UVCCM yatoa tamko kuwa imekosa mwelekeo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM yatoa tamko kuwa imekosa mwelekeo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OgwaluMapesa, Aug 2, 2012.

 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  wana Jf leo tumehudhuria press Confress pale makao makuu ameongea na wana habari na amedai kuwa UVCCM yao imepoteza muelekeo na sasa inahitaji mabadiliko na hili hapa ni tamko lake nimelileta hapa tulijadili.naomba kuwasilisha.


  PRESS STATEMENT


  HOTUBAYA MGOMBEA NAFASI YA MAKAMU MWENYEKITI WA UMOJA WA VIJANA (UVCCM) TAIFA- SANGOGUNGU KASERA

  2August 20112

  Ndg:Wanahabari
  Ndg: wanaUVCCM wenzangu

  Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa naomba kutoa salamu zangu za dhati kwa Watanzania na vijana wenzangu wanchi hii pamoja nanyi waandishi wa Habari kwa kushiriki nami katika safari hiiinayolenga kuunganisha na kujenga hatua za mabadiliko ya maisha ya Vijana waTanzania. Kwa namna ya pekee kabisa niwashukuru na kuwaomba mshikamano vijanawenzangu wa Chama cha Mapinduzi ambao kupitia kwao ninatumia nafasi hii kuomba ridhaa yao ili nipate nafasi ya kuwa chemchem ya mafanikio na mabadiliko katika maisha yetu kwa kuanzia na chama chetu. Leo hii naungana na vijana wenzangu hawa wa ndani ya CCM, kufanya jambo moja kubwa, jambo la kuchukua fomuya kuwania moja ya nafasi kubwa katika jumuiya ya Vijana wa CCM Tanzania. Ninafanya kazi hii leo nikitambua mambo yafuatayo:

  Kwanza, ninalenga kuleta mabadiliko yanayotazama aina ya vijana tuliopo sasa, aina ya maisha tunayoishi na aina ya changanoto zinazotukabili mimi nikiwa mmojawapo.

  Pili kwa upekee mkubwa, nachukua fomu hii nikibaini hali ya vijana huko tulikotoka na , changamoto tulizopitia na hatari inayotukabili mbele kama hatua stahiki hazitaanza kuchukuliwa na vijana wa aina yangu ambao tuna uzoefu wa kutosha wa maisha ya kawaida ambayo yanahitaji nguvu na akili zetu na za wenzetu waliotutangulia katika kuboresha maisha yetu ili tuweze kuwa raia wema katika nchi yetu na wanachama waadilifu wa chama chetu na jumuiya zake.

  Ndugu Waandishi wa Habari;

  Kazi hii ya kuchukua fomu ninayoifanya leo hii na kisha kuanza zoezi la kutafuta kuungwa mkono. Ni kazi inayohitaji ushirikiano mkubwa kwa uongozi wa Jumuiya yetu pamoja na vijana mbalimbali bila kujali itikadi zao za vyama vya siasa. Nasema hivi kwa kutambua kuwa UVCCM ndiyo Jumuiya pekee yenye kubeba taswira na matarajio ya vijana wa Tanzania na ambayo siku zote inatakiwa kusimamia maslahi na matakwa ya vijana wa Tanzania na kwakuwa jumuhia hii ni jumuhia ya chama kinachoongoza si chama tawala .

  Ndugu zangu wanahabari na wana CCM tunafahamu tofauti kati ya kuongoza na kutawala ndio maana nimetumia neno kuongoza, na Kama kazi hii ilikuwa haifanyiki huko nyuma na kama ilifanyika bila kuridhisha, mimi nimeamua kwa moyo mkunjufu kuingia kuonesha namna jumuiya yetu itakavyoweza kuwatumikia vijana wa Tanzaniana kukiboresha chama cha Mapinduzi ili kitambue wajibu wake kwa vijana wote waTanzania na kwa kufanya hivi kiweze kusimamia misingi iliyolijenga Taifa hili na kuachwa na waasisi wa Taifa letu Hayati Baba Wa Taifa na Hayati Rais Karume ambao walilijenga taifa letu katika misingi ya haki, usawa na ustahimilivu.

  Ndugu wana habari; Katika kipindi hiki chakutafuta nafasi ya kuteuliwa kuwa mgombea wa nafasi hii nitabakia kuongozwa na Moto isemayo: Vijana kwanza kwa taifa lenye amani na maendeleo. Bila vijana kuangaliwa na kupewa yale wanayostahiki, ni wazi taifa lenye amani na maendeleo halitakuwepo. Natambua fika kuwa vijana wa Tanzania wanakabiliwa na changamoto kubwa hasa ile inayolenga kubaini ndoto ya maisha yao ya sasa na siku zijazo. Naamini mimi ni mmoja wa vijana hawa ambaye pia ninahitaji kuona vijana walio katika kilimo basi wanaweza kupata soko la mazao yao. Vijanawabeba mikokoteni nao wanafanya kazi hiyo kwa miaka kadhaa na kisha kuboreshaajira zao.

  Vijana wanaosoma basi wanahitimu vema na kupata ajira wanazostahiki na pia walio makazini na waliopata nafasi za kuongoza wanaonesha mfano wakufanya kazi kwa kujituma na kwa bidii ili kuonesha kuwa vijana tunaweza na hatuwezi kuliangusha taifa. Natambua haya ninayoyazungumza ni mambo magumu lakini pia natambua yanahitaji mbinu nyingi ili kukabiliana nayo. Kwa sasa natumia nafasi hii kukiomba Chama changu, kuiomba Jumuiya Yetu ya Vijana kutambua kuwa nina dhamira, nina nia, nina sifa za kutosha, nina uwezo wa kufanya majukumu haya ninayoyaomba na ninafahamu kazi za majukumu haya.

  Tena nina rekodi katika umri wangu huu wa kufanya mambo ya kutukuka ambayo rekodi yake inaweza kutazamwa pote nilipobahatika kutoa utumishi wangu. Kwa namna isiyoonyesha kuyumba naomba kuwaeleza vijana wenzangu kuwa kutokanana mshikamano wa vijana wenzangu kwangu ni wazi tumejiandaa kushinda katika nafasi hii ili tuweze kuleta mwanga wa mabadiliko katika jumuiya yetu na chama chetu katika maandalizi ya chaguzi zijazo. Ndugu wanahabari ninatambua zipo changamoto nyingi zinazoikabili UVCCM na changamoto hizi zinahitaji kiongozi ambaye atakuwa na uthubutu wakuweza kukabiliana nazo, changamoto kuuni kitaswira, kimuundo, kiimani, kimadhumuni kama ambavyo zimehainishwa kwenyekanuni za ummoja wa vijana. Nina maanisha nini ninapozungumzia taswira ya UVCCM.Taswira ya UVCCM Taifa leo siotaswira ya kimapambano.

  Historia yetu ipo wazi jumuiya ya vijana ilishiriki katika mapambano ya kuleta Uhuru, Umoja na mshikamano mtakumbuka wakati TANU Inahangaika na kutafuta Uhuru wa Tanganyika na Afro-Shirazi party ikipambana kuleta Uhuru wa Zanzibar vijana waliunganishwa na jumuiya za umoja wa vijana wa vyama hivi viwili ambavyo ni TANU YOUTH LEAGUE na ASP YOUTH LEAGUE, zinafahamika kazi zilizofanywa na wabeba mizigo wa Kariakoo mfano Mzee Rajabu Diwani, leo UVCCM sio tena yawabeba mizigo, sio tena ya wamachingasio tena ya wakulima ,sio tena jumuiya ya wafanyakazi ni jumuiya ya wafanyabiashara, watoto wa vigogo ama wenyenasaba nao ama rafiki zao, inahitaji viongozi wenye dhamira ya dhati ambao watarudisha jumuiya hii kwa vijana wakitanzania na kurudisha taswira ya kimapambano ambayo ni mapambano ya kiuchumi, kazi ya Uhuru imeshafanyika imebakia jukumu la kuleta Uhuru wa kiuchumi na kuwa kimbilio la vijana wote.

