UVCCM yakoleza kasi ya ushindi wa CCM Monduli

M

MASIGA

Senior Member
Joined
Aug 29, 2015
Messages
129
Likes
280
Points
80
M

MASIGA

Senior Member
Joined Aug 29, 2015
129 280 80
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wameendelea kuongeza kasi ya ushindi wa CCM katika Jimbo la Monduli kwa kukutana na kuwajengea hamasa vijana kutoka makundi mbalimbali kama vile wajasiriamali, wafanyabiashara wa ndizi, wachonga vinyago, madereva bodaboda na bajaji, wanamichezo na wananchi wa rika zote katika jamii kwa kuwataka kumchagua Ndugu Julius Kalanga siku ya Jumapili tarehe 16/09/2018 kwa tiketi ya CCM kuwa mbunge wa Monduli.

UVCCM imewafahamisha vijana na wananchi wengine kuwa Ndugu Julius Kalanga ana uwezo wa kuwawakilisha vizuri bungeni na anatoka katika chama kimoja na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli ambacho ndicho kinachoongoza serikali hivyo ni rahisi kushirikiana na serikali katika kuzitatua kero za wananchi wa Monduli.

Aidha UVCCM imewahakikishia wanawake, wazee na wasichana kuwa hakuna wa kuwabugudhi au kuwatisha wasijitokeze kupiga kura kwani wamejipanga vizuri kuhakikisha chama viongozi na wanachama wao wapo salama wakati wote wa kampeni na baada ya kampeni hivyo wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura na wamchague Ndugu Julius Kalanga kuwa Mbunge wa Monduli.

Timu ya kampeni ya UVCCM inaundwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Musa Mwakitinya, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha na Mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa Ndugu Saitoti Zelothe, Mjumbe wa Baraza Kuu na Mjumbe wa kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa Ndugu Joanfaith Kataraiya, Mhe Edwin Sanda Mbunge wa Kondoa Mjini, Mhe Gudluck Mlinga mbunge wa Ulanga Mashariki na Mhe Mariam Ditopile Mbunge viti maalum kundi la vijana akitokea UVCCM.

Ratiba ya kampeni inaendelea....

#JuliusKalangaTenaMonduli #KaziInaendelea
img-20180912-wa0399-jpg.864604
img-20180912-wa0398-jpg.864605
img-20180912-wa0395-jpg.864606
img-20180912-wa0393-jpg.864607
img_20180912_180848-jpg.864608
img_20180912_182839-jpg.864609
img_20180912_182637-jpg.864610
img_20180912_174632-jpg.864612
img_20180912_161112-jpg.864613
img_20180912_162330-jpg.864616
img_20180912_174611-jpg.864621
 
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
27,224
Likes
30,481
Points
280
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
27,224 30,481 280
Chama kilichoko madarakani huwa hakina haja kubwa ya kujieleza saaana tutaleta hiki, tutafanya vile bali kuwaonyesha kwa kidole yale yanayofanyika.
CCM mbona ahadi tuu na mpo madarakani? Nguvu kubwa inatumika kama vile ndio mnapata usajili?
 
Elli

Elli

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2008
Messages
29,394
Likes
14,632
Points
280
Elli

Elli

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2008
29,394 14,632 280
Nyokooo siku zenu zinahesabika
 
M

MASIGA

Senior Member
Joined
Aug 29, 2015
Messages
129
Likes
280
Points
80
M

MASIGA

Senior Member
Joined Aug 29, 2015
129 280 80
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndugu Tabia Maulid Mwita amekutana na kundi vijana la manyangulo na makorianga wapatao 319 ambao ndio linalotegemewa kama jeshi la ulinzi kwa kabila la wamaasai. Amewaomba wahakikishe mgombea ubunge wa CCM Ndugu Julius Kalanga anapata kura nyingi za ushindi kwa wao kumpigia kura na kumuombea kura kwa wengine.

Amewaeleza wao ni kundi tegemeo kwenye jamii yao wahakikishe wanapata mbunge atakayesikiliza na kuziwasilisha kero zao serikalini kwa utatuzi ambaye si mwingine ila ni Ndugu Julius Kalanga wa CCM ambaye chama chake kinaongoza serikali na kina Rais wa Nchi ambaye ni Dkt John Pombe Magufuli.

Ndugu Tabia amesema mpaka sasa hakuna wa kuizuia CCM kushinda katika Jimbo la Monduli kwani wananchi wameshajua *"Upinzani hauna desturi ya kutatua kero za wananchi maana wanaamini kwa kufanya hivyo watakosa hoja za kuikosoa serikali iliyopo madarakani ndio maana huwakataza wabunge wake kutoshirikiana na serikali. Kwa kuwa wananchi wa Monduli wanataka maendeleo ni vyema mkamchagua Ndugu Kalanga ili akashirikiane na serikali kwa urahisi kuwaletea maendeleo."*

Vijana hawa wa Kata ya Makuyuni Jimbo la Monduli walimhakikishia Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wazee, kina mama, na kina dada wanajitokeza kupiga kura kwa amani na utulivu bila kutishwa na yeyote.

Pia vijana wamemuhakikishia Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Tabia Kuwa kauli yao ni moja tu *"Wanampa Magufuli Kalanga ili kazi iendelee"*

Kabla ya mkutano wake makamu mwenyekiti alishiriki amsha amsha ya kijiwe kwa kijiwe kumuombea kura Ndugu Kalanga akiwa ameambatana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Ndugu Musa Mwakitinya, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha na Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa Ndugu Saitoti Zelothe, Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa Ndugu Joanfaith Kataraia, Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa kutoka Mkoa wa Arusha Ndugu Lulu Mwacha na Ndugu Ramadhan Mlao kutoka Pwani.

Wengine ni Mhe Gudluck Mlinga Mbunge wa Ulanga Mashariki, Mhe Mariam Ditopile Mbunge Viti maalum kundi la Vijana na Katibu wa CCM Wilaya ya Longido Ndugu Juma Simba Gadafi.

Ratiba ya kampeni inaendelea...

#KaziInaendelea
#JuliusKalangaTenaMonduli
img_20180913_175004-jpg.865539
img_20180913_162942-jpg.865541
img_20180913_175022-jpg.865542
img_20180913_162806-jpg.865543
 
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
45,357
Likes
31,571
Points
280
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
45,357 31,571 280
Chadema wanapoteza tu muda
 
Saguda47

Saguda47

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Messages
5,941
Likes
6,484
Points
280
Saguda47

Saguda47

JF-Expert Member
Joined May 1, 2016
5,941 6,484 280
enzi za chaggademA zimekwishaa! lazima tuambizane ukweli!
 
masoud mshahara

masoud mshahara

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2018
Messages
3,922
Likes
1,608
Points
280
masoud mshahara

masoud mshahara

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2018
3,922 1,608 280
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndugu Tabia Maulid Mwita amekutana na kundi vijana la manyangulo na makorianga wapatao 319 ambao ndio linalotegemewa kama jeshi la ulinzi kwa kabila la wamaasai. Amewaomba wahakikishe mgombea ubunge wa CCM Ndugu Julius Kalanga anapata kura nyingi za ushindi kwa wao kumpigia kura na kumuombea kura kwa wengine.

Amewaeleza wao ni kundi tegemeo kwenye jamii yao wahakikishe wanapata mbunge atakayesikiliza na kuziwasilisha kero zao serikalini kwa utatuzi ambaye si mwingine ila ni Ndugu Julius Kalanga wa CCM ambaye chama chake kinaongoza serikali na kina Rais wa Nchi ambaye ni Dkt John Pombe Magufuli.

Ndugu Tabia amesema mpaka sasa hakuna wa kuizuia CCM kushinda katika Jimbo la Monduli kwani wananchi wameshajua *"Upinzani hauna desturi ya kutatua kero za wananchi maana wanaamini kwa kufanya hivyo watakosa hoja za kuikosoa serikali iliyopo madarakani ndio maana huwakataza wabunge wake kutoshirikiana na serikali. Kwa kuwa wananchi wa Monduli wanataka maendeleo ni vyema mkamchagua Ndugu Kalanga ili akashirikiane na serikali kwa urahisi kuwaletea maendeleo."*

Vijana hawa wa Kata ya Makuyuni Jimbo la Monduli walimhakikishia Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wazee, kina mama, na kina dada wanajitokeza kupiga kura kwa amani na utulivu bila kutishwa na yeyote.

Pia vijana wamemuhakikishia Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Tabia Kuwa kauli yao ni moja tu *"Wanampa Magufuli Kalanga ili kazi iendelee"*

Kabla ya mkutano wake makamu mwenyekiti alishiriki amsha amsha ya kijiwe kwa kijiwe kumuombea kura Ndugu Kalanga akiwa ameambatana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Ndugu Musa Mwakitinya, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha na Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji UVCCM Taifa Ndugu Saitoti Zelothe, Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa Ndugu Joanfaith Kataraia, Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa kutoka Mkoa wa Arusha Ndugu Lulu Mwacha na Ndugu Ramadhan Mlao kutoka Pwani.

Wengine ni Mhe Gudluck Mlinga Mbunge wa Ulanga Mashariki, Mhe Mariam Ditopile Mbunge Viti maalum kundi la Vijana na Katibu wa CCM Wilaya ya Longido Ndugu Juma Simba Gadafi.

Ratiba ya kampeni inaendelea...

