Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,438
- 1,026
Jamaa akiwa amepiga suti nyeupe,alikuwa akisafiri kwa mguu kuelekea kijijini kwa wakwe zake pamoja na mkewe.Jamaa alibanwa na mkojo lakini akaona uvivu kuchepuka porini kukojoa,akaamua kujikaza mpaka afike.Zikiwa zimebaki hatua 100 kufika ukweni mara wingu zito likafunga na matone mazito ya mvua yakaanza kudondoka.Jamaa akaamua ajikojolee nguoni akiamini mvua itakayomnyeshea itasafisha mkojo wote aliojikojolea.Alipomaliza tu kujikojolea,mvua nayo ikakata hapo hapo tena ghafla akabaki na bonge la ramani kubwa ya mkojo sehemu za mbele ya suruali.