Uvunjaji wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uvunjaji wa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Hekima Ufunuo, Jan 19, 2012.

 1. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inapotokea serikali iliyopo madarakani kuvunja katiba ya nchi au mhimili mmojawapo wa nchi kuvunja katiba ni hatua gani zinachukuliwa na ni nani anayechukua hizo hatua? Nahitaji elimu hii kwa sababu kuna matukio ambayo mimi nayaona kama uvunjaji wa katiba ya nchi. Natoa mifana ili muone ni nini mtizamo wangu.

  1. Katiba ya Zanzibar inategea sana katiba ya muungano, ili kuwa na uhalali wa kuibadilisha hasa vipengele ambavyo vinaihusu pia katiba ya muungano ni lazima kwanza urekebishe katiba ya muungano ndiyo ubadili katiba ya zanzibar. Kilichotokea mwaka juzi ni wazi kuwa kinakinzana na katiba ya Muungano. Hili si ni uvunjaji wa katiba ya muungano?

  2. Mwaka jana Chadema wamewafukuza uanachama madiwani wa Arusha, huku nyuma Waziri wa Tamisemi akasema waendelee na udiwani wao, ili hali wamepoteza sifa kikatiba. Je huu si uvunjaji wa katiba?

  3. Mwaka jana NCCR-Mageuzi wamemfukuza mbunge wao wa kigoma kusini uanachama kwa yale wanayoyajua wao. leo bunge linasema linamtambua mpaka mahakama itakapoamua. Lakini katika kesi ya mbunge huyo, hakuna mahali popote ambapo bunge limetajwa. Je huo siyo uvunjaji wa katiba.

  4. Juzi karibu na mwisho wa mwaka CUF wamemfukuza uanachama mbunge wao wa wawi, lugha ya mhimili huu wa kutunga sheria ni ile ile. Kwenye matukio haya katiba inasimamiwa na nani?

  Nipeni elimu jamani.
   
 2. BUBE

  BUBE JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa kuwa kwa katiba ya sasa uwepo wa mgombea binafsi ni kitendawili, na kwa kuwa serikali haijatambua mgombea binafsi, kimsingi endapo chama kimemfukuza mtu na bunge au mahakama kukataa maamuzi halisi ya kichama, bila shaka huo ni uvunjaji katiba. Kimsingi nasikiliza kwa masikio marefu kujua Mahakama itaamua nini kuhusu kina Hamadi Rashid wakati ni mahakama hii hii iliyompiga chini Mtikila baada ya kukata rufaa kuwa suala la mgombea binafsi halipo. Yetu macho, let us wait and see
   
 3. n

  ngokowalwa Senior Member

  #3
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 155
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nadhani Jambo likishaweka mguu mahakamani ni mpaka mahakama itakapotoa ruling ndo maamuzi mengine yatachukua mkondo wake kulingana na maelekezo ya Mahakama
   
 4. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  poa mkuu
   
 5. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Rais wetu Jk alikaa kimya baada ya znz kuvunja katiba
  nakiri jk ni presdent bom sana (janga la taifa)
   
 6. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,394
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Kutokuwepo/kutoruhusu mgombea binafsi ni kukiuka Katiba mpaka leo na mpaka hapo mtakapoifuta Katiba iliyopo sasa. Katiba hii inasema wazi kuwa kila mtu anayo haki ya kupiga na kupigiwa kura, lakini haisemi kuwa ili kupigiwa kura ni lazima uwe mwanachama wa chama chochote cha siasa. Ni wazi hapo watu wazima Majaji wa Mahakama waliteleza.
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Si jambo la kwanza kutokea. Aliwahi kufukuzwa uanachama Bi Naila Majid Jidawi ambaye aliwahi pia kuwa kiongozi wa upinzani bungeni kupitia CUF na mahakama ikatengua maamuzi ya CUF na kuendelea kuwa mbunge kwa amri (jimbo) la mahakama paka lilipovunjwa bunge.


  Kwahiyo hilo si geni hilo.   
 8. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,148
  Likes Received: 2,105
  Trophy Points: 280
  kwa mawazo yangu, kuna uvunjanji wa katiba tena ulio dhahiri karibu kila siku. Na kwa mjibu wa uelewa wangu wa taratibu, chanzo cha kuanzisha democrasia na mgawanyo wa madaraka, ni ili mhimili mmoja ukikiuka katiba (kwani wote wameapa kuilinda), basi mihimili mingine iwajibishe ule uliokosea.

  Haya hatuwezi kuyashuhudia hapa kwetu kwa sababu, suala la mgawanyo wa madaraka halipo, madaraka yote yapo kwa Rais. Ndiye anayetengeneza serikali, ndiye anayeongoza bunge ndiye anaye ongoza mahakama. Hivyo, mfano serikali imekosea katika utendaji wake, wabunge wanatakiwa kuiwajibisha na ikiwezekana kuiangusaha, lakini haliwezi kutokea kwa kuwa mkuu wa bunge anapatikana kwa uamuzi wa rais, rais ndiye anayeamua nani awe speaker, kwani hoja zote za kusulubu hazitapita kamwe.

  Ukisema ukimbilie mahakamani, majaji wote ni wateule wa rais, chochote cha kuisulubu serikali lazima wakipindishe ili kulinda ugali wao.

  haya ndiyo ymepelekea kuwepo kwa polisi wabovu, mahakama mbovu, takukuru wabovu, usalama wa taifa wabovu, kila kitu kibovu kwani mkuu wa kaya kashikilia hayo yote, hakuna wa kumwajibisha mwenzake
   
 9. W

  WildCard JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Hebu someni kifungu hiki toka kwenye KATIBA yetu ya JMT: 71(1)(e).
  -71(1) Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo-
  (e) ikiwa Mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge.
  Katiba haisemi lolote kuhusu Mbunge aliyefukuzwa au kuachishwa uanachama. Tafsiri sahihi ya kifungu hiki inahitajika. Ni Mahakama peke yake yenye kazi ya kutafsiri kifungu hiki ambacho vyama vyetu vinakitumia vibaya.
   
 10. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Naomba nikusaidie hapo.

  Kazi yya chama sio kumfukuza mbunge bali ni kumfukuza uanachama wa mbunge.

  Kwani katina anasema wazi lazima mbunge atokane na chama. sasa asipokuwa na chama basi automatic na ubunge huna.

  Kumbuka chama kina mvua uanachama munge kisha wanatoa taarifa kwa Tue ya uchaguzi na spika kuhusu maamuzi yake ya kumvua uanachama.

  Kisha sheria ndio inachukua mkondo wake wa kuvuliwa ubunge.

  Soma vizuri katiba yenu.

   
 11. W

  WildCard JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Huo ndio ubishi wenyewe. KATIBA yetu haisemi haya uliyoyaandika hapa. Kwenye Katiba yetu hakuna kuvuana, kufukuzana wala kuachishwa. Kuna neno moja tu kwenye kifungu (e): ATAACHA. Mahakama itusaidie kutafsiri neno hili. Wenye vyama vyao wanadhulumu haki za wanachama na kuliingiza TAIFA kwenye gharama za ajabu kwa kodi zetu.
  Maalim Seif nilidhani amejifunza kwa kuwa haya yalishamkuta akapata machungu yake kwa kusaidiana na Hamad huyuhuyu. Leo kupewa nafasi hii ambayo imeshindikana kuiingiza kwenye Katiba ya JMT amesahau kila kitu!
   
Loading...