uvccm walivyowahadaa hata great thinkers | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

uvccm walivyowahadaa hata great thinkers

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Plato, Jan 27, 2011.

 1. Plato

  Plato JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  nani asiyetilia shaka tamko la uvccm? Wanataka tu kumsafisha lowasa.baadaye wamesikika wakise wanataka waliodanganya taifa na kuingiza serikali hasara wawajibishwe.sasa mtu akiongea hivyo kwenye muktadha wa dowans richmond,nani hajui wanasema nini.nanyi mwadanganyika! Wanafiki tu hawa
   
 2. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Great thinkers huwa hatudanganyiki..
  Katika thread ile ya Tamko la Uvccm niliandika yafuatayo nanukuu:
  Re: TAMKO LA UVCCM (Soma) na Mwelekeo wa Kisiasa Nchini

  [​IMG] Originally Posted by DENYO [​IMG]
  2. Dowans ni anguko la ccm -hili linaenda kuwaweka kuzimu kabisa, uvccm hawataki downsa ilipwe, mkwere anataka ilipwe-wanataka lirudi bungeni -ili sitta angolewe uwaziri na mwakyembe -hii ccm itabaki kweli? Nguvu ya umma inawaangalia.

  .  Asante sana kwa mtizamo huo.
  Ukisoma katikati ya mistari, utagundua kuwa hili tamko la uvccm ni EL at work - kutaka kugombea urais 2015. Kwa vipi?.. Fuatilia..
  JK ambaye ndiye mkuu wa nchi anataka dowans ilipwe, kwa mabavu ya serikali hii hakuna atakayezuia malipo yasifanyike.
  Baada ya malipo kufanyika au wakati wa mchakato wa kulipa ukiendelea, suala hilo litarudishwa bungeni kwa nia iliyofificha ya kutaka kuonyesha kuwa Tume ya Mwakyembe ililidanganya bunge, na Bunge likiongozwa na Sitta likaishauri vibaya serikali nakufikia serikali kupoteza hayo mabilioni. Hapa maana yake atawajibishwa Mwakyembe na Sitta na EL atakuwa amesafishwa.
  Mkakati huo haukuanza leo; kumbuka namna Sitta alivyoenguliwa kwenye uspika - walijua akiwa spika hoja kama hizi hazitakubaliwa; na JK alimpa huo uwaziri kama kejeli tu kwamba utonja joto ya jiwe baadae.
  Tamko linasema --kama Mwakyembe alilidanganya Bunge basi awajibike... halafu ndiyo inakuja serikali...... Hii maana yake nini, burden of proof kwanza itakuwa kwa Mwakyembe na kwa kuwa bunge lenyewe ndilo hilo, likisema halikuridhika na maelezo yake, the serikali haitakuwa na haja ya kuproove on its side - the game will be over!!
  Lakini nawatahadharisha ccm, wanajaribu kucheza na moto unaofukuta chini kwa chini - ukilipuka!!! au kwa lugha nyngine wamezuia maji yasielekee bondeni kwa muda mrefu, yamejaa na yanatafuta namna ya kuendelea na safari ya kwenda bondeni, kingo zimeshaelemewa; njia sahihi ni kuyafungulia kwa utaratibu, lakini yakibomoa hizo kingo madhara yake ni makubwa!! Mwenye maskio na asikie.
  Ushauri kwa Mwakyembe: uliwahi kutueleza kuwa hamkusema yote ili kuilinda serikali - tukakwambia serikali haiindwi hivyo kwa kufichaficha, hukutuelewa; sasa ni wakati muafaka wa kutoficha kitu maana ukizidi kuficha utaanguka mwenyewe kwanza na serikali baadae. Kwa kusema yote - utajiokoa wewe na taifa..
  ACHA WOGA WA KUPOTEZA MADARAKA KWANI KABLA YA KUWA MBUNGE HUKUWA UNAISHI?.
  Nawe Sitta, yule nyoka uliyemwachia, sasa amefura, amenyayua kichwa juu - kwa fimbo ulimshindwa wakati ule, sasa ni 'risasi' inayotakiwa na si nyingine ni nguvu ya umma. Sema ukweli wote na nguvu ya Umma itakuwa nyuma yako! ​
   
 3. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Great thinkers hatudanganyiki... kwa tamko lile wamewadanganya viongozi wao!!!! Soma majibu ya tamko lile ndani ya JF!!!
   
 4. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,279
  Likes Received: 1,720
  Trophy Points: 280
  Tena wamefanya bad timing. Sasa hivi dunia inafukuta. Watu hawataki ujinga ujinga tena. Angalia Tunisia, Misri na Yemen. As a leader don't you ever underestimate people's power. Mahakama kitu gani. KUna tofauti kati ya illegal and unjust. Sasa kama wao wanaona ni lawful kulipwa si tunaona ni unjust watajiju.
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,899
  Likes Received: 12,031
  Trophy Points: 280

  Kwani wewe ni ndiye DENYO, au umechanganya madesa kwa bahati mbaya.​
   
 6. V

  Vipaji Senior Member

  #6
  Jan 27, 2011
  Joined: Jun 11, 2009
  Messages: 115
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  UVCCM ni nguruwe wao kazi yao ni kurushiwa makombo na vitu vilivyooza ndiyo maana wanaufinyu wa kufikiri. Bado wako usingizini hawajui kuwa LOWASA hasafishiki kabisa. Hawawezi kutuhadaa hata kwa namna yoyote ile.
   
Loading...