UVCCM: Rostam anyang'anywe uraia na kufukuzwa nchini

Kidogokidogo hujaza kibaba,kila ufisadi utakaofanywa na viongozi wetu utakuwa ukiisongesha nchi nyuma kwa maana ya uchumi wake na hapo ni sawa na mtoto anaejumlisha 2+2=I halafu tiki kubwa akidhani anasonga mbele kumbe kila siku anazidi kuwa mjinga.Baba Mungu ibariki Tanzania
 
Watanzania tusidandie gari kwa mbele,kama ccm wameamua kujivua gamba wasafishwe mafisadi wote tena mbele ya sheria ili wakatajane vizuri; kina el,cheng,EPA sio tu ra kwakuwa aliombaga uraia basi leo mumtoe kafara!
Kama mlikula wote kwenye raha,na matanga pia mshiriki wote. Msiudanganye umma wa tz.
 
Yani hao UVCCM ndo wanaona leo kuwa Rostam ni Fisadi, walikuwa wapi enzi zile tunapiga kelele kuhusu Kagoda, Richmond, Dowans nk.
Wamechelewa sana kwa taarifa yao
 
Hawa wanachama wa Chukua Chako Mapema wanatapatapa tu na hoja zao zilizo nyepesi ambazo hata mtoto mdogo anatumbua ni ujinga na upuuzi mtu wanaongea. Hakuna mwenye uwezo wa kumchukulia fisadi yoyote hatua katika safu ya Kiongozi wao mkuu JK, kwani yeye huyo mkuu wao ana yake mengi mabovu ya kujibu. Wewe umeona wapi duniani watu wana ambiwa wajievaluate kama wao ni mafisadi na baada ya siku 90 wafanye maamuzi magumu ya kuachia ngazi, hizi ni dalili za uongozi kushindwa kufanya maamuzi yaliyo magumu. Kwa kweli hawa jamaa wametoka kuwa chama cha wakulima na wafanyakazi, na sasa wamekua chama cha madalali wa rasilimali za nchi kwa wageni ambao wako kwa ajili ya interest zao. Vile vile wamegeuka kuwa chama cha wafanyabiashara za kukwepa kodi kupita kiasi, kwa nia ya kujilimbikizia waonekane miungu watu. Hakika wakati utafiki tuta hakikisha wote wanakwenda segerea, confiscate their properties, limit their movements, trial them and sentence them to life time or 15 years in jail. Hawa ndio wanaosababisha mama zetu wanafariki wakati wa kujifungua kutoka na vituo vya afya kukosa zana za kutosha, wafanyakazi wa serikali wanageuka wala rushwa kutokana na mishahara midogo inayosababisha wakope kupitiliza. Kwa kweli inatia huruma, tunaitaji msafi mmoja with loose nuts in his/her head kulianzisha la kistaarabu mpaka kieleweke.
 
Kumbe sasa wana JF yanayosemwa humu ni kweli sasa yanajinyesha. Kwa TAMKO LA MJUMBE WA UVCCM / NA NAPE baada ya sakata la Dowans kuwaka na CHADEMA and CUF KUSEMA SERIKALI ISILIPE Hali ilikuwa tete na mpaka sasa ni tete kumbe RA alisafirisha familia yake kwenda ng'ambo. Sasa Yametimia na wanamuomba Rostam atoke CCM na atoke nchini maana anatunyonya. SIKU za MWIZO AROBAINI ZINAKARIBIA

WANAHARKATI HILI MNALIONAJE na CHADEMA ENDELEZENI MOTO UNASAIDIA SANA NA SASA HALI NI MBAYA SANA CCM.

BASHE NI WALE WALE TU

Pamoja tunasonga mbele.
 
Hivi Rostam ndo fisadi pekee Tanzania nzima? Maana kila kitu Rostam Rostam....

Ahsante Ndugu kwa kuling'amua hilo, hapa kuna namna ya kutaka kupumbaza watu kwamba eti kweli ikitokea huyo RA kudhibitiwa basi taifa zima tulale kwa amani eti ufisadi umeisha.......
Tusitoane kwenye hoja ya msingi hapa, ufisadi ni matokea tu ila mzizi wenyewe ni MFUMO MBOVU wa kiutawala...
Tukitibu mfumo, wote wenye huo "urostamu" watashindwa kuishi hapa Tanzania.
 
Mjumbe wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro Paul Makonda ameomba serikali imnyang'anye Rostam uraia na kumfukuza nchini

Source radio one news
Ni wakati wa kujikomba sasa tusishangae! Kama bosi wake wa juu kapata kigugumizi na kutowa siku90 yeye atafanya nini? Hata hivyo Domo jumba ya maneno...........!
 
HIvi kumbe Tanzania sio kwao? aligombeaje sasa wakati katiba inataka awe Mtanzania? Yaani inamanisha CHICHIEMU wako mstari wa mbele kuvunja katiba na sheria za Tanzania?

