Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wameendelea kuongeza kasi ya ushindi wa CCM katika Jimbo la Monduli kwa kukutana na kuwajengea hamasa vijana kutoka makundi mbalimbali kama vile wajasiriamali, wafanyabiashara wa ndizi, wachonga vinyago, madereva bodaboda na bajaji, wanamichezo na wananchi wa rika zote katika jamii kwa kuwataka kumchagua Ndugu Julius Kalanga siku ya Jumapili tarehe 16/09/2018 kwa tiketi ya CCM kuwa mbunge wa Monduli.
UVCCM imewafahamisha vijana na wananchi wengine kuwa Ndugu Julius Kalanga ana uwezo wa kuwawakilisha vizuri bungeni na anatoka katika chama kimoja na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli ambacho ndicho kinachoongoza serikali hivyo ni rahisi kushirikiana na serikali katika kuzitatua kero za wananchi wa Monduli.
Aidha UVCCM imewahakikishia wanawake, wazee na wasichana kuwa hakuna wa kuwabugudhi au kuwatisha wasijitokeze kupiga kura kwani wamejipanga vizuri kuhakikisha chama viongozi na wanachama wao wapo salama wakati wote wa kampeni na baada ya kampeni hivyo wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura na wamchague Ndugu Julius Kalanga kuwa Mbunge wa Monduli.
Timu ya kampeni ya UVCCM inaundwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Musa Mwakitinya, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha na Mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa Ndugu Saitoti Zelothe, Mjumbe wa Baraza Kuu na Mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa Ndugu Joanfaith Kataraiya, Mhe Edwin Sanda Mbunge wa Kondoa Mjini, Mhe Gudluck Mlinga mbunge wa Ulanga Mashariki na Mhe Mariam Ditopile Mbunge viti maalum kundi la vijana akitokea UVCCM.
Ratiba ya kampeni inaendelea....
#JuliusKalangaTenaMonduli #KaziInaendelea