  Ni dhamirayangu ya kugombea nafasi hii ni kuhakikisha awamu ya pili ya mapambano ya kiuchumi ya umoja wa vijana inaanza rasmi. Nafahamu zipo changamoto za kiutawala, kiuchumi na jumuiya kuendelea kuishi kwa kutegemea misaada na Ruzuku kutoka kwenye chama, nafahamu watendajiwana hali mbaya kiuchumi hasa katika mawilaya, nafahamu ofisi zetu za wilaya zina upungufu wa vitendea kazi ni dhamira yangu kubadili mwelekeo wa utendajiwa jumuiya yetu kutoka "Business as usual" kuvalisha skafu viongozi na kuimba nyimbo, kuwa jumuiya yenye dira namwelekeo sahihi wa kuwaunganisha na kumkomboa kijana wa kitanzania.

  Ndugu waandishi wa Habari; Ninafahamu matarajio yavijana wa kitanzania yatafikiwa kupitia CCM imara na CCM inatokana na uimara wajumuiya zake kuwa imara na hili inawezekana kwa kupatikana viongozi Imara na mimi nina amini ni mmoja waviongozi ambao wataifanya jumuiya yetu kuwa Imara.

  Kwa kuhitimisha Hotuba yangu naomba kutoa shukrani zangu kwa Mwenyezi Mungu kwa kunifanikisha kuwananyi hapa, niwashukuru wana familia yangu, marafiki na nyie ndugu zanguwaandishi wa Habari kwa kukubali kujumuika nami kunisikiliza leo. Niwaombe Vijana wenzangu wa CCM kuniunga mkono katika azma hii kubwa niliyo nayo na niwakumbushe tu kuwa, zoezi hili la kuchukua fomu nililofanya hapa leo si langu bali la vijana wote wa Tanzania wakiwakilishwa na Vijana wa Chama cha Mapinduzi.

  Ni imani yangu kuwa, wana UVCCM hawatakubali kuangusha taa hiiwaliyoiwasha kule Rorya mkoa wa Mara wao wenyewe na badala yake wataungana namibega kwa bega ili kuufikia ushindi. Tutapitisha fomu hii pamoja nao, tutachujwa pamoja nao na kisha tutashinda pamoja nao na kisha kuanza kuwaongoza vijana wa Tanzania pamoja nao. Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma atubariki na kutupa nguvutufanikishe azma hii muhimu pamoja. Kidumu Chama cha Mapinduzi

  Asanteni kwa kunisikiliza.

  Mimi Ndg Sango Gungu Kasera- Mjumbe Mkutano Mkuu UVCCM (W) Rorya

  Kauli mbiu
  Mbiu "Vijana kwanza kwa taifa lenye amani namaendeleo''.
   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  wakaulimbokane wenyewe hawa, nitamwambia RAMA.
   
 3. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na mgobea makamu aliyoyasema ni ya kweli kabisa uvccm imepoteza dira ,viongozi wa jumuiya makao makuu na mikoa wamebaki kusubiria vyeo vya kuteuliwa

  Makamu mwenyekiti bara Beno Malisa ameua jumuiya ya vijana, katibu wake Martin angalau kidogo amejitahidi lakini anakwazwa na makundi yanayokitafuna ccm.jumuya ya vijana ya leo haifananni na jumiya iliyokuwa inaongozwa na viongozi makini na majasiri kama akina Dr. Emanuel Nchimbi, John Guninita, Amos makala.

