Uvivu wa Vijana unaweza kukwamisha nchi yetu

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
7,273
9,972
Nimesoma takwimu za Tanzania na zinaonyesha Umri wa kati wa Watanzania ni miaka 17-18 hivyo Watanzania wengi ni vijana wadogo. Hizi takwimu ni muhimu sana kwa kupanga mipango ya nchi na ndiyo maana rais Magufuli ali kampeni kwa sera ya elimu ya bure.

Lakini pamoja na changamoto nyingi Watanzania tuna changamoto moja kubwa na ni ukweli kwamba vijana wetu wa siku hizi ni wavivu na hawajitumi kama vijana wa zamani. Mfano mdogo tu wa vijana wa sasa wa wale wa miaka ya 90's. Miaka ya tisini kulikuwa hakuna vyuo vikuu vingi kama vya sasa, kulikuwa hakuna simu za mikononi na mitandao ilikuwa ni ya gharama sana au haipo kabisa. Pamoja na mambo yote hayo vijana wa wakati ule waligoma kukaa chini na kulalamika kila siku na kuanzisha mwamko wao. Vijana wachache walipata nafasi za vyuo vyetu vya wakati ule Mzumbe, Sokoine, Chuo kikuu cha Dar na IFM.

Watanzania wengine wengi walianza kujiuliza watafanya nini na kukatokea mwamko wa kwenda kutafuta maisha nje ya nchi kuliko wakati wakati wowote kwenye historia ya nchi. Huu mwamko haujaletwa wa wazee wala serikali bali ni vijana wenyewe na vijana wengi walienda India, Europe, South Africa, US, Canada, Russia, Turkey, Botswana, Kenya, Uganda na hata Cuba. Hii ilitokana na ukweli kwamba vijana wa wakati ule walikuwa hawakubali kushidwa au kusubiri maendeleo kutoka serikalini.

Na kuna vijana wengi sana waliingia kwenye biashara tofauti Tanzania. Kuna Watanzania walienda mpaka Zambia kuomba viza wakati ubalozi wa US ulipofugwa. Wakati ule kufatuta shule haikuwa rahisi na application watu walikuwa wanatuma kwa DHL wenyewe. Kwasababu Watanzania wengi vijana wa wakati ule walikuwa na uchungu wengine walitengeneza vigezo wenyewe na marafiki zao vya kupata shule, visa ma hata kuazimana nguo ili tu wakaombe viza. Vijana wa siku hizi wana vyuo vya kutosha, mitandao ya kirahisi kiasi kwamba shule siku hizi unatuma kila kitu kwenye internet, mawasiliano rahisi ya emails. Lakini pamoja na yote haya vijana wa siku hizi hakuna mwamko wowote ambao tunauona wa kimaendeleo. Hakuna "radical idea" ambayo vijana wa siku hizi wanao zaidi wa ushabiki wa vichekesho vya kwenye mitandao na kisiasa. Vijana wa siku hizi ni walalamishi kama vile maendeleo ya nchi yamepungua, kama vile technologia imepungua wakati ukweli ni kwamba ni rahisi kwa kijana kufanikiwa sasa kuliko wakati ule wa miaka ya 90's.

Sasa hivi kijana wa miaka 21 ukimpa link kwenye internet ya kufanya application ya chuo hata kama ukimwambia utamlipia ata tafuta sababu za kukukwepa na kujieleza ni kwanini hakupata muda wa kufanya application ingawa yuko kwenye what-up na facebook siku nzima.

Maendeleo hayajifichi wakati ule kila mtu hata wazee waliona mwamko na historia ya Tanzania itakuja kuonyesha kwamba mika ya Tanzania kulikuwa na mwamko kuliko wakati wowote kwa vijana. Ni lazima tukumbuke vijana wengi wa wakati ule ni wale waliomaliza form six miaka 20-22 tu. Sasa pamoja na dunia kufunguka na vyuo vya kifundi kama Veta n.k lakini vijana wetu wanaonyesha uvivu wa ajabu.

Kibaya zaidi ni kwamba vijana wa sasa kwasababu ya technologia kuwa kubwa watashindana na vijana wa dunia nzima sio Tanzania tu maana unaweza kutuma file India wakafanya kazi na kulituma kwako kesho na malipo ukafanya kwenye simu tu bila hata ya kwenda bank!. Na upatikanaji wa Gas tutahitaji vijana ambao wanaweza kushindana na ambao wameweka utamaduni wa kujituma kitu ambacho sasa hakionekani. Vijana wa sasa ni walalamishi sana wanalalamikia Wakenya kufanya kazi wakati ni rahisi tu kujifunza kiingereza kama kweli una nia. Siku hizi vijana hawa wamekuwa watu wa kuombaomba pesa kila siku wakati wenzao wa miaka ile walikuwa hawatafuti watu wa kuomba omba kila siku.

Hivyo msishangae mpaka raisi anasema asiyefanya kazi na asile ni kwasababu uvivu umezidi na badala ya kulalamikia serikali kila siku ni lazima tuelewe vijana wetu ni tatizo pia. Hakuna guarantee kwenye maisha laikini huwezi kukaa tu kila siku na kulalamika kwa serikali maana serikali ya Tanzania haijawahi kuwa tajiri! lakini hawa vijana wanalalamika kama vile serikali za zamani zilikuwa tajiri sana!.

Maendeleo hayataletwa na serikali pekee bali ni lazima tuwe na vijana wenye mwamko na ambao wanataka maendeleo kuliko baba zao. Hivyo ombi langu ni kuwahimiza vijana wetu wawe wachapa kazi "hustle" na sio kushinda kwenye mitandao kila siku
 
Hasa wanaume wa Dar. Hawa siku nzima wanashinda kushabikia team fulani na kinyozi
 
Zamani fursa za ajira zilikuwepo sasa hivi hazipo..vijana wanajua kabisa hata wasome vipi kazi hakuna..wamekata tamaa
 
umesema kweli mkuu, vijana hawajitumi. Tofauti ya vijana wa zamani na wasasa ni kubwa mno na inaonekana wazi wazi. Vijana wa siku hizi wanajiita kizazi kipya.
 
Well said.vijana sasa hivi n ovyo 100%,yaani wanakera sana...!wavivu na walalamishi tuuh.kwa ufupi hawatak kutumia akili yao ata 0.01%.
 
Sina nia ya kuhalalisha uvivu wa watanzania ila mtoa mada kuna mambo yanachanganya. Hao vijana wa zamani unaosema si ndo hawa waliouza madini na rasilimali nyingine za nchi kifisadi? Hao vijana wa zamani si ndo walioua viwanda vyote hadi leo vijana hawana ajira? Vijana wa zamani si ndo waanzilishi wa huu uvivu nna uoga wa kuthubutu kisha kuturithisha? Vijana wa zamani walitumia nguvu nyingi bila akili. Vijana wa Tanzania ya leo wako aggresive sana na pesa kuliko wa zamani. Hao wa zamani ndoto zao zilkuwa mambo madogomadogo. Kuna vitu vya kuiga toka kwao ila mengi waliofanya vijana wa zamani yalikuwa sio ya kimaendeleo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom