Uvuvi haramu kwa serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais wetu John Pombe Magufuli utabaki historia ziwa Victoria

Fahami Matsawili

Senior Member
Mar 8, 2018
152
250
Rais wetu Mh. John Pombe Magufuli anaposema Tanzania ni nchi tajiri ila kuna watu wachache walituchezea inawezekana wachache ndio wanamuelewa.

Tanzania ni nchi iliyojaliwa vyanzo vingi vya uvuvi bahari, ziwa, mito na mabwawa lakini kutoka na uvuvi haramu ulioshamili huko nyuma sekta ya uvuvi ilichangia kiasi kidogo kwenye Pato la Taifa lakini kwa jitihada za waziri wetu wa uvuvi Mhe Luhaga Mpina, atunda yameanza kuonekana kwa sasa.

Mchango wa sekta ya Uvuvi katika uchumi wa nchi yetu hasa Ziwa Victoria.

1. Ziwa Victoria limegawanyika katika nchi tatu; Tanzania, Kenya na Uganda.

Upande wa Tanzania ziwa lina ukubwa wa Maji Asilimia ya 49% ya ziwa lote, Nchini Uganda ziwa lina ukubwa wa asilimia ya 45% ya ziwa lote na Nchini Kenya ziwa lina ukubwa wa Asilimia 6% ya ziwa lote.

2. Ziwa Victoria linakadiriwa kuwa na aina zaidi ya 500 za samaki japo tafiti zinasema kwamba 40% ya aina zote za Samaki zilikuwa mbioni kutoweka kabisa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kibinadamu na zile za asili.

4. Shirika la Chakula Duniani (FAO) linakisia kuwa zaidi ya watu 280,000 wanaajiriwa na shughuli za uvuvi zikiwamo wavuvi, waanika samaki, wakaanga samaki, wanunuzi na wachuuzi wa samaki, watengeneza nyavu, wajenzi wa mitumbwi, wafanya matengenezo ya mitumbwi na wachuuzi wa samaki.

5. Wanunuzi Ulaya wanataka minofu mikubwa na siyo ya samaki wadogo au samaki wanaovuliwa kwa njia haramu kama sumu, mabomu n.k. Hivyo soko la samaki lilianguka vibaya huko na kutegemea zaidi soko la Afrika ambalo halikuwa bora kulinganisha na soko la samaki kwa nchi za Asia na Ulaya.

6. Ziwa hili lina zaidi ya visiwa 100 ambavyo hukaliwa na watu na vingine havikaliwi na watu.

7. Ziwa hili ni la kwanza kwa ukubwa barani Afrika na la pili kwa eneo lenye maji baridi duniani baada ya Ziwa Superior la Marekani, lakini pia ni la tatu kwa ukubwa katika maziwa yote duniani

8. Shughuli kuu zifanyikazo katika ziwa hili ni Uvuvi, Usafirishaji, Utalii, Uvunaji wa maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali n.k.

9. “Jumla ya thamani ya biashara ya mazao ya samaki kwa mwaka mmoja kwa Ziwa Victoria katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda inakadiriwa kuwa Shilingi Trilioni 6 wakati Tanzania inapata Shilingi Trilioni 1.6 wakati inamiliki eneo kubwa la ziwa ilhali Uganda na Kenya zinazomiliki eneo dogo zinapata Shilingi Trilioni 4.4 tafsiri yake ni kwamba bado hatujanufaika vya kutosha na Ziwa Victoria”

10. Serikali yetu ya awamu ya Tano chini ya Rais wetu John Pombe Magufuli ilipozindua Operation ya kuzuia Uvuvi haramu wengi walidhani Wavuvi wanaonewa lakini Juzi, Jana na leo nimepita sokoni, beach kuzungumza na Wavuvi, wachuuzi wa samaki na wauzaji wadogo wa samaki ili kujua hali ipoje kabla ya operation baada ya operation ya kuzuia Uvuvi haramu na kuhimiza Uvuvi rafiki ziwa Victoria.

Ushuhuda kutoka kwa wauzaji wa samaki na wachuuzi pamoja na Wavuvi wanasema samaki wanapatikana kwa wingi na wakubwa na bei nzuri wanampongeza Rais wetu John Pombe Magufuli na Waziri wetu wa Uvuvi mhe Luhaga Mpina kwa kazi kubwa waliyofanya kupambana na Wavuvi haram ambao walisababisa samaki kutoweka ziwani na kupatikana kwa Shida na shughuli nyingi za kiuchumi kusimamia kutokana na samaki kupatikana kwa Shida.

Hivyo nategemea mapato yanayotokana na shughuli za kibiashara ndani ya ziwa Victoria kwa mwaka yataongezeka kutoka Wastani wa shilingi Trilioni 1.6 angalau hadi shilingi Trilioni 3.5 kwa mwaka kutoka ziwa Victoria tu kama matunda ya juhudi za serikali yetu ya awamu ya Tano katika kudhibiti Uvuvi haram nchini.