  Kimsingi viongozi wa sasa wa jumuiya ndio wamikifikisha hiki chama hapa kilipofika,wamekuwa ni viongozi wa makundi na wanayashabikia kwa maslahi yao binafsi kuganga njaa. Naipenda CCM na nawahurumia makada wa uvccm jumuiya hii sio jumuiya ya enzi zetu tulikuwa makini na tulikuwa tunakemae ufisadi, UVCCM ya sasa imepakatwa na mafisadi.

  Maudhui ya huo waraka ni mzuri ila sidhani kama jamaa atatoboa kwa ccm nanayohifahamu ,namshauri aje cdm tuendeleze arakati za kumkomboa mtanzania maskini
   
 4. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  bila kuweka majungu this is da best speech na yenye changamoto kwa vijana wenye kuitaji mabadiliko.
  \
   
 5. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,393
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Waacheni wafu wazike wafu wao.
   
 6. a

  andrews JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ​ccm ni ccm hakuna jipya nape yuko wapi?
   
 7. S

  Sessy Senior Member

  #7
  Aug 2, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 118
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mfa maji haishi kutapatapa
   
 8. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na maudhui yaliyomo kwenye waraka,jumiiya imekosa mwelekeo viongozi wame loose sense of direction ,hawana mvuto wamekuwa kero na karaa kwa makada wa uvccm.wanatumia muda mwingi kukibomoa chama wa kukumbatia makundi wamegeuza jumuiya kuwa source of income na vichaka vya ufuska.

  Jumuiya ya akina Beno malisa haifanani kabisa na jumuiya ya akina Emauel Nchimbi,Amos Makala,john guninita,mohamed seif, suka suka, zahor mohamed.lea hii tukimuuliza beno malisa anajivunia kitu ghani alichokifanya akiwa uvccm atajibu nini, Nchimbi aliwaachia uvccm potential asset kuna jengo la uvccm lipo makao makuu lumumba,aliwaacha vijana wakiwa wamoja .jumuiya ya sasa hivi imeparanganyika haijulikani nani kafanya nini na nani kama nani,mkuu wa idara muhimu kama chipukizi na uhamasishaji haeleweki yupo chama ghani na anaeneza nini.

  Uvccm ya sasa imekuwa kama bendi za muziki viongozi hawaogonzwi na itikadi,sio wazalendo, wanaongozwa na njaa na tamaa, ni walevi,washerati .hawafanani na hata kidogo na viongozi wa uvccm wa awali wapo nje ya platform ya chama.
   
 9. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,990
  Likes Received: 2,649
  Trophy Points: 280
  Anatunga single mpya ya kutoka nayo.
   
 10. mndwadage

  mndwadage JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 345
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mnatuona watanganyika mataira eti.!
   
 11. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #11
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Huyu sango anagombea hiyo nafasi, je amepata 'go ahead' kutoka kwa ridhiwani? Otherwize atakuwa anapoteza muda wake, labda awe muislamu...
   
 12. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #12
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Sango Gungu Kasera?
   
 13. b

  bashemere Senior Member

  #13
  Aug 2, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mhh kwani uvccm ni tawi la uamsho?
   
 14. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #14
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,626
  Likes Received: 3,005
  Trophy Points: 280
  Ngoja nimeshamfahamu
   
 15. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #15
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Wenyewe wanamwangalia tu
   
 16. R

  Rorya Member

  #16
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Hongera makamu umeongea kwa machungu. rorya tupo pamoja na wewe
   
