UVCCM: Rostam anyang'anywe uraia na kufukuzwa nchini

Wanataka kutoroshana kijanja,ili asiwepo wa kuhojiwa kuhusu mabilioni yetu,asifukuzwe huyo tunataka kushuhudia anaozea jela pamoja na wenzake,
wanaleta janja ya nyani kula mahindi mabichi.
 
Ni vizuri sana kusoma alama za wakati..
CCM vijana wapo mbioni kumwondoa Rostan nchini kwa sababu issue zote za Ufisadi zinatakiwa kuzungumziwa na kama watamwondoa Roastam nchini basi ushahidi wote kuhusu EPA,Richmond, Dowans na upotevu wa mabillioni ya fedha yatakosa mshtakiwa au ushahidi, hivyo yatakwisha kama ile scandal ya Balali..

Mimi nitasema kama kweli wana nia nzuri Rostam ashtakiwe kwanza na kufikishwa mbele ya sheria ikiwa chama kinahakikisha yeye ni fisadi na ndio sababu kinamwengua.. Huwezi kumfukuza mtu kazi kisha ukashindwa kumfikisha mahakamani unless kuna sababu maalum..

CCM wanacheza kuduku na maisha ya Watanzania na wajinga wengi wataingia mtego huu. Matatizo ya CCM yapo ktk utendaji kazi na ndipo Rostam anapoingia kwani hizi siasa za chama haziwahusu wananchi..Mhujumu uchumi hafukuzwi bali kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria..

Na mizizi ya Ufisadi imefika mbali sana kiasi kwamba sidhani kama kuna mtu msafi ndani ya uongozi uliopo kwani majuzi tu nilipokuwa bara nimeshuhudia viongozi wa serikali na Wabunge wetu wakinunua maelfu ya ardhi za wakulima kwa kodi za wananchi..Kila mbunge ana mahekta ya ardhi kama mali zao binafsi tena wanaitana kwa makundi na hakuna anayeona uharamu wa vitendo hivi...

Tunaunda kundi la wakoloni weusi wenye kumiliki ardhi kwa kuwahadaa wananchi kuuza ardhi zao, badala ya wao kuwa washauri wazuri wa wananchi ktk kilimo kwanza.. Shame on you all!
 
Wanataka kutoroshana kijanja,ili asiwepo wa kuhojiwa kuhusu mabilioni yetu,asifukuzwe huyo tunataka kushuhudia anaozea jela pamoja na wenzake,
wanaleta janja ya nyani kula mahindi mabichi.
na kweli, watakua wametumwa hawa, hatoki mtu, kwanza wachukue passport yake kabisa ..hatoki mtu, wasije wakaleta story za Balali, oh sijui tukimtaka tutamrudisha, mara sijui amekufa.......HATUDANGANYIKI!
 
Hili nalo wamechemka,wanamaanisha na akina EL nao wafukuzwe uraia? Jamani sheria ziko wapi za wahujumu uchumi? Segerea si ipo tele? Watanzania tuna maswali yetu na tunataka RA ayajibu kabla hajaambiwa aondoke
 
Yule kada machachari wa uvccm mkoa wa kilimanjaro Makonda,amemwaga cheche na kudai RA kipindi issue ya Richmond ilipokuwa imeshika kasi alihamishia familia yake nje ya nchi.Makonda ametaka RA apokonywe uraia na awaachie wtz nchi yao.
Makonda pia alishangazwa na kitendo cha jk kuwapa miezi mitatu mafisadi kufanya maamuzi ya kujiondoa kwenye chama.Makonda kwa kujiamini amesema alitarajia baada ya hotuba ya jk kina EL wangejiondoa wenyewe kweupeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.
 
Hivi Rostam ndo fisadi pekee Tanzania nzima? Maana kila kitu Rostam Rostam....

couple of years ago the name was balali sasa wamejivua gamba wamekuja na jina jipya rostam.....
rostam akiiba haibi peke yake lakini akitajwa anatajwa peke yake, hata kama anaoiba nao wanaiba kidogo sharti watajwe

kama tz kungekuwa na mtu mwenye maamuzi rostam ni mtu mdogo sana
 
Mbona hawajasema mwenyekiti wa chama nae ajiuzulu? rosti tamu is not acting on his own bana tusidanganyane JK ndio master mind wa mchezo wote huu.. wanatakiwa waanzie kwenye mizizi sio matawi
 
kwanini umfukuze raia mwenzako? wanaofukuzwa kwa makosa ni diplomats kwa sababu ya immunity! SHERIA itumike na nipo tayari kodi yangu itumike ipasavyo kwenye kutunza wafungwa magerezani!

Nani aliyekuambia kuwa RA ni raia mwenzako? Hivi unajua kwanini baadhi ya viongozi wetu hawataki sheria ya kuwa na uraia wa nchi mbili ipitishwe? Sasa ni mojawapo ni RA na ndio maana amekuwa mstari wa mbele kupigania dual citizenship.RA si mwenzetu!!!!!!!!!!
 
