UVCCM Yawaka Moto; Waraka mzito washushwa


P

Pagan Amum

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2015
Messages
1,762
Likes
3,254
Points
280
P

Pagan Amum

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2015
1,762 3,254 280
WARAKA KWA UVCCM YA SASA NA MCHAKATO WA UCHAGUZI UNAOENDELEA

Na Hassan Bombokojr

Mwaka huu (mwezi December) ni muhimu sana kwa Jumuiya ya Vijana ya CCM (UVCCM). Ni mwezi ambao Jumuiya linaenda kwenye uchaguzi ngazi ya Taifa kwa mara nyingine tena kwa kuwachagua viongozi wakuu akiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya kurithi mikoba ya Ndugu. Sadifa

Lazima tukiri wazi ya kwamba zaidi ya miaka 10 uongozi wa Taifa UVCCM haujakidhi mahitaji na matakwa ya vijana nchini. Nitakuwa sijawatendea haki vijana wenzangu kama sitasema wazi hapa kwamba uongozi huu unaomaliza muda wake chini ya Sadifa ndio umekuwa uongozi mmbovu kuwahi kutokea ndani ya Jumuiya yetu. Hili halipo machoni mwa vijana wengi nchini hata Mh. Rais wetu mpendwa Magufuli aliliona hili na kuyasena wazi wazi akiwa katika kongamano la vijana wa Shirikisho Kigamboni.

Uchaguzi wa mwaka huu 2017 ni muhimu sana kwetu hata kama viongozi tunaoenda kuwachagua wanajitambua ama hawajitambui. Muhimu ni kwamba muelekeo wa Jumuiya yetu utategemea sana maamuzi yetu. Ni dhahiri hii miaka 5 tumekuwa mashahidi wa namna Jumuiya yetu imekuwa ya ovyo. Jumuiya yetu kwa sasa inachangamoto nyingi ambazo zinahitaji akili za pamoja kuzitatua, na katika msingi huo tunahitaji Mwenyekiti atakayeleta vijana wote kwa pamoja kutatua changamoto hizo.

*Tunahitaji Mwenyekiti mwenye uwezo. Tunahitaji Mwenyekiti msomi. Tunahitaji Mwenyekiti imara. Tunahitaji Mwenyekiti mwenye upeo mpana. Na kubwa, Tunahitaji kuwa organized zaidi ili kutatua changamoto zinazotukabili vijana kwa pamoja*.

*Tunahitaji Mwenyekiti ambaye ataamsha hisia za vijana kuhusu Jumuiya, kuhusu utaifa na kuhusu uzalendo na kuhamasisha vijana kufanya kazi kwa manufaa ya Taifa na serikali ya awamu ya tano*.

Wengi wamejitokeza kuomba ridhaa katika nafasi hiyo ya juu, hatua ambayo tafsiri yake ni ukuaji wa demokrasia katika awamu hii, ingawa ukweli ni kwamba ni wachache sana wenye uwezo wa kushika nafasi hiyo. Kama vijana tuna imani kubwa sana na vikao vya Chama vitakavyofanyika hapa karibuni, tuna imani kubwa sana sana na Mwenyekiti wetu wa Chama na kwa kuwa kwake kipaumbele katika utendaji ni Uwezo wa mtu basi niwatoe hofu vijana wenzangu kuwa safari hii tutaletewa wagombea wenye uwezo na kisha tutapata Mwenyekiti bora na mwenye uwezo. Na mwenye dira ya kututoa hapa tulipozamishwa na huu uongozi wa sasa...

Kuna baadhi ya viongozi wa sasa (Mawaziri, Manaibu waziri, RC's) wenye wagombea wao tayari ila niweke wazi tu kwamba watusamehe, kwa sasa ni lazima tujenge Jumuiya yetu ambalo litatumikia vijana wote nchini na sio kutumikia baadhi ya viongozi. Uchaguzi wa 2008 tulishuhudia Jumuiya ikitumika. 2012 mpaka sasa tumeendelea kushuhudia Jumuiya ikitumiwa ovyo na baadhi ya wanasiasa. Sasa 2017 tunasema hapana Jumuiya yetu iachwe huru ili kiitumikie vijana nchini kwa kuhamasisha maendeleo.

Rais Magufuli amefanya na anaendelea kufanya kazi kubwa sana sana inayohitaji pongezi za dhati, hivyo ili kumsaidia ni lazima Jumuiya iachwe huru na wanasiasa wanaopandikiza watu wao wakiwemo viongozi wa sasa wa Jumuiya..