 17. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) umeanza kuwasha moto tena baada ya mbio za kuwania nafasi za juu za jumuiya hiyo kuanza kwa mbwembwe na tambo za aina mbalimbali. Wakati jana wanachama wa UVCCM walianza kuchukua fomu, mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti Sango Kasera ametangaza kwamba akifanikiwa ataondoa mtindo wa watoto wa vigogo kutaka kuongoza umoja huo. Sango alisema anatambua kwamba UVCCM katika siku za karibuni umeweza kuwa taasisi inayoongozwa na baadhi ya watoto wa vigogo. Alisema akifanikiwa kushinda atahakikisha anaondoa mfumo uliojengeka na kuurejesha umoja huo katika zama zile za TANU Youth League(TYL) ambao ulikuwa ni wa watoto wa watu wote bila kujali matabaka. Hadi jana, majina ya wanachama waliokuwa wamechukua fomu kwa nafasi ya unyekiti ni pamoja na Thabit Jecha Kombo, Sadifa Juma Khamis na Rashid Simai Msaraka. Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti mbali ya Sango wengine ni Ally salum Hapi na Augustino Matefu, wakati wa Halmashauri Kuu (Nec) ni Theresia Mtewele, Halima Bulembo, Olivia Sanare, Ahmed Nyang'ani na Sango tena. Wengine ni Vaileth Sambilwa, Faidha Salim na Augustino Simwiya, huku kwa upande wa Baraza Kuu Taifa wagombea wakiwa ni Mteweke, Bulembo, Ester Mambali, Sanare, David Mwakiposa, Vaileth Sambilwa na Augustino Simwiya. Akizungumzia mchakato huo, Katibu Mkuu wa UVCCM anayemaliza muda wake Martine Shigella alisema wagombea ndiyo kwanza wameanza kuchukua fomu na kwamba mchakato huo unaendelea. "Wapo ambao wamekwisha chukua na wengine wataendelea kuchukua, Kwa hiyo hadi sasa ninachoweza kusema ni kwamba kila mwenye sifa anakaribishwa kuja kuchukua fomu," alisema shigela
   
 18. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #18
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Ni pandikizi la Ben Saanane wa CHADEMA.Taarifa zote zipo na jinsi walivyoshirikiana kuandaa tamko hili hadi Mgombea wa nafasi ya uenyekiti bwana Thabiti Jecha kombo anashirikiana kwa karibu na Ben Saanane.Kama CHADEMA mnataka kuwa na siasa safi zisizo na uchafu wowote basi fanyeni siasa za kistaarabu.Kulalamika kwamba mnapandikiziwa watu na CCM au usalama ni kukosa hoja ikiwa nyinyi mnafanya hayo hayo.Hii si haki kidemokrasia.Huyo jecha kombo tangu mwaka jana alisemwa hapa kupandikizwa na makada wa bavicha wakiongozwa na saanane kwa sababu zisizofahamika.tamko la huyu sango limebeba maudhui yaleyale ambayo baviha wamekuwa wakituhumu UVCCM kuwa ni watoto wa vigogo.Poor you


   
 19. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Sango kasera ni kijana msomi (ana postgraduate), mwenye kujenga hoja na mpambanaji kwa wale waliosoma naye sekondari umbwe wanamfahamu vizuri sana na hata wanafunzi wote waliosoma uganda wanamkumbuka kwa mchango wake mkubwa sana alikuwa ni Raisi wa wanafunzi watokao nje ya uganda,ingawa kwa upande mwingine kwa sasa kuna hisia kuwa ni usalama fulani...Ally hepi ni kijana pia msomi mwanasheria, mzuri wa hoja ingawa ana matatizo kadhaa mosi ni kijana mnafiki sana wengi watamkumbuka alipokuwa mlimani anamkuta yuko kwenye tv anaongea kusapoti mgomo kwa kutetea maslahi ya wanafunzi akifika chuoni aonekani kwenye maandamano kuna kipindi alikutwa akipokea laki 6 kutoka kwa mkandala (ofisini kwa mkandala ) hivyo ni mtu sii hatari ila ni hatari sana kwa sisi vijana,. ingawa anapigiwa chapuo na riz one ila vijana kwa pamoja tutasimama kidete na hata ikibidi Bavicha wajiandae kutupokea.
   
 20. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #20
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  sio uvccm pekee bali na baba yao pia ccm hakuna muelekeo..bora mvunje chama muanze upya
   
Loading...