#KaziInaendelea
#JuliusKalangaTenaMonduli View attachment 865539 View attachment 865541 View attachment 865542 View attachment 865543
Duuh wamasai wamekula kijani , kweli ccm ni balaaaaaa
 
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Messages
14,047
Likes
13,742
Points
280
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2015
14,047 13,742 280
Chadema wanapoteza tu muda
Jimbo la Monduli ni la familia ya Sokoine Lowasa Ana laana ya Marehemu Sokoine.Alipora Jimbo analifanya lake Na familia yake Bila kupata ridhaa ya familia ya Sokoine.Moja ya sababu kubwa ya yeye Lowasa kushindwa uraisi ni dharau kwa sokoine Na familia yake
 
masoud mshahara

masoud mshahara

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2018
Messages
3,922
Likes
1,608
Points
280
masoud mshahara

masoud mshahara

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2018
3,922 1,608 280
Jimbo la Monduli ni la familia ya Sokoine Lowasa Ana laana ya Marehemu Sokoine.Alipora Jimbo analifanya lake Na familia yake Bila kupata ridhaa ya familia ya Sokoine.Moja ya sababu kubwa ya yeye Lowasa kushindwa uraisi ni dharau kwa sokoine Na familia yake
Haya maelezo ya familia ya sokoine kukabidhiwa jimbo la monduli ww umeyapata wap? kwenye makabidhiano wakina nani ndio walikuwa mashahidi?
 
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Messages
14,047
Likes
13,742
Points
280
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2015
14,047 13,742 280
Haya maelezo ya familia ya sokoine kukabidhiwa jimbo la monduli ww umeyapata wap? kwenye makabidhiano wakina nani ndio walikuwa mashahidi?
Sokoine hakuwa fisadi kama Lowasa alikuwa Waziri mkuu asiyepokea mshahara Lowasa tapeli fisadi kipindi kile akajifanya clean.Mzee sokoine akamuaminia kumbe kibaka mwizi toka akisoma chuo kikuu UDSM alikuwa Na kesi za kuibia wanafunzi wenzie mabwenini.Hasidi haachi asili.Anayebisha aende UDSM aangalie kama Lowasa hana kesi za kuibia wanachuo wenzie miaka hiyo akisoma.
 
masoud mshahara

masoud mshahara

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2018
Messages
3,922
Likes
1,608
Points
280
masoud mshahara

masoud mshahara

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2018
3,922 1,608 280
Sokoine hakuwa fisadi kama Lowasa alikuwa Waziri mkuu asiyepokea mshahara Lowasa tapeli fisadi kipindi kile akajifanya clean.Mzee sokoine akamuaminia kumbe kibaka mwezi toka akisoma chuo kukuu UDSM alikuwa Na kesi za kuibia wanafunzi wenzie mabwenini.Hasidi haachi asili.Anayebisha aende UDSM aangalie kama Lowasa hana kesi za kuibia wanachuo wenzie miaka hiyo akisoma.
Hayo maelezo yako hayaonyeshi wapi jimbo la monduli walikabidhiwa familia ya sokoine, zaidi Naona unamshambulia lowassa , mimi siko interested na kashfa za watu kwasababu hata mimi nina kashfa zangu
 
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Messages
14,047
Likes
13,742
Points
280
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2015
14,047 13,742 280
Hayo maelezo yako hayaonyeshi wapi jimbo la monduli walikabidhiwa familia ya sokoine, zaidi Naona unamshambulia lowassa , mimi siko interested na kashfa za watu kwasababu hata mimi nina kashfa zangu
Utajijua Lowasa hana adabu kwa familia ya sokoine tapeli alimyenyekea sana akiwa hai kumbe it was false conman humility Rangi zake halisi alizionyesha 2015. Sasa majibu atayapata uchaguzi wa mbunge Monduli.Ataijua laana ya Marehemu sokoine Alichokisema 2015 kwa dharau wakati Namelok sokoine akipogombea ubunge kupitia CCM bado kipo kwenye mafaili ya familia ya Sokoine
 
masoud mshahara

masoud mshahara

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2018
Messages
3,922
Likes
1,608
Points
280
masoud mshahara

masoud mshahara

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2018
3,922 1,608 280
Utajijua Lowasa hana adabu kwa familia ya sokoine tapeli alimyenyekea sana akiwa hai kumbe it was false conman humility Rangi zake halisi alizionyesha 2015. Sasa majibu atayapata uchaguzi wa mbunge Monduli.Ataijua laana ya Marehemu sokoine Alichokisema 2015 kwa dharau wakati Namelok sokoine akipogombea ubunge kupitia CCM bado kipo kwenye mafaili ya familia ya Sokoine
Duuh hapa hakuna cha kukusaidia , ila maelezo yako yanaonyesha unatatizo na lowassa (hilo nawaachia wenyewe), mimi nilitaka kujua tu kuwa jimbo la monduli ni kweli kakabidhiwa sokoine na familia yake? hivyo the basi kwasababu umeshindwa kuthibitisha mimi nitachukulia maneno yako kama uzushi tu
 
fundinaizer

fundinaizer

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2016
Messages
1,251
Likes
1,620
Points
280
fundinaizer

fundinaizer

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2016
1,251 1,620 280
Genge la wahuni sio ccm ya Mwl. Nyerere
 
msweety

msweety

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2014
Messages
476
Likes
668
Points
180
msweety

msweety

JF-Expert Member
Joined Dec 5, 2014
476 668 180
Hakuna ushindi tena kwa upinzani awamu hii. Ni kupoteza muda na pesa tu. Kichaa kapewa rungu.
 
Forum statistics

Threads 1,235,153
Members 474,353
Posts 29,213,380