UVCCM waadhimisha mwaka mmoja wa Rais Samia madarakani

Hamduni

Senior Member
Apr 25, 2020
155
107
UVCCM WAADHIMISHA MWAKA MMOJA WA RAIS SAMIA MADARAKANI KWA KISHINDO

Katibu Mkuu UVCCM Ndg. Kenani Kihongosi, aliongoza Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, tarehe 19/3/2022 katika Uwanja wa Taifa Kahama, Shinyanga.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan alipiga simu kuzungumza na vijana katika kongamano la kuadhimisha mwaka mmoja wa Kishindo wa Serikali ya Awamu ya sita kupitia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana ndugu Kenani Kihongosi

Aliwapongeza na kuwashukuru vijana kwa mchango wao katika siku 365 za Serikali ya awamu ya sita na kuwasisitiza juu ya kulinda Amani na utulivu.

"Niwaombe sana tuendelee kulinda Amani na utulivu, tuchape kazi, tufanye siasa za kistaarabu. Vijana ninyi ndio nguzo yangu nawategemea sana" Alisema Rais Samia

Kongamano hilo lilifanyika Wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama, Jumuiya na Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mh. Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mh Festo Kiwaga, Wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM TAIFA, Wenyeviti na Makatibu wa Chama na Jumuiya.

#uvccmkazini
#AlipoMamaVijanaTupo
#KiongoziMakini
#UongoziShirikishi

IMG-20220321-WA0003.jpg
 
Mbona inatumika nguvu nyingi kuadhimisha mwaka mmoja wa rais kiasi hiki? Zama za kulamba miguu bado zipo sana. Soon tutaanza kusikia muda huongezwe na kama hataki alazimishwe. Mungu atusaidie.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom