UVCCM: Wataalam wa tiba na afya ni mashujaa wetu

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
Umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi tumeona ni muhimu hiki cha janga la corona tuwaombe watanzania wote tuungane katika kampeni za kuelimisha na kukumbushana kuzingatia maelekezo ya tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona pamoja na kutambua moyo wa kipekee wa madaktari, wauguzi na wataalam mbalimbli wa tiba na afya waliojitoa kuokoa maisha ya wagonjwa wa corona bila kuhofu hatari zilizopo.

Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Tanzania Bara na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndugu Galila Wabanh'u amesema wao kama vijana wameona ni muhimu kufanya kitu kitakachoonesha mshikamano kati ya wananchi na wataalam wetu wa tiba na afya.

"Wamekuwa jasiri, wenye upendo na ustahimilivu wa hali ya juu. Kubwa zaidi ni uzalendo waliouonesha hakika wanastahili kuitwa mashujaa wa mstari wa mbele katika mapambano haya ya kukabiliana na janga la corona." Alisema Galila

Ndg Galila alisisitiza "Katika kuonesha tunatambua na kuthamini kazi hii kubwa wanayoifanya nawaomba watanzania wote kwa umoja wetu tuwatumie ujumbe wa kuwatia moyo, kuonesha kuthamini na kujali wanachokifanya kupitia kadi, barua fupi, nyimbo, dua au maombi kwa Mungu pamoja na njia mbalimbali zinazoweza kuwaonesha mshikamano wetu kwao."

Naye Kaimu Katibu Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa Ndg Leonard Singo alisema "Tuitumie mitandao ya kijamii kuwatia moyo na kuwaonesha kuwa tunathamini kazi yao. Unaweza jirekodi video clip fupi ya kuwaonesha upendo na kuwatia moyo halafu ukairusha mtandaoni ikiwa na hashtag #AsanteniMashujaaWetu


Mwisho Ndugu Singo alihimiza "Ikiwa jamii inawajali na kuwathamini wataalam wetu hawa basi tuhimizane kuzingatia maelekezo ya tahadhari dhidi ya ugonjwa huu wa corona ili kuwapunguzia mzigo."

Corona ipo, tujikinge na kuwakinga wengine.
IMG-20200417-WA0046.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hehe 😅, hii nchi bwana, hizi futuhi mpaka kwenye majanga kama haya zitaisha lini?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom