UVCCM wanahangaika kuchanganya maji na mafuta, Haiwezekani!

Mnyanyembe wa Mboka

JF-Expert Member
Feb 10, 2017
2,347
3,033
Salam kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

KAZI IENDELEE !!!

Ama baada ya salam waswahili wanasema Muungwa akivuliwa nguo huchutama ... !!! UVCCM chutameni kwanza na muinamishe vichwa chini

Nawasihi msiwe kama M/Kiti wenu mtazidi kujidhalilisha kwa unafiki usio na uelekeo, tafuteni uelekeo kwanza ndio muendelee na mapambio yenu huku mkijua mnapambia nini kuelekea wapi tofauti na tulipotoka

Sote tunafahamu kuwa kuna hali ya mkanganyiko imewakuta kuhusu nani asifiwe na nani akandiwe kulingana na propaganda zinazolenga mafanikio ya itikadi na mitazamo ya kiutawala. Na kama kusifiwa au kukandiwa basi iwe ni kwa lipi kati ya SSH na JPM.

Hii ni kwa sababu ipo wazi mbele ya jamii ya watanzania wote bila kujali chama, dini au itikadi, na imeonekana wazi dhahiri shahiri kuwa utawala wa JPM ni sawa na HASI(-) wakati utawala wa Mama unaonekana kuwa ni CHANYA(+)

Kwa hiyo kumsifia Magu ni kumponda Mama na kumsifia Mama ni kumponda Magu. Kwa kufupi Mama kachora mstari kati yake na Magu hivyo basi ni watanzania tu kuamua upande mmoja kati ya upi wa kusifia na upi wa kukandia na kamwe haiwezekani usifie pande zote utakua ni mnafiki wa kiwango cha lami

Ndg. Zangu UVCCM ni wazi kabisa kwa hali ilivyo haiwezekani kusifia wote na kufanya hivyo ni sawa na kutaka kuchanganya Maji na Mafuta yachanganyike ili upate solution moja

Hapa la msingi kila mmoja kwa wakati wake ajifanye kama Kigwangala tu tujue moja au kama alivyofanya Jafo na barakoa yake siku ya kumuaga Magu kitendo bila kuchelewa kabla jogoo halijawika watu wakaigeuka Nyungu

Ukisikia kupotezwa ndio huku lazima uchague moja kuramba matapishi na kukubali kuitwa mnafiki au kukaza na misimamo ya kijiwejiwe.

Kazi mnayo!!!
 
JPM amefanya yake makubwa yaliyompasa amemaliza mwendo amepumzika
SSH ameanza mwendo anafanya makubwa na yanayompasa kwa viwango vilevile

Hiyo habari ya kusifia na kuponda haina nafasi, kikubwa ni kasi na utekelezaji

Kazi iendelee 😍🇹🇿🙏
 
View attachment 1746221

Kazi iendelee

Hapana sio kweli kuwa muwazi usibanebane maneno funguka tu kigugumizi cha nini ???

Kwa upana ulitakiwa useme hivi:

JPM amefanya yake makubwa YASIYOMPASA kwa mtazamo wake aliodhani na kuamini uanafaa tena wakati mwingine tofauti na mtazamo wa CHAMA CHAKE na hata kwenda tofauti na matakwa ya KATIBA YA NCHI YA YAKE

KATIBA ambayo aliapa kuilinda na kuiheshimu lakini kwa bahati mbaya au nzuri (Allahu Ya'alam) HAKUMALIZA mwendo amepumzika au anataabika (Allahu Ya'alam)

Allahu Ya'alam = Mungu ndie ajuae

SSH ameanza mwendo HAJAFANYA makubwa yanayompasa kwa viwango VYOVYOTE bado ila ameonyesha mwanga na mwelekeo wa kufuata na kuheshimu ilani ya CHAMA CHAKE pia kulinda na kuheshimu KATIBA YA NCHI YAKE

