UVCCM wana nia ya Kuwasaidia wanavyuo au ni propaganda zao zimeanza?

STEIN

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
1,770
553
Ndugu zangu wanaJF,

Nimetafakari sana kauli za hivi karibuni za hawa wanaojiita watoto wa JK, Makamba, Sumae, Mzindakaya, Lowasa, Msekwa etc. wakiongozwa na redio na TV ya propaganda kama Clouds FM/TV chini ya wanapropaganda kama kina Kibonde wanayo jeuri ya kuwakomboa wanachuo?????

Nashangaa sana kutokana na wazazi wa hawa vijana wanaojiita UVCCM ndio walioshikilia mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu kwa kuamini tutawaongoza wajanja wachache kwa ridhaa ya wajinga wengi, matajiri wachache kwa ridhaa ya masikini wengi.

Eti leo vijana wao wanakuja na kusema wana dhamira ya kweli ya kutetea wanavyuo, hini propagandi iliyopita kiasi maana haingii akilini kuona Ridhiwani anaandamana ili baba yake aivunje bodi ya mikopo nasema haiwezekani hawa mafisadi wachanga wanakuja na agenda ya siri nyuma ya pazia.

Agenda hiyo ni ya kuendelea kuwapumbaza hawa vijana wa vyuo vikuu wasiendelee kudai haki zao za msingi. Kama kweli wanaona hawa vijana wananyanyaswa na wazee wao basi wawataje hadharani kuwa ndio wanaoihujumu bodi ya mikopo.

Na katika hili hawa vijana wamepewa hela za kuwapumbaza vijana ili tu wawe washabiki huku wakiendelea kunyanyasika.

Nasema mtu ambaye CCM anaona bodi inawanyanyasa vijana ajiuzulu mara moja kwani bodi hiyo imeundwa na kuongozwa na makada wa CCM.

Nawashauri wanavyuo waendelee kudai haki zao kupitia serikali zao za wanafunzi na si UVCCM maana wataendelea kuwa mtaji wa CCM na mafisadi hadi lini?

Majuzi tu walikuwa wanasema CDM ndio inapandikiza migomo vyuoni, wiki mbili badae wanasema eti bodi ndio inayasababisha haya, hivi hawa UVCCM na CCM yao wanafikiri sisi tunasau kama wao wanvyosahau mara kwa mara? Hii haikubaliki kamwe.

Naomba tupaze sauti zetu kupitia JF ya kuwaelimisha na kupinga hujuma yeyote dhidi ya wanavyuo.

Mungu ibariki TZ na wau wake.
 
Miaka yote walikuwa wapi?

Toka lini mtoto UVCCM ampinge mtoto BODI wa Baba CCM?

Yaani UVCCM wanaingilia elimu ya juu, kuna nini hapo? Ujinga mtu!

TAHLISO inafanya kaz gan? UVCCM kaz zake ni nini? Ujinga mwingne huo!

Kwa nn TAHLISO wasitangaze maandamano...
 
Bahati mbaya UVCCM haina tena vijana wenye tafukuri, labda NAPE kwa hapo zamani.

Wasikimbilie kusema Bodi ya Mikopo Ivunjwe bali waitake serikali ya CCM itoe fedha za kutosha kwa bodi na kwa wakati. Kama bodi haina pesa wanataraji italipa nini?

Tunasubiri sana kwa hamu kuona maandamano yao kupinga bodi ya mikopo maana mawaziri wa mikopo katika vyuo husika tayari wameshapinga mtazamo wa UVCCM. Pili shirikisho la vijana wa CCM elimu ya juu sio serikali za wanafunzi katika vyuo hivyo nakwanamna hiyo UVCCM inakazi kubwa kushawishi maandamano. Labda huko sekondari na shule za msingi.

Nawashauri wasikurupukie mambo ila watafakari kwa kina.
 
Wameona CHADEMA wameteka vyuo vikuu, naona sasa na wao wanataka kuwahadaa. Kazi kweli.

2015 hiyoooooooooooo inakuja tutaona mengi ya ajabu.
 
Ni kweli walituhadaa tangu 2005 hadi leo sasa wanataka kutudanganya.
 
Ivi Jk tarehe 31 alipotwambia migomo vyuoni inaletwa na wanasiasa wanaotaka umaarufu alimaanisha mwanae Riz1 na Shigela wakiwa na vazi la kijani/uvccm? Ivi riz1 anayechukua fungu kuzunguka Tz nzima kutafuta wazamini wa mafisadi ndo anarudi kwa wanachuo nchi nzima kuwaambia kuwa aliowasaidia kuingia madarakani ni wazembe au? Ivi kuandamana kwa hao Ccm ina maana serikali yao inabidi kuondolewa au? Uvcc dhima ya maandamano ni kuwa watu wamekosa kuelewana. Kwa iyo mmeshindwa kuwaelewa akina makamba na RA au? Nyie mnaleta maswali zaidi ya majibu na tumesubiri mulete ujinga wenu tuwaone,si kwamba wanachuo tutawagomea nyie,ila tunaelewa mmetumwa kupima joto la jiwe,nawashauri mje kijanja yasijewakuta ya Mtikila kule Tarime kwa msiba wa Wangwe.
 
Firstly Hatudanganyiki
watu wapo kuwasafisha watu
2ndly Wanatafuta umaarufu kutoka kwa vijana especialy vyuoni
3rd Jiulize kwa nini wasemaji ni wale kutoka Arusha malisa na chatanda?
4th Swala la bodi lishughulikiwe kitaalam siyo kiisiasa
 
Wamechemsha hawana nguvu za hoja, pia hawawezi kumshawishi mtu ujinga wao kwani hakuna siri teeena watanzania woote wanawajua kua wao ni watoto wa mafisadi
 
Wale vijana wanakurupuka sana, wanakaa kikao halafu wanafanya maisha ya mtu binafsi kuwa ajenda ya kikao, ukiangalia tamko lao wameongelea zaidi maisha binafsi ya Dr. Slaa badala ya hoja za kitaifa, wamelaaniwa wale kama watangulizi wao.

Wanataka bodi ya mikopo ivunjwe bila kutoa njia mbadala ya kutatua tatizo la mikopo elimu ya juu.
 
Swala la msingi la kujiuliza ni kuwa wale tuliopigwa mabomu pale mlimani city wakati palikua nyika tukiandamana kupinga kuanzishwa kwa bodi tulikuwa wapumbavu? Ikaanza kwa mbwembwe baadae maamuzi ya kutafuta kura yakaingilia kati mkopo ukawa kwa wote na siyo kwa walengwa kama ilivyokusudiwa na kama tulivyoambiwa pale bungeni tulipoitwa tena tukatoka nje ya kikao baada ya kuitwa wahuni. Sasa bodi ikishirikiana na vyuo na TCU wamefika mahali hata kukusanya madeni imekua taabu UVCCM wanajileta kiherehere eti ivunjwe. Nilifurahia sana maana tahliso wao walisema wazi kuwa bodi ya mikopo iwezeshwe maana kiundani ina mapungufu ya kiutendaji ambayo yanaingiliwa na sias. Huyo riz1 alimtumia sana salum kuanzisha vuguvugu la kuitoa daruso tahliso kwa kuanzisha maandamano na kumuweka rais wake wa daruso anayemjua mwenyewe kisa tu Kipara hataki kuingiza siasa za vyama vyuoni ingawa naye kipa ni ccm. Salu aliwahdaa wana DARUSO kuwa yeye ni mtu mwema na ana nia nzuri na wanachuo lakini leo anaonekana front page The Citzen akitaka bodi ifutwe bila kufafanua kisomi kuwa ifutwe alafu nini kifanyike, nani akusanye madeni mengi tunayodaiwa na je nchi inaongozwa na vijana wa chama fulani au inaongozwa na watanzania?
 
Watafuta wapenzi,, wanaleta propanganda kwenye mambo ya msingi sh**zy zao:A S 20:
 
waandamane kuuliza mabilioni yaliyochotwa na meremeta,kagoda,tanpower nk yanarejeshwa lini na baba zao? ccm na uvccm makenge kwelikweli! yaani baba anasubiri shinikizo kutoka kwa mtoto?why protest while u have every power to act?ndo yale yale eti sijui umasikini wa nchi ninayoiongoza unatokana na nini? tahliso hongereni sana kuukataa utawala wa kifalme!
 
kwani slaa si aliahidi kuivunja ndani ya siku 100 na kuweka kitu kiitwacho uhuru fund pamoja na mamlaka ya mikopo ya vyuo vya juu hawa uvccm si walikuwa wakipinga? ni nani aliyewaroga? afadhali kwa sasa wametokea dar
 
Back
Top Bottom