UVCCM watishia kuandamana

UVCCM kukaa chini na vijana UDSM kujadili kwa nini serikali iwalipe dowans? Well this is a dirty game..I will rephrase and put it in a simple example. Kijana kukaa chini na jirani kujadili kwa nini baba yake amlipe tapeli? It could have been logical for kijana kumshauri baba yake huko huko nyumbani maana kuongea na jirani what does he really trying here? Kumdhalilisha baba? kutafuta huruma ya jirani? au katumwa na baba kumchanganya jirani ambae keshapata fununu jinsi baba alivyotapeliwa? Digest....
 
Hivi vijana wasomi Tanzania ni Cheap kiasi hiki??

Kwanza kama wako Serious na hii kitu kwa nini hawajaenda pale Nkruma Hall wanakwenda vichochoroni Kinondoni??

Pia kama sikosei wamewapelekea mabasi/malori ili kuwapeleka huko kinondoni.

Wanafunzi wa vyuo vikuu wamesahau shida na taabu zilizoletwa na mfumo unaoipa nguvu UVCCM. PIa wamesahau matusi makubwa ambayo UVCCM imekuwa ikiyatoa dhidi ya Viongozi wazalendo wenye nia na hamu ya kuleta maendeleo.

Pia wameshau jinsi UVCCM walivykuwa kimya kwa miongo kibao pale wanafunzi wa vyuo walipoanzisha migomo ya kudai mazingira mazuri ya vyuo vyao.

UVCCM wana ziba gap iliyoachwa wazi na UVCDM ambao hawajaonyesha makali yao hata kidogo.
What am seeing is different, kuna wimbi la migomo vyuo karibu vyote TZ.....

UVCCM inajua vijana walichagua CDM, UVCCM inajua vijana ndio waliopiga kura wengi , UVCCM is not stupid! Inajua pa kuwashika vijana ni kuvunja bodi ya mikopo, they are poised to win big on uni students!

Mashinikizo yote yanayotolewa ni ili iwe agenda ya 2015...other parties and particulary youths beware!
 
Tatizo ninaloliona ni kuwa vijana wa Chadema bado hawajawa radical enough.. sasa UVCCM ndio wanaonesha njia. Yale ambayo yalikuwa yafanywe na vijana wa upinzani yatafanywa na vijana wa CCM! A classic example of political triangulation!


MM...UVCCM is a monotonous organ… it is used by the parent organ to derail fact and deploy fiction… comparing and contrasting UVCCM and BAVICHA is far away to conclude …. UVCCM is a titanic recently in need of wholly prayers before the ship completely capsize


UVCCM patrons have no option against the people’s power …. The only worry within sisiem is the fear of a failed regime
 
Hapo nakupata Mzee mwenzangu.

Vijana wa CDM wamelala, wako Butu, wanafuata nyumanyuma kaa mkia wa ndezi hawako active wamwemwachia Mzee wetu Dr Slaa kuanzisha mashambulizi na kuyaendeleza THIS IS A SHAME UVCDM

Nadhani ni vizuri kwa Chadema to know their strengths and weaknesses UVCCM is more powerful than UVCDM, time and money has made it that way.... therefore you have got to fight using your strength and the only weapons chadema have is their strong MPS and Dr Slaa.., these people need to fight tooth and nail day and night kwa kufichua maovu ya CCM..., they need to expose everything CCM and not caring about UV or CCM..., They have got truth in their side..., and thank God propaganda dont work as it used to.... enzi za kumwabia mtu kashiba huku ana njaa zinaanza kwisha... people now can tell real from fake....
 
Wameshtushwa na wastani wa kura 25 alizokuwa anapata JK kila kituo pale UDSM kwenye uchaguzi mkuu, huku Dr Slaa akipata wastani wa zaidi ya 150. Angeumbuka zaidi kama wanachuo wengi wangeshiriki uchaguzi
Nitajie kama imewahi kutokea rais wa Daruso kuwa muislam. kwa hiyo sishangai kwa Kikwete. watu wenyewe wengi wamekuzwa huko makanisani, unatarajia nini? kwa taarifa yako angalia walichokuwa wakifanya hapo chuo hata kipindi cha Mwinyi. Angalia uchaguzi uliopita, unajua Jk alipata kura ngapi hapo chuo? Mimi ninamarafiki zangu wakaribu lets say Oscar ambaye sasa hivi yupo mzumbe, nakumbuka aliniambia hawezi kuchagua mtu kama JK na jamii yake.
Angalizo, jirani zetu badilikeni, dunia inabadilika siku hizi uwezekano wa nyinyi kuendelea kula keki ya taifa peke yenu imefikia ukingoni, jifunze kutoka Ivory coast. Tutaishia kupigana, afterall sisi hatuna cha kupoteza kwani tayari tupo kwenye matatizo siku zote zilizopita.
 
Nitajie kama imewahi kutokea rais wa Daruso kuwa muislam. kwa hiyo sishangai kwa Kikwete. watu wenyewe wengi wamekuzwa huko makanisani, unatarajia nini? kwa taarifa yako angalia walichokuwa wakifanya hapo chuo hata kipindi cha Mwinyi. Angalia uchaguzi uliopita, unajua Jk alipata kura ngapi hapo chuo? Mimi ninamarafiki zangu wakaribu lets say Oscar ambaye sasa hivi yupo mzumbe, nakumbuka aliniambia hawezi kuchagua mtu kama JK na jamii yake.
Angalizo, jirani zetu badilikeni, dunia inabadilika siku hizi uwezekano wa nyinyi kuendelea kula keki ya taifa peke yenu imefikia ukingoni, jifunze kutoka Ivory coast. Tutaishia kupigana, afterall sisi hatuna cha kupoteza kwani tayari tupo kwenye matatizo siku zote zilizopita.
Hoja yako siielewi, unapata shida ya kuwa hakuna rais muislam from DARUSO au huyo rafiki yako Oscar ambaye kwa mtazamo wake hamtaki JK ?

Pia sentensi yako ya mwisho inatatiza kuwa hamna cha kupoteza... Tukirudi kwenye mada una lolote la kuchangia?
 
UVCCM hivi sasa wanakutana na wanafunzi wa UDSM ktk ukumbi wa Vijana Social Hall Kinondoni na hapo Riz1, Bashe na Shigela wametoa matamko mazito dhidi ya serikali. Wamerudia kama yale ya tamko lao, Bashe kazungumzia Dowans


Wakawadanganye wengine, yaani kwao malipo ya Dowans ndiyo dhuluma pekee kwa watanzania?

Mbona hawaongelei EPA?

Ni vigumu kwa hawa vijana kubadilika kwa muda mfupi. Haya wanayotaka kuyakemea yamekuwapo siku zote sasa iweje waanze kuyachukia ghafla?

TAFAKARI!
 
mbona niliona maraisi wa vyuo yaani daruso tahliso na vyuo vingine wamepinga kauli ya UVCCM taarifa ya habari ITV saa mbili ,nakadhalika na sasa hivi UVCCM wapo channel 10 idadi yao ni ndogo sana ha kuna hamasa kabisa kwa hiyo hii ni janja ya nyani ,wanasafari ndefu kwa kweli ni vizuri wakaja na strategy nyingine hawana pa kutokea
 
Wamebeba watu kwa Magari..and I hope wametoa na Posho..!
Siku alipokuja Dr Slaa Wanavyuo walienda weneyewe kwa Miguu yao..na hawakupewa hata senti...!
 
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi umetishia kuitisha maandamano nchi nzima iwapo serikali haitoivunja bodi ya mikopo ya elimu ya juu na kuiunda upya.

Malisa amesema kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kuona kila kukicha migomo ya wanafunzi imekuwa ikitokea na sababu kubwa ni watendaji wa bodi hiyo kutowajibika.

Alibainisha kuwa bodi hiyo imekuwa ikiwanyanyasa wanafunzi na kuichonganisha serikali ya CCM na wasomi hapa nchini.

Alisema kama serikali haitokisikia kilio chao hicho watafanya maandamano ya nchi nzima wakiwashirikisha wanafunzi wa shule za sekondari kwa sababu wao ni wahanga watarajiwa wa bodi hiyo inayofanya ubaguzi na unyanyasaji wakati wa kutoa mikopo.


Ukishangaa ya musa utaona ya filauni, yangu macho nasubiri habari za kiintellijensia za afande Mwema.
 