Hii habari ya KUSIFIA na KUPONDA INAYO nafasi tena kubwa sana katika maisha ya watanzania, mwisho wa yote TUNAHITAJI kasi na utekelezaji kwa faida ya watanzania wote bila ya kujali KABILA, DINI wala ITIKADI ZA SIASA, tena kwa usawa na kwa mujibu wa KATIBA na SHERIA za nchi bila ya VISASI, UBAGUZI, UBINAFSI, UNAFIKI, UONGO, UBAHILI, WIZI, UBABE, UONEVU, UDHALIMU, UDIKTETA, USHAMBA, UJUAJI, UJINGA, UPUMBAV, UBWEGE, UBOYA .... n.k

Nimekujibu neno kwa neno na ukisoma neno kwa neno na imani utanielewa na kukubaliana na hoja yangu ... Karibu Sana !!!
 
kuchanganya maji na mfuta inawezekana tunaongezea emulsifying agent baada ya hapo yanachanganyikana.
!!! Ooh Ok ... tuseme sifa za mtazamo wa kiutawala wa JPM ni maji ambayo bei yake ni Sh. 500 na sifa za SSH ni mafuta yanayopatika kwa wastani wa bei ya Sh. 2,000

Je, ni emulsifying agent gani hiyo kama si propaganda za kinafiki zilizoligharimu taifa kwa bei ya uhasama wa kisiasa uliopelekea chuki zilizoleta mvunjiko wa umoja wa watanzania, chuki na uhasama uliokwenda mbali na kuathiri makundi mbalimbali katika jamii ya watanzania katika maeneo yao mpaka kwenye kaya zao

Huku wengine mapema kabisa wanawahi kujiinua eti kuomba radhi as if walikua wamelewa hivyo walikua hawajui wafanyalo pumbavu kabisa Mxieusssszzzz!!!

Naturally Maji na Mafuta haviwezekani kuchanganyika mpaka uongeze kitu kingine ...

Uzuri Sayansi haiongopi bana

Sasa amua moja tubaki na JPM kwenye kujifukiza au twende na SSH tukashirikiane na wenzetu jumuiya ya kimataifa kupambana kisayansi

Halafu leo hii unawezaje kuwasifia hawa watu wote kwa pamoja bila ya wewe kuwa mnafiki ase!!!
 
FB_IMG_1575390800494.jpg
 
ni sawa na kutaka kuchanganya Maji na Mafuta yachanganyike ili upate solution moja
Mbona kisayansi ni jambo la kawaida sana hilo la maji na mafuta kuchanganyika?

Hata hiyo mada yako, unaifanya kuwa ngumu bila sababu.

Mtu mwenye akili ya kujitegemea kwa kufikiri hawezi kusubiri kuchagua upande mmoja ausifie na aponde upande wa pili.
Hakuna 'absolute' katika maswala haya. Magufuli pamoja na yale mabaya yake, pia alikuwa na mazuri yake. Sasa, kwani mtu mwenye akili timamu inayojitegemea kifikra hawezi kusifu yale mazuri na kuponda yale mabaya bila kuonekana kuwa ni mnafiki?

Samia, bado ni mgeni sana. Mtu mwenye akili nzuri hawezi kurukia mara moja hii na kujitupa miguuni kwa huyu mama wakati huu kwa kusifia.
Asifie nini kama sio unafiki wa kujipendekeza kwa mategemeo ya kujaza tumbo!

Haya matamko mawili, matatu aliyotoa hivi karibuni ambayo hata utekelezaji wake bado ndiyo asifiwe kwayo?

Mtu mwenye akili nzuri, atavuta subira aone kazi inayofanyika kwanza.

Kwani kuna mashindano ya kusifia, kana kwamba kuna 'roster' nani atakuwa wa kwanza kusifia?

Nilitaka kumalizia kwa kuandika kwamba mada yako ni ya 'kipuuzi', lakini ngoja nisifanye hivyo kwa sasa.
 
JPM amefanya yake makubwa yaliyompasa amemaliza mwendo amepumzika
SSH ameanza mwendo anafanya makubwa na yanayompasa kwa viwango vilevile

Hiyo habari ya kusifia na kuponda haina nafasi, kikubwa ni kasi na utekelezaji

View attachment 1746221

Kazi iendelee 😍🇹🇿🙏
MC fokafoka mlimsifia sana na hamtaki msikie anapondwa , tulieni tu mbona team Msoga ilijikalia kimyaaa sasa kuna team SSH so wenzetu tupisheni
 
Sawa kabisa, mtu hupimwa kwa matendo yake, si ahadi, matamko, maagizo au uteuzi alioufanya. Na hakuna tatizo kumsifia mtu katika mema aliyofanya na kumkosoa alipokosea
Mbona kisayansi ni jambo la kawaida sana hilo la maji na mafuta kuchanganyika?

Hata hiyo mada yako, unaifanya kuwa ngumu bila sababu.

Mtu mwenye akili ya kujitegemea kwa kufikiri hawezi kusubiri kuchagua upande mmoja ausifie na aponde upande wa pili.
Hakuna 'absolute' katika maswala haya. Magufuli pamoja na yale mabaya yake, pia alikuwa na mazuri yake. Sasa, kwani mtu mwenye akili timamu inayojitegemea kifikra hawezi kusifu yale mazuri na kuponda yale mabaya bila kuonekana kuwa ni mnafiki?

Samia, bado ni mgeni sana. Mtu mwenye akili nzuri hawezi kurukia mara moja hii na kujitupa miguuni kwa huyu mama wakati huu kwa kusifia.
Asifie nini kama sio unafiki wa kujipendekeza kwa mategemeo ya kujaza tumbo!

Haya matamko mawili, matatu aliyotoa hivi karibuni ambayo hata utekelezaji wake bado ndiyo asifiwe kwayo?

Mtu mwenye akili nzuri, atavuta subira aone kazi inayofanyika kwanza.

Kwani kuna mashindano ya kusifia, kana kwamba kuna 'roster' nani atakuwa wa kwanza kusifia?

Nilitaka kumalizia kwa kuandika kwamba mada yako ni ya 'kipuuzi', lakini ngoja nisifanye hivyo kwa sasa.
 
Hapana sio kweli kuwa muwazi usibanebane maneno funguka tu kigugumizi cha nini ???

Kwa upana ulitakiwa useme hivi:

JPM amefanya yake makubwa YASIYOMPASA kwa mtazamo wake aliodhani na kuamini uanafaa tena wakati mwingine tofauti na mtazamo wa CHAMA CHAKE na hata kwenda tofauti na matakwa ya KATIBA YA NCHI YA YAKE

KATIBA ambayo aliapa kuilinda na kuiheshimu lakini kwa bahati mbaya au nzuri (Allahu Ya'alam) HAKUMALIZA mwendo amepumzika au anataabika (Allahu Ya'alam)

Allahu Ya'alam = Mungu ndie ajuae

SSH ameanza mwendo HAJAFANYA makubwa yanayompasa kwa viwango VYOVYOTE bado ila ameonyesha mwanga na mwelekeo wa kufuata na kuheshimu ilani ya CHAMA CHAKE pia kulinda na kuheshimu KATIBA YA NCHI YAKE

Hii habari ya KUSIFIA na KUPONDA INAYO nafasi tena kubwa sana katika maisha ya watanzania, mwisho wa yote TUNAHITAJI kasi na utekelezaji kwa faida ya watanzania wote bila ya kujali KABILA, DINI wala ITIKADI ZA SIASA, tena kwa usawa na kwa mujibu wa KATIBA na SHERIA za nchi bila ya VISASI, UBAGUZI, UBINAFSI, UNAFIKI, UONGO, UBAHILI, WIZI, UBABE, UONEVU, UDHALIMU, UDIKTETA, USHAMBA, UJUAJI, UJINGA, UPUMBAV, UBWEGE, UBOYA .... n.k

Nimekujibu neno kwa neno na ukisoma neno kwa neno na imani utanielewa na kukubaliana na hoja yangu ... Karibu Sana !!!

Mimi nimeandika ninachokijua na kukiamini
Na wewe umeamdika unachokiamini

Unataka tufanane? Au unataka tupangiane imani??
 
MC fokafoka mlimsifia sana na hamtaki msikie anapondwa , tulieni tu mbona team Msoga ilijikalia kimyaaa sasa kuna team SSH so wenzetu tupisheni

Tusipangiane imani.... tena tusipandikizane chuki kabisaa

JPM atabaki kuwa Mwamba kwa mazuri aliyofanya kwa nchi yetu

SSH ni anaendelea kuwa chuma imara kundelea kuchapa kazi katika ubora wake na spidi kukamilisha zile kurasa 303
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom