo lote la ziwa bado linaendesha uvuvi haramu kwa kusimamiwa na maafisa uvuvi. Wakikosana ndo wanajidai kuchoma nyavu.

Baadaye unasema uvuvi haramu ndo uliharibu uvuvi wa ziwa victoria. That is absolutely rubbish! Hujasema juu ya over fishing ya ziwa victoria. Nchi zote zinashindania kuvua bila maelewano. Viwanda ni vingi kuliko uwezo wa ziwa. Na kuna taarifa nyingi za kisayansi ambazo hazielweki hata kwa watendaji wa serikali. Nikuulize au napoteza muda?

Baadaye umebowa kutuambia wanunuzi wa ulaya wanataka minofu mikubwa, so what? hiyo ndo iwe sababu ya enforcement ktk ziwa? btw., where is management?

Mengine ya FAO, idadi ya visiwa, faida za ziwa, nk. haya yamejaza nafasi tu!
 
Rais wetu Mh. John Pombe Magufuli anaposema Tanzania ni nchi tajiri ila kuna watu wachache walituchezea inawezekana wachache ndio wanamuelewa.

Tanzania ni nchi iliyojaliwa vyanzo vingi vya uvuvi bahari, ziwa, mito na mabwawa lakini kutoka na uvuvi haramu ulioshamili huko nyuma sekta ya uvuvi ilichangia kiasi kidogo kwenye Pato la Taifa lakini kwa jitihada za waziri wetu wa uvuvi Mhe Luhaga Mpina, atunda yameanza kuonekana kwa sasa.

Mchango wa sekta ya Uvuvi katika uchumi wa nchi yetu hasa Ziwa Victoria.

1. Ziwa Victoria limegawanyika katika nchi tatu; Tanzania, Kenya na Uganda.

Upande wa Tanzania ziwa lina ukubwa wa Maji Asilimia ya 49% ya ziwa lote, Nchini Uganda ziwa lina ukubwa wa asilimia ya 45% ya ziwa lote na Nchini Kenya ziwa lina ukubwa wa Asilimia 6% ya ziwa lote.

2. Ziwa Victoria linakadiriwa kuwa na aina zaidi ya 500 za samaki japo tafiti zinasema kwamba 40% ya aina zote za Samaki zilikuwa mbioni kutoweka kabisa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kibinadamu na zile za asili.

4. Shirika la Chakula Duniani (FAO) linakisia kuwa zaidi ya watu 280,000 wanaajiriwa na shughuli za uvuvi zikiwamo wavuvi, waanika samaki, wakaanga samaki, wanunuzi na wachuuzi wa samaki, watengeneza nyavu, wajenzi wa mitumbwi, wafanya matengenezo ya mitumbwi na wachuuzi wa samaki.

5. Wanunuzi Ulaya wanataka minofu mikubwa na siyo ya samaki wadogo au samaki wanaovuliwa kwa njia haramu kama sumu, mabomu n.k. Hivyo soko la samaki lilianguka vibaya huko na kutegemea zaidi soko la Afrika ambalo halikuwa bora kulinganisha na soko la samaki kwa nchi za Asia na Ulaya.

6. Ziwa hili lina zaidi ya visiwa 100 ambavyo hukaliwa na watu na vingine havikaliwi na watu.

7. Ziwa hili ni la kwanza kwa ukubwa barani Afrika na la pili kwa eneo lenye maji baridi duniani baada ya Ziwa Superior la Marekani, lakini pia ni la tatu kwa ukubwa katika maziwa yote duniani

8. Shughuli kuu zifanyikazo katika ziwa hili ni Uvuvi, Usafirishaji, Utalii, Uvunaji wa maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali n.k.

9. “Jumla ya thamani ya biashara ya mazao ya samaki kwa mwaka mmoja kwa Ziwa Victoria katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda inakadiriwa kuwa Shilingi Trilioni 6 wakati Tanzania inapata Shilingi Trilioni 1.6 wakati inamiliki eneo kubwa la ziwa ilhali Uganda na Kenya zinazomiliki eneo dogo zinapata Shilingi Trilioni 4.4 tafsiri yake ni kwamba bado hatujanufaika vya kutosha na Ziwa Victoria”

10. Serikali yetu ya awamu ya Tano chini ya Rais wetu John Pombe Magufuli ilipozindua Operation ya kuzuia Uvuvi haramu wengi walidhani Wavuvi wanaonewa lakini Juzi, Jana na leo nimepita sokoni, beach kuzungumza na Wavuvi, wachuuzi wa samaki na wauzaji wadogo wa samaki ili kujua hali ipoje kabla ya operation baada ya operation ya kuzuia Uvuvi haramu na kuhimiza Uvuvi rafiki ziwa Victoria.

Ushuhuda kutoka kwa wauzaji wa samaki na wachuuzi pamoja na Wavuvi wanasema samaki wanapatikana kwa wingi na wakubwa na bei nzuri wanampongeza Rais wetu John Pombe Magufuli na Waziri wetu wa Uvuvi mhe Luhaga Mpina kwa kazi kubwa waliyofanya kupambana na Wavuvi haram ambao walisababisa samaki kutoweka ziwani na kupatikana kwa Shida na shughuli nyingi za kiuchumi kusimamia kutokana na samaki kupatikana kwa Shida.

Hivyo nategemea mapato yanayotokana na shughuli za kibiashara ndani ya ziwa Victoria kwa mwaka yataongezeka kutoka Wastani wa shilingi Trilioni 1.6 angalau hadi shilingi Trilioni 3.5 kwa mwaka kutoka ziwa Victoria tu kama matunda ya juhudi za serikali yetu ya awamu ya Tano katika kudhibiti Uvuvi haram nchini.

Sekta binafsi imeanza kuinuka na kufufua viwanda vya samaki vilivyosimama kutokana na uhaba wa samaki uliosababishwa na Uvuvi haramu sasa Uvuvi haramu Tanzania umeenda kubaki historia..

Kiwanda cha samaki Prime Catch cha Musoma, Supreme Perch, Tanperch...

Lakini serikali yetu imefuta Ushuru wa Ongezeko la thamani (VAT ) kwa zana za Uvuvi ili zipatikane kwa urahisi na kwa bei nafuu.
Kama injini za kupachika, nyavu za Uvuvi, na vifungashio n.k

Hazi ndio Jitihada za serikali yetu ya awamu ya Tano chini ya Rais wetu John Pombe Magufuli kuhakikisha Uvuvi haramu unabaki historia na nchi yetu inanufaika ipasavyo kiuchumi na sekta ya Uvuvi...

Fahami Matsawili.


Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa hivi hali ikoje
 
Back
Top Bottom