UVCCM yakanusha tuhuma za mgogoro

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umesema hakuna mpasuko miongoni mwa viongozi wa umoja huo kama ilivyoripotiwa na gazeti moja la kila wiki la Mwanahalisi katika toleo lake namba 178 la Machi 3 mpaka 9, mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela, alisema UVCCM iko imara chini ya uenyekiti wa Hamad Masauni na hakuna mpasuko wa aina yoyote ile kwa viongozi wake.

Katika taarifa yake Shigela alisema UVCCM imesononeshwa na kusikitishwa na taarifa ya uzushi, uchochezi na uchonganishi iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho “ Mtoto wa JK azua tafrani” ambayo ililenga kuonesha kuwa kuna mpasuko baina ya viongozi wa UVCCM.

Shigela alisema UVCCM inalaani taarifa ya upotoshaji, uchonganishi na uzushi iliyotolewa na gazeti hilo kwa lengo la kuwachonganisha viongozi na kuipaka matope UVCCM.

Ikifafanua zaidi taarifa hiyo ilisema Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Hamad Masauni, aliwasili Kilimanjaro Februari 27, mwaka huu saa 11.30 jioni akitokea Dar es Salaam na kupokewa na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Beno Malisa, viongozi wa UVCCM Mkoa wa Kilimanjaro na Wajumbe wa Baraza Kuu Taifa waliokuwa wamealikwa.

Ilisema siku hiyo pia kulikuwa na shughuli ya kuwasimika makamanda wa vijana ambayo ilikuwa imemalizika saa 10 jioni mgeni rasmi akiwa Malisa.

Mara baada ya kupokewa, Masauni alipelekwa katika hoteli aliyokuwa amepangiwa wakati akisubiri muda wa kuelekea kwenye ukumbi uliokuwa umeandaliwa kwa ajili ya harambee, shughuli ambayo ndiyo iliyompeleka mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mwenyekiti huyo hakufanya kikao rasmi chochote, bali alikutana tu na baadhi ya wageni waalikwa waliokwenda katika hoteli aliyofikia kumsalimia wakati wakijiandaa na shughuli ya harambee na mtoto wa Rais Jakaya Kikwete, Ridhiwani Kikwete hakwenda kumsalimia Masauni.

Masauni alikuwa mgeni rasmi katika shughuli ya harambee iliyofanyika usiku na ilikuwa tofauti kabisa na sherehe ya kusimikwa kwa makamanda iliyofanyika mchana na katika harambee hiyo, Sh milioni 40 zilikusanywa.

Pamoja na kusikitishwa na kupotoshwa kwa habari hiyo, UVCCM ilisema katika taarifa yake hiyo kuwa UVCCM ni shwari na wala ziara hiyo ya Masauni haina uhusiano wowote na harakati za uchaguzi katika Jimbo la Kikwajuni bali ni mkakati wa UVCCM katika kujipanga kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Habari Leo
 
Martin Shigela ni miongoni mwa viongozi wachache makini na wenye hekima katika CCM,kama yeye ndiye aliyetoa hii taarifa kuna uwezekano mkubwa kwamba anachokisema ni sahihi.
 
Martin Shigela ni miongoni mwa viongozi wachache makini na wenye hekima katika CCM,kama yeye ndiye aliyetoa hii taarifa kuna uwezekano mkubwa kwamba anachokisema ni sahihi.
Ila kwa uzoefu wangu ukiona watu wanakanusha upesiupesi jua kuna jambo na mara nyingi NO ya watanzania huwa ni YES
 
"Katika taarifa yake Shigela alisema UVCCM imesononeshwa na kusikitishwa na taarifa ya uzushi, uchochezi na uchonganishi iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho “ Mtoto wa JK azua tafrani” ambayo ililenga kuonesha kuwa kuna mpasuko baina ya viongozi wa UVCCM"

Na huyo Ridhiwani anatafuta nini huko kasoma vizuri tu hana mambo mengine ya kufanya.aache ushamba
 
Back
Top Bottom