Uvumi wa tick kuhama na matumizi ya karamu ambayo wino hufutika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uvumi wa tick kuhama na matumizi ya karamu ambayo wino hufutika

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Njowepo, Oct 31, 2010.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nimeamka saa 12:45 nkajiandaa nkapata chai then mida ya saa 3:00 nkawa kanisani kusali na moja ya maombi yangu ikawa kuiombea Tanzania uchaguzi wa Amani na utulivu.
  Then kunako mida ya saa 5:08 nkafika eneo langu la kupiga kura eneo la Chuo cha Tumaini Iringa kituo namba moja.
  Sikukuta ata mtu mmoja zaidi ya wawakilishi wa NEC ambao walinikaribisha vizuri tuu na kupekua jina langu na kulikuta akatick then nikaingia ndani ya darasa.Pia nje kulikuwa na FFU wawili kwa ajili ya ulinzi
  Ndani ya darasa nkakuta watu sita:watatu ni mawakala wa CHADEMA,CCM na watatu anawakilisha muunganiko wa vyama vingine.
  Pembeni kuna mdada wa NEC ambaye alichukua kitambulisho changu na kucrosscheck namba tena.
  Then pembenii yake kuna kidume wa NEC ambaye alichukua pia kitambulisho change na kuandika namba ya kitambulisho katika kila karatasi ie ya ubunge,uraisi na udiwani.
  Nkaenda na ayo makaratasi kwa kijichumba ambapo nkatimiza wajibu wangu na mwishowe mtu wa mwisho ndoo akawa ananielekeza namna ya kukunja then nkaweka kura zangu katika vibox husika na hatiame kuchovya kidole kwa wino.
  Nilipokuwa natoka ndo kuna watu kama watatu nao wakawa wanakuja piga kura
  MY TAKE
  Utulivu ulikuwa wa hari ya juu as hakukuwa na fujo
  Nilipomuuliza kijana mmoja wa NEC kuhusu uchache wa watu akanambia wengi wao waliojiandikisha walikuwa wanafunzi moyoni nkaumia sana bse hawa wamekosa haki yao ya msingi.
  Kuhusu uvumi wa kuwa kwenye kwenye karatasi ya kupiga kura kwenye kibox cha Slaa kuna gundi ambayo ambayo inaweza hamisha tick kama nilivyopata sms asbi.Ikabidi niscartch kama mara tatu kwenye kibox hakukuwa na gundi na ile karatasi ina texture kama ya khaki ivi ila ingekuwa ina texture ya nylon naona ingewezekana wanachosema watu hasa kwa ile karatasi ya uraisi.
  Na ata nilipoikunja bado ile tick haikuhama angalau nkawa na amani ya roho na mwili
  Uvumi mwingine wa kuwa ukitumia karamu yao pale baada ya mda ile tick kwa mpinzani hufutika ivyo nkaenda na karamu yangu nkatick ingawa yao ilikuwepo ni karamu ya speedo amabayo ni ya kawaida tuu.Ila kuna haja ya kucross check maeneo mengine kuhusu huo uvumi
  Poleni kwa wale ambao hawakuyakuta majina yao
  Kwa ujumla mji wa Iringa uko na utulivu wa hali ya juu kinyume na matarajio yangu labda tungoje jioni
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  UCHAGUZI 005.jpg UCHAGUZI 004.jpg katika picha
   
 3. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Speedo iko poa sana tu!!! Haina shida hata....

  Watanzania wameshafanya mabadiliko nahisi kama watu 12 milioni tayari wameshapiga kura hadi sasa!!
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nasikia uchaguzi uliopita ulikuwa unalaziishwa kutumia karamu unayoikuta pale kituoni kwa bahati mbaya sikuwepo nchini ila ni kwa mujibu wa msimamizi wa kipindi icho
   
 5. c

  chanai JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mabadiliko tarayi.
   
Loading...