Uvunjifu wa Amani CCM, mbona NEC na IGP mpo Kimya?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,797
71,217
Tulisikia maonyo Makali makali toka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi NEC na mkuu wa Polisi IGP kuhusu vurugu na kuchafua amani ndani ya vyama wakati huu wa uchaguzi kunako weza kuharibu amani lakini pamoja na kuona ofisi za vyama vya upinzani zikichomwa moto, msafara wa mgombea urais ukipigwa mawe kwa ushahidi wa wazi wa muandaaji ni nani na kubwa kuliko yote ni la fujo zinazoleta ugomvi hadi kupirushiana matofali ndani ya CCM na sio hao walio toa kauli kuonekana Kukemea.

Je, fujo na kuharibu amani kukifanywa na CCM maonyo yale hayawahusu? Au CCM wao ni ruksa kufanya lolote ndani ya nchi hii na sio NEC au IGP mwenye uwezo wa kuwakemea? Ndivyo alivyo agiza "mzalendo #1" na Amiri jeshi wetu?
 
Hiyo ya ofisi za chadema kuchomwa moto nyie endeleeni kuchoma hizo ofisi zenu na mmwambie huyo bwabwa wenu kuwa hizo mbinu zake alizokuja nazo toka kwa hao vibaraka wake hazitafanikiwa. Hatuko tayari kuchafua amani ya nchi yetu sisi hatuna pa kukimbilia yeye ataenda alikokuwa.
Mkipewa misaada wanakuwa watamu Sana, huwezi endesha nchi bila ushirikiano wa kimataifa hasa kwa nchi tegemezi Kama hizi, kataeni kuomba hiyo misaada, magari Kila siku ni DFP, DFPA.
 
Hiyo ya ofisi za chadema kuchomwa moto nyie endeleeni kuchoma hizo ofisi zenu na mmwambie huyo bwabwa wenu kuwa hizo mbinu zake alizokuja nazo toka kwa hao vibaraka wake hazitafanikiwa. Hatuko tayari kuchafua amani ya nchi yetu sisi hatuna pa kukimbilia yeye ataenda alikokuwa.

Hahaha yan watu wanaamini kuwa side ya upinzani ni kukaribisha machafuko
 
Kwani hukuona police pale na watu walikamatwa,
Au ulitaka mpewe taarifa chadema?
 
Hiyo ya ofisi za chadema kuchomwa moto nyie endeleeni kuchoma hizo ofisi zenu na mmwambie huyo bwabwa wenu kuwa hizo mbinu zake alizokuja nazo toka kwa hao vibaraka wake hazitafanikiwa. Hatuko tayari kuchafua amani ya nchi yetu sisi hatuna pa kukimbilia yeye ataenda alikokuwa.

kwanini wasikamatwe hao wanaochoma ofisi hata kama ni CHADEMA wenyewe?

POLIS kazi yao nn sasa?
 
Matendo ya kihuni wanayofanyiwa Chadema nchi hii huku pakiwa na jeshi la polisi yanasikitisha sana. Kila siku Sirro anasema anataka amani wakati wa uchaguzi, lakini haoni ofisi za Chadema zinazochomwa moto kila siku, haya mambo yanashusha hadhi ya jeshi letu la polisi.

Sirro na vijana wako badilikeni sasa.
 
Hiyo ya ofisi za chadema kuchomwa moto nyie endeleeni kuchoma hizo ofisi zenu na mmwambie huyo bwabwa wenu kuwa hizo mbinu zake alizokuja nazo toka kwa hao vibaraka wake hazitafanikiwa. Hatuko tayari kuchafua amani ya nchi yetu sisi hatuna pa kukimbilia yeye ataenda alikokuwa.
" Hatuko tayari kuchafua amani ya nchi yetu ".

Ndio tayari mshachafua amani ya nchi kwa kutupiana matofali. Ama hili unalizungumziaje kiongozi?
 
Tulisikia maonyo Makali makali toka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi NEC na mkuu wa Polisi IGP kuhusu vurugu na kuchafua amani ndani ya vyama wakati huu wa uchaguzi kunako weza kuharibu amani lakini pamoja na kuona ofisi za vyama vya upinzani zikichomwa moto, msafara wa mgombea urais ukipigwa mawe kwa ushahidi wa wazi wa muandaaji ni nani na kubwa kuliko yote ni la fujo zinazoleta ugomvi hadi kupirushiana matofali ndani ya CCM na sio hao walio toa kauli kuonekana Kukemea.

Je, fujo na kuharibu amani kukifanywa na CCM maonyo yale hayawahusu? Au CCM wao ni ruksa kufanya lolote ndani ya nchi hii na sio NEC au IGP mwenye uwezo wa kuwakemea? Ndivyo alivyo agiza "mzalendo #1" na Amiri jeshi wetu?
"Je, fujo na kuharibu amani kukifanywa na CCM maonyo yale hayawahusu? Au CCM wao ni ruksa kufanya lolote ndani ya nchi hii".

Ulevi wa madaraka umewafanya hao watu wajione ndio wenye nchi, na walio baki wote ni wahamiaji haramu.
 
Hiyo ya ofisi za chadema kuchomwa moto nyie endeleeni kuchoma hizo ofisi zenu na mmwambie huyo bwabwa wenu kuwa hizo mbinu zake alizokuja nazo toka kwa hao vibaraka wake hazitafanikiwa. Hatuko tayari kuchafua amani ya nchi yetu sisi hatuna pa kukimbilia yeye ataenda alikokuwa.
Hii nchi haijawahi kuwa na amani ni uwoga wa Watanzania...
 
kwanini wasikamatwe hao wanaochoma ofisi hata kama ni CHADEMA wenyewe?

POLIS kazi yao nn sasa?
Wakishindwa kuwakamata wakuu wa Polisi wa mikoa na wilaya husika wawajibishwe,ukiwekwa utaratibu wa namna hiyo hautasikia ofisi ikiunguzwa.Hata kama CDM wanachoma ofisi zao wenyewe wanatakiwa kushughulikiwa kwa sababu hata nyumba yako mwenyewe sheria hairuhusu kufanya hivyo.Kila mmoja anatakiwa kutimiza wajibu wake.
 
Sijui wakiamka baada ya hii miezi mitatu hapo oktoba watasema nini?
Labda ndio Yale ya najuta ningejua!
 
Hiyo ya ofisi za chadema kuchomwa moto nyie endeleeni kuchoma hizo ofisi zenu na mmwambie huyo bwabwa wenu kuwa hizo mbinu zake alizokuja nazo toka kwa hao vibaraka wake hazitafanikiwa. Hatuko tayari kuchafua amani ya nchi yetu sisi hatuna pa kukimbilia yeye ataenda alikokuwa.

Hizo mbinu za ulaya mashariki ya zamani za wale madictator ndio mmeiga na kuleta huku karne hii!? Hiyo michezo ilifanyika sana huko, kisha Makada wa vyama tawala walikuwa wanaleta propaganda kuwa wapinzani ndio wanajihujumu, kisha vyombo vya dola hukaa kimya au kujifanya wanafanya uchunguzi kusaulisha wananchi. Hizo ni mbinu za kizee ile mbaya.
 
Back
Top Bottom