Uvunjifu wa amani nchini.

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
3,409
0
Kuwakamata wahusika wa makundi haya si
suluhisho la kudumu, makundi haya
yalikuwepo muda yanaendelea kuwepo na
yatazidi kuongezeka endapo hatuta hangaikia
chanzo cha tatizo, si Dar pekee kwani hata
baadhi ya mikoa kuna makundi kama haya.
Mara kuna makundi mawili pia, ambayo ni
Jamaica Moto na Mbio za Vijiti.
Nianze kwa kusema, nilaani vikali tabia na
mienendo yote ya makundi haya; uporaji,
ubakaji na mauaji.
Lakini, kwanini watu hawa wameamua kupora
watu kubaka pamoja na kuua? kwanini vikundi
hivi vinaundwa maeneo ambayo yanaonekana
kuwa na uwepo wa watu wengi zaidi wa hali ya
chini? Je, ukisikia majina kama panya road au
mbwa mwitu unapata picha gani kichwani?
Unadhani hawa ni watu wa kada gani?
Matajiri? Maskini au watu wa kada ya kati?
Ukiona mtu anaumwa kichwa ukampa panadol,
kichwa kitapoa kwa muda lakini badae
kitaendelea kuuma tena. Ukiona mtu anaumwa
kichwa ukajaribu kujua chanzo cha kichwa
chake kuuma na kujua kuwa tatizo ni homa,
ukimtibu homa basi mtu huyu kichwa chake
hakitauma tena.
Si kwamba napinga juhudi za serikali za
kuwakamata wahusika wa makundi haya kwa
kuamini kuwa ndio suluhu ya tatizo hili,
hapana, hiyo si njia mbaya kwasasa lakini
tunapaswa pia kuangalia zaidi kwanini vijana
hawa wanafanya wanachofanya. Je, ni tamaa ya
maisha? umaskini? ajira? chuki? au kukosekana
kwa maadili?
Mtazamo wangu binafsi ni kwamba, vijana
hawa wanasumbuliwa na umaskini uliokithiri
unaosababishwa na wao kukosa ajira
sambamba na kukosekana kwa mitaji ili
wajiajiri. Vijana hao ambao wamefika mahali
hawaoni kesho yao, hawajui hatima ya maisha
yao imefikia hatua wamekata tamaa na
wakaona "liwalo na liwe".
Siku zote maskini akikata tamaa ni wazi kuwa
hakutakuwa na amani katika eneo husika.
Suluhisho la kudumu ni kufufua viwanda ili
vijana hawa na wote wanaofanana na hawa
waende wakafanye kazi huko, yafungiliwe
mashamba makubwa vijana hawa wapate ajira,
kwa kuwa vijana wengi hawakopesheki (hawana
vigezo vya taasisi za kifedha) itafutwe njia
mbadala na salama ya kuwakopesha vijana
hawa. Maisha yakiboreshwa tatizo hili
litapungua kwa kiasi kikubwa sana na hatimae
kubaki historia lakini tukitumia njia ya kusubiri
wafanye matukio kisha wapelekwe magereza
huko wataenda kukutana na majambazi sugu
wanaojua kutumia silaha za kivita,
watafundishana mambo makubwa zaidi na
baada ya kutoka yawezekana wakaunda
makundi ya kigaidi kama Bokoharam, Al-
shabaab na mengineyo.
Namaliza kwa kusema kuwa suluhisho la
kudumu juu ya makundi haya ya uvunjifu wa
amani ni kupunguza umaskini uliokithiri na
kutengeneza mazingira rafiki ya vijana kujiajiri
wao wenyewe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom