UVCCM: Viongozi CHADEMA hawajui tofauti ya Uhuru wa Mahakama, Utawala Bora na Uongozi wa Kiimla

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,280
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mtwara, Nasibu Kanduru amesema kuwa matamshi ya Tundu Lissu akiwa nje ya Nchi yanaonyesha wazi Viongozi wa CHADEMA hawajui kutofautisha kati ya Uhuru wa Mahakama, Utawala Bora na Uongozi wa Kiimla.

Kanduru amesema: "TunduALissa anaonyesha fika anajua Mashitaka yanayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hivyo yuko katika juhudi kubwa ili kuficha ukweli nyuma ya mashitaka yanayomkabili Mbowe kabla ya Mahakama kutoa hukumu... Lissu anatumia taaluma yake ya Sheria na kuwa Wakili wa Mahakama Kuu ili kuficha madai na tuhuma au madhambi na makosa yanayoweza kumkabili kila mtuhumiwa yeyote anayetoka Chadema huku akijificha kwenye kichaka cha Siasa."

"Ni kipi kinachomfanya Lissu azungumzie kesi ilioko Mahakamani huku akijua kufanya hivyo ni wazi Makamu Mwenyekiti huyo anaithibitishia Dunia kua, anaizuia Mahakama isitende haki dhidi ya tuhuma zinazomkabili Mbowe mahakamani" - Aliongezea Bwana Kanduru

My Take:
Nmejaribu kufuatilia matamko ya UVCCM mwaka huu, nimegundua huyu Mwenyekiti wa Mtwara yupo On Fire. Sijajua reason Behind.

Time will tell
 
Mnamtaka asiongelee hiyo kesi kwa kuwa ipo mahakamani, na nyinyi mnavyojijengea hiyo kinga ya kushitakiwa, hamuoni nanyi mnavunja sheria?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Ni kipi kinachomfanya Lissu azungumzie kesi ilioko Mahakamani huku akijua kufanya hivyo ni wazi Makamu Mwenyekiti huyo anaithibitishia Dunia kua, anaizuia Mahakama isitende haki dhidi ya tuhuma zinazomkabili Mbowe mahakamani
Uhuru wa mahakama kwa kesi isiyokuwa na msingi kwa motive za kisiasa? Mtu anadai katiba reforms badala apewe kesi ya uchochezi anapewa ya kutaka kuua viongozi then surprisingly inageuka ya kulipua vituo vya mafuta?

DPP ana uwezo wa kuondoa shauri muda wowote ule so sio kweli kwamba kesi ikienda mahakamani basi hakuna influence ya nje ya mahakama inayoweza batilisha kesi. Tumeona hayo kwa kesi ya UAMSHO!
 
Hivi wale bavicha waliotaka katiba yao ifanyiwe marekebisho ili mwenyekiti wa chama hicho awe anakaa madarakani kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano kama ilivyokuwa kabla ya Mbowe, wameshasikilizwa na uongozi wa chama au wamepuuzwa na utawala wa kidikteta?
 
UVCCM ilikuwa zamani. Siku hizi vijana bogus unawakauta huko. UVCCM ya siku hizi kimekuwa kiwanda cha kuwafanya vijana kuwa wanafiki, wauaji na watekaji.
 
Hivi wale bavicha waliotaka katiba yao ifanyiwe marekebisho ili mwenyekiti wa chama hicho awe anakaa madarakani kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano kama ilivyokuwa kabla ya Mbowe, wameshasikilizwa na uongozi wa chama au wamepuuzwa na utawala wa kidikteta?
Utawala gani wa kidikteta?
 
Back
Top Bottom