UVCCM wamkataa mkuu wa wilaya Iringa


nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Likes
86
Points
145
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 86 145
SUNDAY, DECEMBER 15, 2013Mwenyekiti wa Uvccm wa Wilaya ya Iringa Benitho Kayugwa akizungumza na uvccm baada ya kuhitimisha mafunzo ya siku 5 kuhusu ujasiliamali, kuhitimisha mafunzo hayo yaliyofanyika katika kambi ya vijana ya Ihemi hivi karibuni.

baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo

mwenyekiti wa Uvccm wa Wilaya hiyo Benitho Kayugwa akimkabidhi cheti ya utambulisho wa mafunzo hayo Newton (Picha zote na Denis Mlowe Iringa)

========== ======= =========

Na Denis Mlowe


UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Iringa wamemkataa Mkuu wa Wilaya ya Iringa Dk. Leticia Warioba na kumuomba, Rais Jakaya Kikwete aweze kumuondoa katika Wilaya hiyo na kumpangia Wilaya nyingine ya kufanyia kazi baada ya kushindwa kuwajibika ipasavyo katika majuku yake na kutokuwa na ushirikiano kwa wananchi wa wilaya hiyo.


Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya Itikadi, Siasa,Utendaji na Ujasiliamali yaliyofanyika katika Chuo cha Vijana Ihemi kwa siku tano mwenyekiti wa Uvccm wa Wilaya hiyo Benitho Kayugwa, alisema Warioba hana ushirikiano katika kuwajibika na kutoa agizo ndani ya siku 60 serikali inayoongozwa na Jakaya Kikwete kuweza kumwondoa katika wilaya hiyo na kuwaletea mkuu wa wilaya anayejua wajibu wake katika kazi.


Kayugwa alisema wameamua kwa kauli moja kutokumtaka mkuu wa wilaya hiyo kwa kuwa hana ushirikiano katika majukumu yake kulalamikiwa na wananchi pamoja na baadhi ya viongozi kwa kushindwa kuzingatia ushirikiano na kuendelea kukumbatiwa.


“Sisi Vijana wote tumeamua kwa pamoja tunataka kupata majibu ndani ya siku 60 kuweza kuondolewa kwa mkuu huyu wa wilaya ambaye anaonyesha kabisa kazi yake hawezi kuifanya na tutamgomea katibu yoyote atakayeletwa hapa wilayani hadi katibu aliyekuwa likizo ya miaka 3 apewe fedha zake kwenda kusoma, aidha kiongozi yoyote aliyechaguliwa na wananchi na hayuko tayari kuwajibika tuko tayari kumshughulikia ." alisema Kayugwa


Kayugwa aliitaka serikali kuwawajibisha watumishi wote wa vituo vya afya wanaokiuka maadili ya kazi kwa kuuza madawa ya serikali yanayotakiwa kupelekwa katika vituo vya afya na kushindwa kuyafikisha sehemu husika na kusababisha wananchi wasiwe na imani na serikali.


Aidha aliitaka serikali kuweza kuwajibisha viongozi wote wa ngazi tofauti ambao wanakiuka kuweka wazi matumizi na mapato ya kijiji kwa wananchi kwa kuwachukulia hatua kali kwa kuwa wanasababisha wananchi kuichukia serikali yao kutokana na uzembe wa watu wachache.


Aliongeza kwa kuiomba Serikali kuwahamisha watumishi waliokaa sehemu moja kwa muda mrefu kuwea kuleta mabadiliko chanya kutokana na baadhi ya watumishi kufanya kazi kwa mazoea na kufanya kazi pasipo weledi kwa kuzoea mazingira.


MICHUZI

 
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Likes
86
Points
145
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 86 145
Kila mtu ndani ya hiki chama cha kikomunisti ana nguvu zaidi ya serikali?
 
mnyikungu

mnyikungu

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2009
Messages
1,814
Likes
1,723
Points
280
mnyikungu

mnyikungu

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2009
1,814 1,723 280
Kha!raisi anaamrishwa? Hivi vitoto vimekosa adabu, eti ndani ya siku sitini!!!!!!, kwani chama kina nguvu gani ya kumfundisha kazi rais....wabunge ambao ndo wawakilishi wa wananchi mbona hawatumiki.....si wamuite mbunge wao wa viti maalum ndo wamuambie hayo kama kero ya wananchi....hichi chama sasa...kila mmja anatoa amri..hata hivi vitoto kweli...kazi ipo
 
M

Mafuluto

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2009
Messages
1,647
Likes
293
Points
180
M

Mafuluto

JF-Expert Member
Joined Aug 25, 2009
1,647 293 180
Nchi ya usanii sasa hata haka kajamaa ambako hata kuandika jina lake hakajui eti kanatoa agizo kwa laisi amtimue DC...ha ha ha. Lakini kwa siku kadhaa media zimekuwa zikiremba remba sana habari za uvccm na hata sijui chipukizi wa mkoa huu. Mlezi wao ni mmoja wa wale majangili wakuu na amezoea sana kukumbatiwa na kubembelezwa sana kutoa mbuzi au mgando kwa ugeni, sasa inawezekana kabisa haka kakijeba ka UV CCM kametumiwa tuu

Hawa tunawajua sana si ajabu walimtaka DC acheze rafu kwa upinzani hapo mujini sasa kama akigoma lazima zengwe litengenezwe.

Watahangaika sana kutoa maagizo au amri kwa sirikali ya kisanii lkn wananchi sio wa kugaiwa ubwabwa tena au kubabaikia viatu vya plastik vya Mwakalebela au kofia za hako kachangudoa Droo au sijui Kabati
 
H

Haji Salum

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2013
Messages
1,022
Likes
9
Points
0
H

Haji Salum

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2013
1,022 9 0
Hawa vijana ni matokeo ya sekondari za kata!!
 
McDonaldJr

McDonaldJr

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2013
Messages
6,429
Likes
6,382
Points
280
McDonaldJr

McDonaldJr

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2013
6,429 6,382 280
Haaaahaa vijanaaaaaa.....!ngoja tusubiri izo cku zifike,
 
MtamaMchungu

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Messages
4,171
Likes
1,193
Points
280
MtamaMchungu

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2011
4,171 1,193 280
Hamna cha ajabu huu ni ukoo wa makambare, kila mtu ana sharubu, so Kila mtu ni mkubwa tu.
 
K

Kajunjumele BA

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2012
Messages
674
Likes
19
Points
35
K

Kajunjumele BA

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2012
674 19 35
Kila mtu ndani ya hiki chama cha kikomunisti ana nguvu zaidi ya serikali?
Ndugu yangu nngu007 mi nadhani aliwanyima gari ...ukisikia ushirikianao ni pamoja na kudokoa vimafuta vya gari wilayani au kutumia magari ya serikali kwa shughuli za chama chao.
 
Ikwanja

Ikwanja

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2011
Messages
2,083
Likes
341
Points
180
Ikwanja

Ikwanja

JF-Expert Member
Joined Jul 12, 2011
2,083 341 180
acha wamalizane wenyewe kwa wenyewe
 
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Messages
15,871
Likes
86
Points
145
nngu007

nngu007

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2010
15,871 86 145
Ndugu yangu nngu007 mi nadhani aliwanyima gari ...ukisikia ushirikianao ni pamoja na kudokoa vimafuta vya gari wilayani au kutumia magari ya serikali kwa shughuli za chama chao.

Kama ni kweli aliwanyima GARI NAAM alifanya kazi yake inayotakiwa... Sababu CHAMA na SERIKALI ni vitu viwili tofauti haviendani pamoja... Sasa hao VIJANA wa CCM wanaona kuwa UVUNJAJI SHERIA ni haki yao sababu tu wao ni CCM je wakiingia MADARAKANI Si ndio MWISHO wa wa UWAJIBIKAJI WAO??

Watavunja sheria kushoto na kulia - na wametoa wapi HIZO MANTIKI za KUVUNJA SHERIA??? Kwa WAKUBWA WAO NDANI ya CCM kwahiyo CCM CHAMA KIZIMA KIMEOZA UFISADI na UCHUMAJI MALI ndani ya CHAMA...
 

Forum statistics

Threads 1,250,853
Members 481,494
Posts 29,747,788