UVCCM waikataa DOWANS | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM waikataa DOWANS

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nickname, Jan 19, 2011.

 1. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  UVCCM-Mara waitaka serikali itangaze kuwa DOWANS ni kampuni hewa, wahamashishana kama vijana waamke na kuwashauri viongozi wa CCM waibane serikali iwajali wananchi wake na wasitangaze takwimu za uongo za maendeleo wakati ukweli unaonekana.Walalamikia CCM kuogopa midahalo ya kitaifa na pia wawakilishi wa CCM na jumuiya zake kukosekana kwenye mdahalo wa katiba mpya uliofanyika UDSM.Pia UVCCM waitaka serikali ya CCM itoe kweli ajira kwa vijana kupitia kilimo cha umwagiliaji.

  Tafsiri yangu: Hili ni jambo jema liilooneshwa na UVCCM mkoani Mara.Nimegundua kitu kuwa watu wa mkoa wa Mara ni wana mabadiliko na wasio waoga kusema ukweli,safi sana hii inatakiwa kuigwa na viongozi wa UVCCM wa mikoa mingine pamoja na wakitaifa wakiwemo Beno na Riz1


  UVCCM WAITAKA CCM KUTOA TAMKO
  Wakati huo huo, wajumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Mara, wamekitaka chama hicho kuitaka Serikali kutamka kuwa Dowans ni kampuni hewa ambayo hastahili kulipwa kiasi chochote cha fedha za walipakodi wa Tanzania.

  Wamesema kukaa kimya kwa CCM wakati serikali yake ikiendelea na mchakato wa kuliipa Dowans fedha hizo kutatafsiriwa kuwa kinahusika moja kwa moja na njama hizo za wizi wa fedha za umma.
  Wakizungumza katika mkutano ulioitishwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mara kupitia UVCCM, Esther Bulaya, kwa ajili ya kuwashukuru, wajumbe hao walisema kama Bunge lilibaini kuwa kampuni ya kufua umeme ya Richmond ni kampuni hewa, iweje leo Dowans iliyorithi mikoba yake ikawa ni kampuni halali ya kulipwa fedha hizo.
  "Tumefika mahali kama vijana wa CCM kukitaka chama chetu kitamke kwa kuitaka serikali kusitisha malipo kwa Dowans. Dowans leo inapataje uhalali wa kulipwa mabilioni ya Watanzania wakati Richmond tulielezwa ni kampuni hewa. Hivi CCM inataka kuwaambia nini Watanzania ambao wengi hawawezi kuwa na uwezo wa kupata mlo wa siku?" alihoji Fidelis Manyerere, mjumbe wa Baraza Kuu wa umoja huo mkoa wa Mara na kushangiliwa.
  Manyerere alisema ili kulinda heshima ya CCM ambayo imejengwa kwa miaka mingi, lazima viongozi wakuu wakaishauri serikali kuacha kuilipa Dowans na kutahadharisha kuwa ikiwa fedha hizo zitalipwa kwa Dowans chama hicho kitakuwa katika wakati mgumu hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015.

  Mjumbe huyo pia alishauri CCM kuacha kutoa taarifa zinazopingana kwa wananchi. Mjumbe mwingine Marwa Mirumbe, pamoja na kueleza kukerwa na mambo mbalimbali yanayoendelea likiwemo la malipo kwa Dowans, alimuomba mbunge huyo kutumia Bunge kuomba kuharakishwa kwa ujenzi wa barabara ya lami kutoka Makutano-Musoma hadi Mto wa Mbu mkoani Arusha hatua ambayo pia alisema itachangia ukuaji wa uchumi wa maeneo hayo.

  Mjumbe mwingine kutoka Wilaya ya Tarime, Denis Zacharia, akizungumzia suala la katiba mpya, alisema inasikitisha kwa kiasi kikubwa kwa chama hicho kutozungumzia suala hilo wakati wakitambua wazi hoja hiyo ni ya Taifa zima kwa sasa.
  "Juzi kulikuwa na mdahalo kuhusu katiba pale Chuo Kikuu ambao ulirushwa hewani na ITV, lakini ilinisikitisha kuona hakuna hata mwakilishi wa chama wala jumuiya zake. Hivi kwanini tunapenda kufanyia mzaha kiasi hiki jambo la kitaifa, tunakwepa kujitokeza nasi tuzungumze mnadhani wananchi wanatuelewa vipi wakati wote tunajua matizo mengi ya nchi yako ndani ya katiba?"alihoji na kuongeza:
  "CCM tunaanza kuogopa makongamano ya kitaifa, tunaogopa mijadala, jamani tufike mahali tubadilike ili sisi pia tushiriki mijadala ya kitaifa na kutoa michango yetu kuhusu mambo muhimu ya nchi, tusiwaachie wapinzani kazi hizi," alisema Zacharia.
  Alisema woga huo umesababisha vijana wa CCM kukosa uthubutu hata wa kuhutubia ama kuelezea mafanikio ya serikali katika mikusanyiko ya watu, jambo ambalo alisema ni hatari kwa chama.
  Kwa upande wake, mwenyekiti wa UV-CCM mkoa wa Mara, Marwa Mathayo, alisema wakati umefika kwa vijana kujipanga vizuri kwa kuwashauri viongozi wa CCM kuibana serikali yake kutekeleza mambo mbalimbali yanawakabili wananchi ili kuepuka kuhojiwa wakati wa chaguzi.
  Mathayo alisema jambo hilo limekuwa likisababisha kushindwa na wapinzani katika kata, majimbo hata kupunguza kura za rais.
  "Vijana wanahoji tunataka ajira, na viongozi wa serikali wanatamba kuwa wamezalisha ajira ambazo hazionekani. Wasomi wanataka maabara, mnasema hakuna fedha huku serikali ikitumia mamilioni ya fedha kununulia Ma-VX," alisema na kuongeza:
  "Hivi chama kimeshindwa kuibana serikali yake sababu sasa tumeshaona baadhi ya viongozi wa serikalini ambao wanaendesha hujuma katika kuhakikisha CCM inaondoka madarakani na CCM yenyewe inakaa kimya."
  Mjumbe mwingine, Rudia Mareza, alisema serikali ya CCM ina kila sababu ya kuhakikisha inatengeneza mazingira mazuri ya ajira kwa vijana kwa kujiajiri wenyewe baada ya kuhitimu masomo ya sekondari na vyuo vikuu badala ya kutegemea ajira toka serikalini.

  Alisema sehemu kubwa ambayo inaweza kutoa ajira kubwa kwa vijana ni kilimo kwa kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika sekta hiyo kwa kupewa nyenzo ambazo zitakazotumika katika kuendesha kilimo cha umwagiliaji badala ya kutegemea mvua, jambo ambalo litachangia vijana kuzalisha wakiwa vijijini.

  Source : Nipashe
   
 2. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Waambie wamuone Mbunge wa Musoma mjini,atawapatia kadi za CADEMA..
   
 3. nickname

  nickname JF-Expert Member

  #3
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 516
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Hata mimi nakuunga mkono hao jamaa wana roho ya ki-CHADEMA kabisa.:A S 39:
   
 4. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Big up UV-CCM Mara kwa nao kuona kuwa Richmond/Dowans ni kampuni hewa. Tunataka watu wanaoweka mbele maslahi ya Taifa/nchi kwanza. Vyama vinakuja baadaye...
   
 5. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,728
  Likes Received: 1,636
  Trophy Points: 280
  lakini UV-CCM si inafadhiliwa na Edward L. N. ndio maana alisaini kuuzwa kwa jengo lao pale karibu na Mnazi mmoja eti anawaingiza kwenye UBIA,nao wakakubari kunywa BIA utaona akiwasikia hawa watawatuma wakina Riz 1 kuleta mtafaruku, lakini watu wa Musoma nawaamini maana wakiamua wameamua hata Baba wa Taifa alipowaomba kumsaidia kumtoa nduli Idi Amini Dada walikuwa wa kwanza, labda hawa watusaidi kuondoa fisadi na one NM&RA, EL, siku hizi eti naye EL anajikomba kuomba katiba Mpya, ikiwa hivyo atatueleza mali zake zote kazipata wapi, yeye kama nyani anayechekelea kichaka wakati kinaungua sijui hatalala wapi!!
   
 6. s

  smz JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Vijana mkoa wa Mara mmesema ukweli wenu. Siyo siri viongozi wa kitaifa wa ccm na serikali yake wanaogopa midahalo, kongamano kama ukoma. Tujiulize kulikoni?? Wanaogopa nini, au hawana hoja zenye mashiko. Maana ni afadhali kukaa kimya kuliko kujibu majibu ya dharau na ya kitoto kama alivyojibu waziri wa sheria - Kombani kuhusu katiba: Eti nilikuwa natingisha kiberiti!!!??? Dharau hii

  Watanzania sasa hivi ni waelewa wa mambo kuliko anavodhani, ni vizuri viongozi walioko madarakani kuwa makini wanapotoa matamko kwa niaba ya serikali.

  Haiingii akilini mtu kama Jaji Werema kusema waTz wanaongea kama "mabata" Kweli tunafananishwa na mabata!!
   
 7. Freestyler

  Freestyler Senior Member

  #7
  Jan 19, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kuna umuhimu wa kupatikana watu wa kutoa mashambulizi kutokea ndani pia.Mwizi akiwa ndani ya nyumba hutoki nje halafu umwambie atoke umpe kipigo, unamfuata huko huko!
   
 8. M

  MaryGeorge Member

  #8
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Binafsi nilipenda "move" ya wanachama wa UV-CCM mkoa wa Mara - inadhihirisha ni namna gani Mkoa wa Mara ulivyo na misimamo, nawapongeza sana wanachama waliokutana na kukubaliana kwamba mabadiliko ndani ya chama imefika mahali yanatakiwa! - Siasa zenye ukweli na zenye kufuata haki ni siasa nzuri - ila nina jambo moja kwa hawa vijana - kwamba, wakiona hakuna mabadiliko yanatokea ndani ya chama chao, basi nawasihi waondoke taratiiiiiiibu kuelekea CHADEMA....Honegereni sana wana UV-CCM Mara! :smile-big:
   
 9. M

  MaryGeorge Member

  #9
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  MALARIA SUGU and COMPANY wapo jamani? mbona hawajatoa comments zao kuhusiana na hili suala la UV-CCM Mara????
   
 10. mama yuva

  mama yuva JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  I like I like I like! Kweli wana CCM msiwe tu bendera kufuata upepo na kushangilia tu vijembe vya kusutana vya viongozi wenu. waseme ukweli Watanzania si wajinga. Bei ya Umeme inatuathiri sote, wanachama wa CUF, CCM, CHADEA, CCJ, nk. tuungane wote kulipinga Hili. wakati sisi tunalala giza, Ridhiwani aporomosha majengo tu, kwa nini tuumie sisi tu?
   
Loading...