HIvi kumbe CCM inapitisha wagombea wa nafasi za juu za chama na pia serikalini ambao sio Watanzania?

Hivi kumbe CCM wameamua kabisa kuuza nchi yetu kwa wageni hata kuwaachia watutawale na kutuibia?

Ama kweli mwalimu alikuwa sahihi kusema baada ya kuwaondoa wakoloni weupe kuna hatari ya kuibuka wakoloni weusi watakaokuwa wabaya kuliko weupe

ALL in all, hatutaki kujua anaenda au la, CCM na mwizi wao walipe pesa zetu ndio wamuondoe na sheria ya uhamiaji itumike kuwabana CCM kwa kumuweka mkimbizi mwizi nchini kwetu na wakijua sio mkazi maadam tu anawahakikishia mbinu za kuiba na kuchangia chama kupata ushindi wa "kishindo" wa NEC na miujiza ya masanduku ya kura
 
Vijana wa CCM ni wapuuzi kweli kweli, na hiyo inaonyesha jinsi uongozi wa CCM ulivyo kwani akina Nchimbi na Makala walianzia huko huko vijana. Wanataka Rostam anyang'anywe uraia na kufukuza nchi ili aende wapi ilihali yeye ni raia wa Tanzania na mbunge wa Igunga?.

Una uhakika wa hilo unalosema Mkuu?
 
haina haja ya kumfukuza kwani yeye kama alikuwa mbunge ni raia wa Tz so cha muhimu ni yeye kufunguliwa mashtaka ya kuhujumu uchumi, afungwe gerezani na afilisiwe mali zote alizozipata kwa magendo. Ndo serikali itakuwa imefanya kazi bila ubaguzi, tusimmbague tumtreat kama mtanzania mwezetu akiiba anavyoadhibiwa
 
eti Umoja wa vijana wa CCM....pppfff!! Hivi kweli hao ni vijana kiumri...mbona kila nikiona kwenye mikusanyiko yao mi naona ni vizee na njemba zilizokomaa, na nyingine mpaka inatoka oili utosini!!!
 
kabla hawajamfukuza basi haturudishie pesa yetu kama alivyofanya Zakayo, pili kwani Rostam sio raia wa nchi hii ana yeye ni fisadi tu ila ni raia, isijekuwa wanataka kumficha nchi za ng'ambo kutupoza!!!! wakimfukuza basi wamfilisi kwanza mimi sina love na huyo mkuu, kaiba sana
Mjumbe wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro Paul Makonda ameomba serikali imnyang'anye Rostam uraia na kumfukuza nchini

Source radio one news
 
mkuu ni tafusiri ya ccm kama hujawai kuwa kiongozi basi wewe ni kijana hata ukiwa na miaka hamsini, si unaona januray makamba anajiita mbunge kijana wakati anacheza na 40s
eti Umoja wa vijana wa CCM....pppfff!! Hivi kweli hao ni vijana kiumri...mbona kila nikiona kwenye mikusanyiko yao mi naona ni vizee na njemba zilizokomaa, na nyingine mpaka inatoka oili utosini!!!
 
Jamani mmeona taarifa ya ITV jinsi UVCCM walivoongea live kuhusu Rostam Aziz kuondoka haraka sana hapa nchini? Mwalionaje hilo ni unafiki au wanamaanisha? Au ndo JF imewachallenge to that extent?

Mambo ya Balali hayo. Lakini Rostam hatakufa naona yeye ataishia kuishi uarabuni akitafuna kwa ulaini mali za Watanzania. Kweli huu ni usanii si mchezo.
 
Nani aliyekuambia kuwa RA ni raia mwenzako? Hivi unajua kwanini baadhi ya viongozi wetu hawataki sheria ya kuwa na uraia wa nchi mbili ipitishwe? Sasa ni mojawapo ni RA na ndio maana amekuwa mstari wa mbele kupigania dual citizenship.RA si mwenzetu!!!!!!!!!!

Anaweza kuwa raia au sio raia lakini uraia wake unakuwepo tu pale CCM wakipenda. Huoni Bashe alikua sio raia sasa amekua raia. Kweli nchi imeoza hii!!
 
Kidogokidogo hujaza kibaba,kila ufisadi utakaofanywa na viongozi wetu utakuwa ukiisongesha nchi nyuma kwa maana ya uchumi wake na hapo ni sawa na mtoto anaejumlisha 2+2=I halafu tiki kubwa akidhani anasonga mbele kumbe kila siku anazidi kuwa mjinga.Baba Mungu ibariki Tanzania
Mnataka Mungu aibariki Tanzania mara ngapi?
 
Jk kashindwa kutoa tamko juu ya mafisadi iweje huyo Makônda ambaye ni kipele tu ndan ya chama cha magamba?
 
Haifai kufukuzwa ila ashtakiwe na kufungwa ili akashike kuta za magereza yetu aonje utamu wa kutuibia
 
Back
Top Bottom