Uvivu wa kufikiri ulioanzia katika enzi za Mkapa unazidi kutesa nchi yetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uvivu wa kufikiri ulioanzia katika enzi za Mkapa unazidi kutesa nchi yetu.

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Byendangwero, Mar 10, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Utamaduni wa kuanza kutekeleza mara moja, na bila ya kuhoji, kila ushauri unaotolewa na mashirika ya fedha duniani, ulioanzia katika enzi ya awamu ya tatu ya uongozi, ndio unaotishia kulisambaratisha taifa letu. Wakati wa awamu ya tatu serikali ya Mkapa ilishauriwa na IMF na Benki ya Dunia ya kwamba ili nchi iweze kupiga hatua zaharaka kiuchumi kulikuwepo umuimu wa kuunda tabaka la kati kimapato (middle class), kwa madai kwamba tabaka hilo ndilo litakalochukuwa nafasi ya mhimili wa uchumi kwa kuwekeza na hivyo kuongoza ajira na kipato cha wanzania wengine. Mkapa alianza kutekeleza ushauri huo kwa pupa, kwa kuchukua hatua mbali mbali ikiwa ni pamoja na; kubadirisha mfumo wa mishahara na marupurupu kwa lengo la kupendelea wale wa ngazi za juu, kuuziana mali za umma kwa bei ya kutupwa, na kufumbia macho ufisadi mkubwa wa mali asili ya taifa. Kwa njia hizo rais Mkapa alifanikiwa kuunda katabaka kadogo kakipato cha kati katika muda mfupi. Lakini hata hivyo kinyume na matarajio, watu hao baada ya kuwekeza hapa ndani , kiasi kikubwa cha utajiri wao kimeishia kwenye "offshore accounts". hii ndilo chimbuko la ukosefu wa ajira unaolikumba taifa letu.
   
 2. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2017
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,334
  Likes Received: 22,186
  Trophy Points: 280
  twafwa
   
 3. Galapagosi

  Galapagosi JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2017
  Joined: Apr 21, 2017
  Messages: 2,653
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Mkuu naona leo unachimbua yote cha kale kinadumu.
   
Loading...