Sekta binafsi imeanza kuinuka na kufufua viwanda vya samaki vilivyosimama kutokana na uhaba wa samaki uliosababishwa na Uvuvi haramu sasa Uvuvi haramu Tanzania umeenda kubaki historia..

Kiwanda cha samaki Prime Catch cha Musoma, Supreme Perch, Tanperch...

Lakini serikali yetu imefuta Ushuru wa Ongezeko la thamani (VAT ) kwa zana za Uvuvi ili zipatikane kwa urahisi na kwa bei nafuu.
Kama injini za kupachika, nyavu za Uvuvi, na vifungashio n.k

Hazi ndio Jitihada za serikali yetu ya awamu ya Tano chini ya Rais wetu John Pombe Magufuli kuhakikisha Uvuvi haramu unabaki historia na nchi yetu inanufaika ipasavyo kiuchumi na sekta ya Uvuvi...

Fahami Matsawili.

20200514_175522-1.jpeg
FB_IMG_1589479953697.jpeg
20200514_180148-1-1.jpeg
20200512_110559.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
6,476
2,000
9. “Jumla ya thamani ya biashara ya mazao ya samaki kwa mwaka mmoja kwa Ziwa Victoria katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda inakadiriwa kuwa Shilingi Trilioni 6 wakati Tanzania inapata Shilingi Trilioni 1.6 wakati inamiliki eneo kubwa la ziwa ilhali Uganda na Kenya zinazomiliki eneo dogo zinapata Shilingi Trilioni 4.4 tafsiri yake ni kwamba bado hatujanufaika vya kutosha na Ziwa Victoria”
Katika mambo nisiyotaka kumlaumu Rais Magufuli ni kama hili, la kuhakikisha raslimali zetu tunazilinda na kuzitumia kutunufaisha.

Hili ni jambo ambalo sina tatizo nalo kwake, isipokuwa katika namna na baadhi ya njia za utekelezaji zinazotumika. Watu wanaumizwa huko chini, hata kama yeye hajui yanayofanyika. Mara nyingi si lazima iwe hivyo, na pale inapolazimu kutumia mabavu, watu waelewe umhimu wa kufanya hivyo.

Kuna hili uliloliweke kwenye taarifa yako; juu ya mapato yaliyokuwa yanapatikana kutokana na uvuvi huko ziwani.

Hao jamaa, jirani zetu, hasa huyo wa mwisho uliyemtaja, sasa hivi analia ile mbaya.
Hawa jamaa hawana aibu. Wanakuja kuvuna kwako huku wakitukana na kulazimisha wavune. Sasa hivi wamebanwa sawa sawa na mapato yao kutokana na uvuvi ziwani yameporomoka kwa zaidi ya nusu (nimejaribu kutafuta takwimu nikuwekee hapa, lakini sijui niliziweka wapi - nikizipata nitaziweka).

Uganda walikuwa wananufaika na kahawa yetu. Hawa wengine ndio walikuwa wanazoa kama hawana akili..., hadi madini, ngozi, vitunguu hadi wanakuja kuweka mikataba na wakulima wetu, wananunua mazao yangali shambani, wakivuna yanapelekwa kuwekwa lebo yao na kusafirishwa nje, kama mali yao.

Haya tusikubali yarudi tena hata utawala ukishabadilika.

Simpigii Kampeni Rais Magufuli, kwa sababu kuna mambo yamsingi ameyaharibu sana, kiasi cha kwamba kubaki kwake kama atayaendeleza hayo, nchi itaharibika sana.

Lakini, endapo kama uchaguzi huru utafanyika, na waTanzania kwa hiari yao wakiamua aendelee, basi binafsi ningeomba ageukie kilimo na elimu.

Katika kilimo ni hawa vyama vya ushirika ndio wanaotakiwa wavurugwe kabisa na kutiwa adabu. Wanadhoofisha sana juhudi za wakulima kujikwamua kutoka kwenye umaskini.

Ingependeza zaidi aanze hata leo. Hii miezi iliyobaki awe amevinyoosha kabisa hivi vyama vya majizi.
 
JOHNKEKE

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
969
1,000
Nakumbuka wanasiasa walivyopinga kiujumla zoezi la kupiga vita uvuvi haramu, kwamba halina manufaa yeyote na halitaleta manufaa.
Baada ya zoezi na wavuvi kufurahia manufaa makubwa yaliyopatikana, wanasiasa hao na vyombo vya habari vilivyokuwa vinatumika wote kimyaaa
 
magu2016

JF-Expert Member
Oct 8, 2017
2,458

Wanasaccos wa.CDM wanakuja kupinga na hili.
 
Fahami Matsawili

Senior Member
Mar 8, 2018
152
250
Nakumbuka wanasiasa walivyopinga kiujumla zoezi la kupiga vita uvuvi haramu, kwamba halina manufaa yeyote na halitaleta manufaa.
Baada ya zoezi na wavuvi kufurahia manufaa makubwa yaliyopatikana, wanasiasa hao na vyombo vya habari vilivyokuwa vinatumika wote kimyaaa
Umeona hapo ndio utajua walipinga kwa hila sio nia njema walikuwa nayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fahami Matsawili

Senior Member
Mar 8, 2018
152
250
Wee jamaa umeimba sana mapambio ya kusifu na kutukuza ukililia nafasi za uteuzi. Unahangaika kweli ndugu hata utendaji wa kijiji usipate.
Na wewe unaekashfu na kutukana uteuzi wako lini mkuu au wewe umejitolea kutukana na kubeza mwenyewe kama ni hivyo why not na mimi isiwe hivyo nafanya kwa hiari bila kutegemea hayo mawazo yako Ndugu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fahami Matsawili

Senior Member
Mar 8, 2018
152
250
Katika mambo nisiyotaka kumlaumu Rais Magufuli ni kama hili, la kuhakikisha raslimali zetu tunazilinda na kuzitumia kutunufaisha.

Hili ni jambo ambalo sina tatizo nalo kwake, isipokuwa katika namna na baadhi ya njia za utekelezaji zinazotumika. Watu wanaumizwa huko chini, hata kama yeye hajui yanayofanyika. Mara nyingi si lazima iwe hivyo, na pale inapolazimu kutumia mabavu, watu waelewe umhimu wa kufanya hivyo.

Kuna hili uliloliweke kwenye taarifa yako; juu ya mapato yaliyokuwa yanapatikana kutokana na uvuvi huko ziwani.

Hao jamaa, jirani zetu, hasa huyo wa mwisho uliyemtaja, sasa hivi analia ile mbaya.
Hawa jamaa hawana aibu. Wanakuja kuvuna kwako huku wakitukana na kulazimisha wavune. Sasa hivi wamebanwa sawa sawa na mapato yao kutokana na uvuvi ziwani yameporomoka kwa zaidi ya nusu (nimejaribu kutafuta takwimu nikuwekee hapa, lakini sijui niliziweka wapi - nikizipata nitaziweka).

Uganda walikuwa wananufaika na kahawa yetu. Hawa wengine ndio walikuwa wanazoa kama hawana akili..., hadi madini, ngozi, vitunguu hadi wanakuja kuweka mikataba na wakulima wetu, wananunua mazao yangali shambani, wakivuna yanapelekwa kuwekwa lebo yao na kusafirishwa nje, kama mali yao.

Haya tusikubali yarudi tena hata utawala ukishabadilika.

Simpigii Kampeni Rais Magufuli, kwa sababu kuna mambo yamsingi ameyaharibu sana, kiasi cha kwamba kubaki kwake kama atayaendeleza hayo, nchi itaharibika sana.

Lakini, endapo kama uchaguzi huru utafanyika, na waTanzania kwa hiari yao wakiamua aendelee, basi binafsi ningeomba ageukie kilimo na elimu.

Katika kilimo ni hawa vyama vya ushirika ndio wanaotakiwa wavurugwe kabisa na kutiwa adabu. Wanadhoofisha sana juhudi za wakulima kujikwamua kutoka kwenye umaskini.

Ingependeza zaidi aanze hata leo. Hii miezi iliyobaki awe amevinyoosha kabisa hivi vyama vya majizi.
Rais wetu Mhe John Pombe Magufuli amejitahidi kuhakikisha rasirimali za Watanzania zinalindwa kwa ulinzi mkali madini, misitu, wanyama, Uvuvi, Hifadhi n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
guwe_la_manga

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
1,175

Ushauli mzuri sana
 
guwe_la_manga

JF-Expert Member
Oct 20, 2019
1,175
2,000
Mkuu nashukuru kwa uzi huu
Ila kama hautojali naomba uniunganishe na wavuvi wa dagaa wa bukoba wale maarufu kwa kutokuwa na mchanga
Kama hautojali nakuja pm
Natanguliza shukrani.
 
G.25

JF-Expert Member
Jun 12, 2013
1,284
2,000
Hata mi japo kuna mambo yenye kuudhi ktk uongozi huu wa awamu ya tano, lakini pia kuna mambo mengi mazuri aliyoyasimamia mh. Raisi.

Mojawapo ni kuhusu rasilimali za nchi yetu, hata kama hajafanikiwa sana lakini tumeona dhamira ya dhati"

Hivi idadi ya tembo wetu ukilinganisha na utawala uliopita ikoje?
Rais wetu Mhe John Pombe Magufuli amejitahidi kuhakikisha rasirimali za Watanzania zinalindwa kwa ulinzi mkali madini, misitu, wanyama, Uvuvi, Hifadhi n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
 
sblandes

JF-Expert Member
Apr 25, 2010
4,505
2,000
Mhh kuna unafuu,lakini wavuvi wakitanzania wamesajiri mitumbwi yao Uganda.
Wanachofanya wanavua katika eneo la Tanzania na kuuza huko Uganda.
Wanafanya hivyo kwa kuwa wanajua Tanzania haina kikosi cha polisi cha majini kijulikanacho kama Police Marine.
Enzi za Jemedari Mkuu Mwl.Nyerere Kulikuwa na meli nyingi za police zikifanya patrol 24/7
Weka police patrol boats za kutosha zina kazi muhimu nyingi Search and Rescue, Pollution control, Antipiracy, Illegal fishing etc.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom