UVCCM wadai hawana mipasuko...lakini ni kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM wadai hawana mipasuko...lakini ni kweli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Dec 25, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,364
  Trophy Points: 280
  UVCCM: Hatuna mpasuko, tunajipanga 2015

  Imeandikwa na Angela Semaya; Tarehe: 24th December 2010 @ 23:26

  JUMUIYA ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) imesema haina mpasuko wala makundi ndani ya jumuiya hiyo na kwamba hivi sasa wameanza kufanya tathmini kwa ajili ya kujipanga vizuri kwa chaguzi za siku zijazo.

  Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigella alibainisha hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

  Shigella alisema hakuna mgawanyiko wowote ndani ya taasisi hiyo kama inavyodhaniwa na kwamba kila jambo ndani ya UVCCM linafanyika kwa kufuata taratibu na kanuni zilizowekwa.

  Alisema UVCCM kama taasisi na CCM kwa ujumla imeanza kufanya tathmini ya uchaguzi uliopita na namna ya kujipanga kwa chaguzi zijazo na kuongeza kuwa tathmini hiyo imeanzia ngazi ya shina na itafika hadi ngazi ya kitaifa.

  Akizungumzia suala la kujaza nafsi ya Mwenyekiti wa UVCCM iliyoachwa wazi na Hamad Masauni Yusuf alisema hakuna mtu anayezuia uchaguzi kwa ajili ya kujaza nafasi hiyo ila taratibu lazima zifuatwe.

  Akitoa ufafanuzi alisema kwanza Halmashauri Kuu ya CCM itajadili kuhusu kujaza nafasi hiyo, kisha wataleta barua kwa Katibu Mkuu wa UVCCM ambaye ndiye atapeleka barua hiyo kwa Kamati ya Utekelezaji na Baraza la UVCCM ndipo atapata maelekezo ya kuitisha uchaguzi.

  Shigella alisema pia utaratibu wa wagombea wa viti maalum ulifuata taratibu na kanuni walizokuwa wamekubaliana kama taasisi na kwamba UVCCM pia haina mtu yoyote wanayemuandaa kwa ajili ya kuja kugombea nafasi ya Urais.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,364
  Trophy Points: 280
  Ukitaka kujua UVCCM imejaa wachovu angalia wanapodai ya kuwa wanajipanga kwa 2015............wananjipanga kivipi? Hivi wananhusika vipi katika utatatuzi wa kero zetu?

  Siwahi kuwasikia wakidai katiba mpya, punguzo la bei ya umeme au hata kukemea ufisadi.......na viongozi wao wengi hata umri hauwaruhusu kuwemo humo UVCCM na kuwepo kwao wanawazibia vijana nafasi zao............sasa iweje tuwaamini wanaposema hawana mipasuko wakati ukweli ni kuwa chaguzi za viti maalumu zimeonyesha nyufa za wazi wazi kabisa.......................
   
 3. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #3
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  UVCCM wat? Taasis ya umbea tupu...
   
 4. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #4
  Dec 25, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hapo atakuwa ameambiwa aeleze hayo mbele ya waandishi wa habari. Kutokuwepo mgogoro si kitu cha kuficha wala siyo kwamba ukienda mbele ya waandishi wa habari watu ndiyo watauamini ukweli wake
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Dec 25, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180


  CHADEMA hatupokei pumba.
   
 6. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #6
  Dec 25, 2010
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kama uvccm hawana mgogoro ni kwa nini gazati la rai la alhamisi limezuiliwa kuuzwa dsm na mikoani????
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Dec 25, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hata Dar lilikuwa linakusanywa (kwa kuyanunua) kutoka vibanda vya magazeti, ingawa hawakufanikiwa kufikia vibanda vyote. Habari ni kwamba Riz-One ndiye aliamuru magazeti yakusanywe
   
Loading...