UVCCM tuacheni unafiki kama kweli sisi ni wazalendo. Mwenyekiti James kaonesha njia

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Ndugu zangu vijana wangu na wanaccm tuache unafki na ubishi usiokuwa na sababu. Hivi anayoyasema mwenyekiti Heri James kuna kipi kipya hapo? Tunabisha kitu gani kama kweli tunataka kulijenga taifa kwa pamoja?

Tuache ujinga, tusitake kulazimisha mambo wakati tunajua kabisa kuna uwezekano wa mfumo wetu wa uendeshaji wa Chama na serikali ukabadilika. Mama Samia ni Mwanaccm mwenzetu na ni lazima atekeleze ilani ya chama. Lakini tunachotakiwa kufahamu ni kila mtu na utashi wake na ni lazima uongozi wa Mama utofautiane na wa Magufuli maana huyu ni Samia na yule ni Magufuli.

Kwa sasa Mama ndiye mwenye power ndani ya Chama na serikali, tukijifanya jeuri kwa mamlaka ya ndani ya katiba ya chama na ile ya Jamuhuri mamama akiamua anapanga timu yake anayoitaka itakayomsaidia kutekeleza ilani ya Chama. Sisi tudipoeleweka atatafuta timu nyingine ya kufanya nae kazi tuache porojo.

Mwenyekiti wetu Heri James ni mtu mwenye akili nyingi sana, anajua fika kabisa mazingira ya siasa za sasa ni lazima yatofautiane na ya sasa. Kwani uongo kwamba tulitumia nguvu nyingi kuendesha siasa zetu nje na ndani ya chama? Tunapokumbuka pale tulipoharibu na kutaka tuishi vizuri na ndugu zetu tuliokwisha wakwaza kuna tatizo gani?

Kama Mama yetu nafsi yake itakua na na amani akiona anaongoza taifa lenye amani na upendo kuna tatizo?

Mwisho na Muhimu.Tusitake kuanza kujenga makundi yatakayotoa faida kwa wapinzani wetu.Tufungamane na mwenyekiti wetu wa Jumuiya yetu na wa chama taifa, tuache kua wanafiki.
 
Rubbish nonsense
Unyama wenu mje tu na kusema eti 'kama tuliwakosea .... konyokonyokonyo
Mmewaliza wazazi wetu wazee wetu mama zetu ndugu zetu halafu msamehewe tuuu
Kwa hili hata imani itatupisha kidogo maana mlijikweza mno kheee
 
Huyo Kheri James alishasema atamuua Tundu Lissu kwa sindano ya sumu.
Mwenyekiti wa @ccm Temeke, kwenye mkutano wa Sandali alisema tunaompinga Magufuli, polisi wawaruhusu watukatekate tufe.
Sasa mapatano na watu ya kaliba yenu sisi hatuyataki.
Rais wetu mnyenyekevu, asiye dhalimu ametumwa na Mungu, baada ya kusikia kilio chetu.
Hatutaki Shirika na nyie
 
Rubbish nonsense
Unyama wenu mje tu na kusema eti 'kama tuliwakosea .... konyokonyokonyo
Mmewaliza wazazi wetu wazee wetu mama zetu ndugu zetu halafu msamehewe tuuu
Kwa hili hata imani itatupisha kidogo maana mlijikweza mno kheee
Umejua kunifurahisha aisee
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Ujinga gani wakati huu ndio ukweli? Wewe huhitaji tunda la upendo?
Mlikuwa wapi kutupenda siku zote?
Mmeua watu wangapi wasio na hatia?
Mmefunga kwa kuwasingizia watu wangapi?
Hilo tunda la upendo linaota kwenye mti wa chuki, uhasama na uadui?
Huwezi ukapanda mbegu ya chuki uote upendo
 
UPUUZI MTUPU! Maadui wakubwa wa Tanzania na Watanzania nyie.
Ndugu zangu vijana wangu na wanaccm tuache unafki na ubishi usiokuwa na sababu. Hivi anayoyasema mwenyekiti Heri James kuna kipi kipya hapo? Tunabisha kitu gani kama kweli tunataka kulijenga taifa kwa pamoja?

Tuache ujinga, tusitake kulazimisha mambo wakati tunajua kabisa kuna uwezekano wa mfumo wetu wa uendeshaji wa Chama na serikali ukabadilika. Mama Samia ni Mwanaccm mwenzetu na ni lazima atekeleze ilani ya chama. Lakini tunachotakiwa kufahamu ni kila mtu na utashi wake na ni lazima uongozi wa Mama utofautiane na wa Magufuli maana huyu ni Samia na yule ni Magufuli.

Kwa sasa Mama ndiye mwenye power ndani ya Chama na serikali, tukijifanya jeuri kwa mamlaka ya ndani ya katiba ya chama na ile ya Jamuhuri mamama akiamua anapanga timu yake anayoitaka itakayomsaidia kutekeleza ilani ya Chama. Sisi tudipoeleweka atatafuta timu nyingine ya kufanya nae kazi tuache porojo.

Mwenyekiti wetu Heri James ni mtu mwenye akili nyingi sana, anajua fika kabisa mazingira ya siasa za sasa ni lazima yatofautiane na ya sasa. Kwani uongo kwamba tulitumia nguvu nyingi kuendesha siasa zetu nje na ndani ya chama? Tunapokumbuka pale tulipoharibu na kutaka tuishi vizuri na ndugu zetu tuliokwisha wakwaza kuna tatizo gani?
Kama Mama yetu nafsi yake itakua na na amani akiona anaongoza taifa lenye amani na upendo kuna tatizo?

Mwisho na Muhimu.Tusitake kuanza kujenga makundi yatakayotoa faida kwa wapinzani wetu.Tufungamane na mwenyekiti wetu wa Jumuiya yetu na wa chama taifa, tuache kua wanafki.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom