Dhamir Ramz
Member
- Jan 13, 2016
- 5
- 9
Fikra ya leo kwa kifupi:
Kwanza: Jana kulizagaa taarifa za Maalim kumuandikia barua Pope Francis ili aingilie kati kutafuta suluhisho la uhuni uliofanyika Oktoba 28 na kuitia Zanzibar katika mkwamo wa kisiasa na kiuchumi.
Kinachozungumzwa sana na wasiojielewa ni kunasabisha udini na utamaduni wa Zanzibar ambao umejengeka kwa misingi ya dini ya kiislamu. Walichosahau hapa ni mambo mawili:
1. Ya kuwa Maalim Seif alifanya hivyo kwa sababu mkubwa wa fitna ya mkwamo huu ni mkatoliki, ambae ni Ben Mkapa. Maalim ameliona hili na kaitumia fursa ya imani ya dini ya Ben Mkapa ambayo inangozwa na Pope Francis kama ni njia ya kumnasihi ajivue na dhambi ya kufitini siasa za Zanzibar.
2. Ya kuwa chama cha CUF kama vyama vyote hakina udini. Hivyo suala la Maalim kumuandikia barua Pope Francis ni njia mojawapo ya jitihada za kidiplomasia anazochukua kutafuta suluhu kwa njia ya amani, na pia ni kuonyesha kwamba anaheshimu dini ambazo yeye mwenyewe sio muumini. Kwa hivyo watu wanaopita wakibeza wanaonyesha wazi kwamba akili zao ni finyu sana na hawana upeo wa kuelewa kwa nini Maalim Seif kafanya hivyo.
Pili: Jana kulitokea kituko cha mwaka pale mzee wa IN BIOLOGICAL, Shaka Hamdu shaka alipoitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutoa taarifa kwamba lile bango (kiukweli halikuwa moja, tuliyaona mawili) eti limetengenezwa na wapinzani kufanya propaganda?!
Hivi ajiulize, imefikiaje tarehe ya juzi 12/01/2016 CCM ngazi ya Taifa kupitia Mkuu wa Mawasiliano ya Umma, Daniel Chongolo, watoe tamko la kuomba radhi kwa picha iliyotengenezwa na wapinzani?! Anataka kutuaminisha kwamba CCM Taifa ni vilaza na hawana wataalam wa ICT ambao wana uwezo wa kupambanua hilo kuliko yeye mtaalam wa IN BIOLOGICAL ?!
Hili la Shaka ni la kichekesho kweli kweli, na inatufanya tuanze kuamini kwamba ule msemo wa “Wamegeuka samaki sasa walana wao kwa wao” tuanze kuulekeza upande wao. Iweje chama kimoja wanakuja na rai mbili tofauti, tena moja kutoka ngazi ya juu kabisa, na nyengine kutoka kwa mtaalam wa ICT kipimo cha IN BIOLOGICAL........
Mwisho, nakutakieni ijumaa njema na mapumziko mema ya mwisho wa wiki.
Ahsanteni.