Ni vizuri sana kusoma alama za wakati..
CCM vijana wapo mbioni kumwondoa Rostan nchini kwa sababu issue zote za Ufisadi zinatakiwa kuzungumziwa na kama watamwondoa Roastam nchini basi ushahidi wote kuhusu EPA,Richmond, Dowans na upotevu wa mabillioni ya fedha yatakosa mshtakiwa au ushahidi, hivyo yatakwisha kama ile scandal ya Balali..

Mimi nitasema kama kweli wana nia nzuri Rostam ashtakiwe kwanza na kufikishwa mbele ya sheria ikiwa chama kinahakikisha yeye ni fisadi na ndio sababu kinamwengua.. Huwezi kumfukuza mtu kazi kisha ukashindwa kumfikisha mahakamani unless kuna sababu maalum..

CCM wanacheza kuduku na maisha ya Watanzania na wajinga wengi wataingia mtego huu. Matatizo ya CCM yapo ktk utendaji kazi na ndipo Rostam anapoingia kwani hizi siasa za chama haziwahusu wananchi..Mhujumu uchumi hafukuzwi bali kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria..

Na mizizi ya Ufisadi imefika mbali sana kiasi kwamba sidhani kama kuna mtu msafi ndani ya uongozi uliopo kwani majuzi tu nilipokuwa bara nimeshuhudia viongozi wa serikali na Wabunge wetu wakinunua maelfu ya ardhi za wakulima kwa kodi za wananchi..Kila mbunge ana mahekta ya ardhi kama mali zao binafsi tena wanaitana kwa makundi na hakuna anayeona uharamu wa vitendo hivi...

Tunaunda kundi la wakoloni weusi wenye kumiliki ardhi kwa kuwahadaa wananchi kuuza ardhi zao, badala ya wao kuwa washauri wazuri wa wananchi ktk kilimo kwanza.. Shame on you all!
wanataka kuleta mambo ya BALALI, "apotelee" nchi za nje!
 
mkiongelea Rosti tamu kufukuzwa inabidi muwahusishe na JK, EL, AC na ngeleja katika hilo, huwezi kumtenganisha na hao watu kamwe
 
Wamekula sasa hawana cha kumtumia kula zaidi ndio wanaongea pumba hizi kweli wana ccm wanakazi afukuzwe kwa nini wasisemwe ashitakiwe

Ili wote tusikie ukweli wa mambo, afukuzwe aondoke na siri zao wote mafisadi tu

Ni kweli huyu anatakiwa ashitakiwe ili hatimaye ahukumiwe na kunyongwa hadharani. lakini kama ilivyo kwa makosa yanayoshughulikiwa na Ocampo, he bears the gratest responsibility na kwa hiyo hoja ya kwamba wengine kwa nini wanaachwa ni kwamba hata mti huwa unakatwa shina na siyo matawi maana hayo yatakufa yenyewe ukishakata shina.

Huyu bwana hana siri zozote kuhusu ufisadi, labda awatolee hao hao aliokuwa anawatumia kwenye mabomu yake. Lakini mtu mmoja siyo serikali na kwa hiyo hawezi kudai kwamba matendo hayo ni ya serikali nzima. Athubutu kufanya hivyo aijue dola.
 
Baadae tutasikia amefia Iran na mazishi ni India. Duh, second episode
 
Makonda couldnt be more precise and truthful. Huu ni wakati wa kumkabili adui wa umma wa watanzania head on tena macho makavu. Watu wangepewa nafasi ya kutekeleza mob justice, hawa jamaa sasa hivi tungekuwa tunasoma hitma na misa za kumbukumbu ya wafu! lakini hatujachelewa maana sisi tupo na wao wapo. Tunaweza kuwanyoa bila maji na tukarejesha amani na ustawi wa nchi hii!
 
Hawa nao waache kutuzuga, kwani jamaa zao walio washirika wakuu wa watuhumiwa wa hizo kashfa mbona wako kimya? Hao UVCCM nao wanatuona kama vile wananchi wote wana vichwa vya panzi, uchaguzi uliopita wa uongozi wa uvccm ulikuwa funded na haohao and they didn't reject the funding, nakumbuka kuona kwenye taarifa ya habari mmoja wa watuhumiwa wa kashfa zilizopo kwenye billboard kwa sasa hapa nchini akimkabidhi mwenyekiti wa ccm hundi ya 400/ milioni kama mchango wake ili kufanikisha uchaguzi huo. Je hawa uvccm sasa wanataka tuimbe kama kasuku eti wamejivua gamba, is it possible?
 
Kwa nini yeye tu au kwa kuwa ni ngozi nyeupe? Kwani kila anayeibia serikali hufukuzwa nchini?
 
Hawa wanatuona majuha kama wao, wanajaribu kutuingiza kwenye mtego na huu mchezo wao wa kuigza. CCM WATANZANIA TUMEWACHOKA NA HATUDANGANYIKG TENA.
 
Back
Top Bottom