UVCCM kuandamana Bodi ya Mikopo ivunjwe
• Kuwashirikisha wanafunzi wa sekondari

na Mwandishi wetu


amka2.gif
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), umetishia kuitisha maandamano nchi nzima iwapo serikali haitoivunja bodi ya mikopo ya elimu ya juu na kuiunda upya.
Umesema kuwa bodi hiyo hivi sasa imekuwa ikiwanyanysa wanafunzi na kuwa chanzo cha migomo kwa wasomi wa vyuo vikuu hapa nchini.
Tishio hilo limetolewa jana jijini Dar es salaam na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM, Taifa, Beno Malisa muda mfupi baada ya kukubaliana na ombi la Shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu (CCM) mkoa wa Dar es Salaam lililotaka kufanyika kwa maandamano hayo .
Shirikisho hilo lilisema kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya kuona kila kukicha migomo ya wanafunzi imekuwa ikitokea na sababu kubwa ni watendaji wa bodi hiyo kutowajibika.
Malisa pamoja na Katibu Mkuu wa umoja huo, Martin Shigela waliishutumu vikali bodi ya mikopo kwamba imeshindwa kazi, na kuwataka viongozi wa bodi hiyo watumie busara zao kuziacha ofisi hizo kabla ya kufukuzwa.
Alibainisha kuwa bodi hiyo imekuwa ikiwanyanyasa wanafunzi na kuichonganisha serikali ya CCM na wasomi hapa nchini.
Alisema kama serikali haitokisikia kilio chao hicho watafanya maandamano ya nchi nzima wakiwashirikisha wanafunzi wa shule za sekondari kwa sababu wao ni wahanga watarajiwa wa bodi hiyo inayofanya ubaguzi na unyanyasaji wakati wa kutoa mikopo.
“Kimsingi tumekubaliana na tamko lenu lililoutaka uongozi wa UVCCM tukaiambie serikali iivunje bodi…sisi tumewaelewa na tunawaahidi kuanzia sasa UVCCM itaandaa maandamano makubwa nchini nzima kuishinikiza serikali iivunje bodi hiyo kwani imekuwa ikiropokaropoka hovyo na kuwanyanyasa wanafunzi.
“Serikali imekuwa ikiipatia fedha bodi ya mkopo kwa wakati, lakini kwa sababu inazozijua imekuwa ikiwacheleweshea wanafunzi hadi wamejikuta wakiishi maisha ya taabu na kuanza kuichukia serikali yao.
“Kila kukicha wanafunzi wamekuwa wakiilalamikia bodi na migomo haiishi…hivi bodi ni dudu gani hadi tuliruhusu liwanyanyase Watanzania wenzetu…tunasema hatukubali lazima tuandae maandamano ya kushinikiza bodi hii ivunjwe,” alisema.
Kwa upande wake, Katibu wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Salum Ally, alisema lengo la mkutano huo ni kutoa tamko la kuipongeza UVCCM la hivi karibuni lililotaka bodi ivunjwe na kuiomba UVCCM iandae maandamano nchi nzima kushinikiza bodi hiyo kuvunjwa na kwamba tamko hilo wamelitoa kwa niaba ya vyuo vikuu vyote nchini.
Ally alisema katika tamko hilo wameainisha matatizo yanayoikabili bodi hiyo likiwamo la kiutendaji kwamba bodi imekuwa na uwezo mdogo wa kuhakiki taarifa zinazotolewa na waombaji wa mikopo.
Pia alisema tatizo lingine ni la utunzaji mbovu wa kumbukumbu za waombaji, hali inayochangia usumbufu kwa wanafunzi.


Source: Tanzania Daima.
 
Wakati wao UVCCM wakikaa kikao kuandaa maandamano, wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kupitia mawaziri wao wa mikopo walikaa kikao na kukataa maandamano ya UVCCM. Sasa vijana wa CCM wameumbuka, sielewi kama wataandamana wao pekee, na wakienda huko kwa waziri sijui watatoa madai ya mikopo gani wakati wao hawasomi!
 
wamekurupuka!

bodi haiwezi kuwa na ufanisi kama mlolongo wa taasisi nyingine kama TCU na vyuo husika hautabadilishwa pia. mchakato wa mikopo ya wanafunzi ni mrefu mno na vigezo vimejaa utata. ubaguzi wa madaraja nao ni sehemu ya matatizo yanayoonekana kama ya bodi lakini kumbe ni sera ya serikali yenyewe.

kama ikivunjwa itakuwa mhanga tu wa sera mbovu za serikali na hata kikiundwa chombo kingine kama mamabo hayatabadilika nacho kitajikuta katika lawama kama hizo
 
waanze kuandamana kumpinga rostam na uchakachuaji wa kura, wakimaliza waandamane wakipinga ufisadi halafu ndio tuanze kuwaamini
 
Wakati wao UVCCM wakikaa kikao kuandaa maandamano, wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kupitia mawaziri wao wa mikopo walikaa kikao na kukataa maandamano ya UVCCM. Sasa vijana wa CCM wameumbuka, sielewi kama wataandamana wao pekee, na wakienda huko kwa waziri sijui watatoa madai ya mikopo gani wakati wao hawasomi!
Hii kweli nimeiona jana kwenye news. Hawa UVCCM wanatafuta kujitakasa sasa dhidi ya dhambi za baba zao. Sijui kama watapata hiyo support wanayoitarajia. Walishindwa pia kutoa mbadala wa tatizo kama ikivunjwa
 
Back
Top Bottom