UVCCM inahitaji mabadiliko makubwa ya kimuundo, kifikra na kimfumo. Hatuwezi tena kukubali kukaa miaka 5 mingine bila kuendelea mbele. Kuna nafasi kubwa sana kwetu vijana kuendelea zaidi ya tulipo sasa na hili litatokea tu, kama tukipata kiongozi sahihi, imara, mwenye uwezo, msomi na kubwa zaidi kama tukisikilizana na kuwa na sauti moja.

Ni jukumu letu vijana kusimama na kutembea kifua mbele kwa kumsapoti Rais wetu Magufuli na kutokana na sababu hizo vijana hatuna budi kuliomba vikao husika vya Chama kupitia wasifu wa kila mgombea na kisha kutuletea watu sahihi na wenye uwezo...

*
Ndugu
Comrade Bombokojr
 
Allen Kilewella

Allen Kilewella

Verified Member
Joined
Sep 30, 2011
Messages
9,283
Likes
14,510
Points
280
Allen Kilewella

Allen Kilewella

Verified Member
Joined Sep 30, 2011
9,283 14,510 280
Acha wafu wazike wafu wao!!
 
Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
30,656
Likes
87,071
Points
280
Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2012
30,656 87,071 280
Eti moja ya vigezo vya kumpata mgombea uraisi ni ushiriki wake UVCCM. Msishangae siku Sadifa akija kujadiliwa kama mgombea urais.
 
pepsin

pepsin

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Messages
3,171
Likes
3,949
Points
280
pepsin

pepsin

JF-Expert Member
Joined Apr 23, 2015
3,171 3,949 280
Wekeni watu watakaomtumikia na kumsaidia Dr.Shika angalau kujenga viwanda 30!! Hiyo itapendeza,au vipi? Ila msijidanganye kuweka mtu jasiri,wekeni type za Poleple na JANE Murro!
 
Elli

Elli

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2008
Messages
29,913
Likes
15,372
Points
280
Elli

Elli

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2008
29,913 15,372 280
Acha Wafu wazike Wafu wenzao....
 
M

Maharo

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2016
Messages
2,839
Likes
1,762
Points
280
M

Maharo

JF-Expert Member
Joined Aug 22, 2016
2,839 1,762 280
CCM oyeeeeeeee.
 
B

BRAYANI

New Member
Joined
Dec 21, 2016
Messages
1
Likes
0
Points
3
Age
49
B

BRAYANI

New Member
Joined Dec 21, 2016
1 0 3
Ccm inavijana kweliii?
Maana naona vijana wenye makamo ,,fikira,,dressing code ya weze mpaka think tank zunu za kizee✌✌
 
Automata

Automata

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2015
Messages
1,859
Likes
1,640
Points
280
Automata

Automata

JF-Expert Member
Joined Mar 3, 2015
1,859 1,640 280
Sadifa na genge lake wameiharibu sana UVCCM
 
Mzee wa Masauti

Mzee wa Masauti

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2014
Messages
2,105
Likes
2,132
Points
280
Mzee wa Masauti

Mzee wa Masauti

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2014
2,105 2,132 280
Kiongozi kwenye sifa tajwa hapo juu ndani ya CCM hayupo na hajazaliwa bado!
 
mwayungi

mwayungi

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2017
Messages
1,588
Likes
2,700
Points
280
mwayungi

mwayungi

JF-Expert Member
Joined May 9, 2017
1,588 2,700 280
CCM ni sawa sawa na wachawi
 
Efendi

Efendi

Senior Member
Joined
Aug 23, 2016
Messages
130
Likes
157
Points
60
Efendi

Efendi

Senior Member
Joined Aug 23, 2016
130 157 60
Bora ningejaza mimi fomu ya uwenyekiti uvccm taifa
 
S

stemila

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Messages
779
Likes
320
Points
80
S

stemila

JF-Expert Member
Joined May 25, 2011
779 320 80
Wekeni watu watakaomtumikia na kumsaidia Dr.Shika angalau kujenga viwanda 30!! Hiyo itapendeza,au vipi? Ila msijidanganye kuweka mtu jasiri,wekeni type za Poleple na JANE Murro!
Jamii forum Raha tupu aisee, hapa stress zooote huniisha mie.
 

Forum statistics

Threads 1,249,953
Members 481,167
Posts 29,715,746