UVCCM: Rostam anyang'anywe uraia na kufukuzwa nchini

fangfangjt

JF-Expert Member
Apr 25, 2008
571
139
Mjumbe wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro Paul Makonda ameomba serikali imnyang'anye Rostam uraia na kumfukuza nchini

Source radio one news
 
Hivi Rostam ndo fisadi pekee Tanzania nzima? Maana kila kitu Rostam Rostam....
 
Vijana wa CCM ni wapuuzi kweli kweli, na hiyo inaonyesha jinsi uongozi wa CCM ulivyo kwani akina Nchimbi na Makala walianzia huko huko vijana. Wanataka Rostam anyang'anywe uraia na kufukuza nchi ili aende wapi ilihali yeye ni raia wa Tanzania na mbunge wa Igunga?.
 
Tanzania nchi yangu, sanaa nyingi sana.

Kama ya kufanya inayosemekana kujivua gamba, UVCCM walianza ngonjera sana.

Kumbe Ngonjera za UVCCM ilikuwa maandalizi ya kujivua gamba, walitumwa na wakubwa.

haya sasa tena, UVCCM ametuma aseme kile wanachotarajiwa kufanya... Teh teh ha ha haaa. Tanzania nchi wa wadanganyika wapole,... enyi wadanganyika mkisema au kuandamana mwaambiwa mwavuruga amani ..ooo udini ... na taka taka zote.

Sasa kwa vile Rostam ameshafanya kazi na ametimiza alilotumwa ... (mission accomplished) anatakiwa akapumzike na ale Hela alizowaibia watanzania bila usumbufu.

Tafadhali, Rostam Rudisha Hela za watanzania kwanza ndo uondoke??

Tafadhali Serikali ya JK, acheni usanii. Kwanza mafisadi warejeshe hela za Watanzania kwanza....
 
Tanzania nchi yangu, sanaa nyingi sana.

Kama ya kufanya inayosemekana kujivua gamba, UVCCM walianza ngonjera sana.

Kumbe Ngonjera za UVCCM ilikuwa maandalizi ya kujivua gamba, walitumwa na wakubwa.

haya sasa tena, UVCCM ametuma aseme kile wanachotarajiwa kufanya... Teh teh ha ha haaa. Tanzania nchi wa wadanganyika wapole,... enyi wadanganyika mkisema au kuandamana mwaambiwa mwavuruga amani ..ooo udini ... na taka taka zote.

Sasa kwa vile Rostam ameshafanya kazi na ametimiza alilotumwa ... (mission accomplished) anatakiwa akapumzike na ale Hela alizowaibia watanzania bila usumbufu.

Tafadhali, Rostam Rudisha Hela za watanzania kwanza ndo uondoke??

Tafadhali Serikali ya JK, acheni usanii. Kwanza mafisadi warejeshe hela za Watanzania kwanza....

kwanini afukuzwe? kwani jela za Tanzania zimejaa?
 
Uvccm Wacharuka Wakimtaka Rostam Aziz Ahame Nchi na kuwaomba wananchi wote,
kila sehemu wamuonapo au kukutana na Rostam Azizi, wamuambie aende zake sio mwenzetu na hana manufaa kwa nchi yetu.. hahaha

Na kuhusu Mafisadi wengine waliopewa siku 90, wawashangaa Rostam Azizi, Edward Lowassa na Andrew Chenge wanasubiri nini? au hadi wafukuzwe watoke fasta hayo yaliwakilishwa na Paul Mkonda..wa UVCCM Kazi Imeanza CCM mpya ishakusanya wanachama wapya zaidi ya mia sita...
 
Wamekula sasa hawana cha kumtumia kula zaidi ndio wanaongea pumba hizi kweli wana ccm wanakazi afukuzwe kwa nini wasisemwe ashitakiwe

Ili wote tusikie ukweli wa mambo, afukuzwe aondoke na siri zao wote mafisadi tu
 
thats good-ngoja wadonoane wenyewe kwa wenyewe ndani ya chama-tuone wata baki kina nani as wasafi
 
haisaidii ccm wote wezi tuu!hembu sikiliza habari kila siku ufisadi tuu!leo mkuu wa wilaya kilosa katoa hati ya kukamatwa maafisa wa halmashauri wamekula 250m kwa powetiller fake!jana darasa la shule 7.5m kuta zinaanguka bunda.mkuu wa mkoa anasema wakamatwe!kwa kweli ccm tumewachoka miaka 50 bila mafanikio hata tukiwapa 1000 haitatufikisha tupate maendeleo!kwanza mmeshaanza mtindo wa kupokezana madaraka na watoto wenu!watoto wa mwinyi,karume,nyerere,kawawa,nnauye,sokoine sasa imetosha!
 
Huyu kijana amechanganyikiwa. Kama ameiba awajibishwe kwa mujibu wa sheria. Uvccm inakuwa kama kundi la wajinga fulani linatoa vihoja vyepesi. They better shut up wenye substance waongee
 
Wamembana sana huyu bwana as if yeye peke yake ndo amesababisha matatizo tunayokuwa nayo ndani ya Tanganyika yetu. Suala ni mfumo mzima na wao wenyewe kuendelea kushikamana na chama mfu cha matumbo!
 
Afukuzwe kwenda wapi! Akamatwe na afilisiwe. Kumuondoa nchi wakati ametuibia vibilioni vyetu haimsaidii mtu yeyote. Kwa kumfikisha mahakamani tutajua mengi yaliyojifisha na pia washiriki wake wakuu watafikishwa mahakamani.
UVCCM tafadhali kwa masilahi ya taifa leteni hoja zenye mashiko, taifa hili ni letu sote majambazi sharti yashughulikiwe
 
Mimi nafikiri wametumia neno baya [ kujivua gamba] anaejivua gamba ni nyoka na nyoka ni adui wa Binadamu [Watanzania] kwahiyo hawatufai hawa nyoka tena [Black Mamba] dawa ni kuwakataa kabisa kuepuka kuendelea kuumwa na nyoka hawa.
 
Jamani mmeona taarifa ya ITV jinsi UVCCM walivoongea live kuhusu Rostam Aziz kuondoka haraka sana hapa nchini? Mwalionaje hilo ni unafiki au wanamaanisha? Au ndo JF imewachallenge to that extent?
 
kwanini umfukuze raia mwenzako? wanaofukuzwa kwa makosa ni diplomats kwa sababu ya immunity! SHERIA itumike na nipo tayari kodi yangu itumike ipasavyo kwenye kutunza wafungwa magerezani!
 
iyo no vita ya panzi wakuu.....acha kunguru afaidi. Nshawaambia chadema walisema tunaweza kufanya nchi isitawalike nyie wenye akili ya kuambiwa mkuhutubia taifa eti mnapinduliwa sasa kumbe hamkujua maana ya mweledi Ndesambulo na cdm,sasa si mlimwaga mboga, subiri tumwage ugali ndo muje kuomba samahani. Tafunana ivo ivo ili 2015 chama tawala kiwe cdm na chama kikuu cha upinzani kiwe Nccr maana chama cha kitaifa(CCM+CUF)kitakuwa mh.marehemu. Jamani chochea tena kuni za kutosha ,wakimbizane wenyewe kwa wenyewe mpaka wakome.......
 
Back
Top Bottom