UVCCM mwendo wa kuchapana kama CUF enzi hizo... Sasa ni Mara

Nimeona Morogoro Huko wametoka Nje Na kucheza ndombolo. Hiki Kikundi kinachoitwa CCM ni hatari sana
 
Aisee nimewacheki kwenye taarifa ya habari ITV,wamevulumishiana viti na mawe hadi raha,yaani nime enjoy sana kwa kweli.
 
ukisoma heading unapata hisia kwamba kuna vita kati ya zanzibar na tanganyika............ this is bad

sipendi kabisa muungano, tuwape nchi yao tu
 
MY TAKE:
Chama cha mapinduzi kimekuwa mstari wa mbele kueneza propaganda za udini, ukabila dhidi ya vyama vya upinzani lakini kwa tukio hili la uchaguzi wa vijana mkoa wa Mara imedhihirika kwa mara nyingine tena kwamba ccm ndiye baba na mama wa ukabila na udini.

Muasisi wake si unamjuwa?
 
Nimeona Morogoro Huko wametoka Nje Na kucheza ndombolo. Hiki Kikundi kinachoitwa CCM ni hatari sana

hao nao wamenishangaza sana........wamesusa mkutano kisa hakuna chai.....hivi hawa watu wa CCM ni wazima kweli.....? what is chai mpaka wasuse mkutano ?......inadhihirisha ni kiasi gani rushwa na dezo ilivyojaa kwenye hiki chama.......ndio maana nchi ni maskini mpaka leo....kwa wao kupenda kujifikiria kwanza......shame on you CCM....bahati nzuri mwisho wako ni 2015.......
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, uchaguzi wa jumuiya ya umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM mkoani Mara, umeingia dosari baada ya kuzuka vurugu kubwa za kurushiana ngumi, viti, mawe na silaha mbalimbali za jadi ndani ya ukumbi wa mkutano jambo ambalo limesababisha mkutano huo kuvunjika kwa muda.

Tizama mkongoto wenyewe kwa wenyewe UVCC


source: ITV TANZANIA ya youtube
 
Last edited by a moderator:
Hii balaa sasa Ufisadi ukizidi katika chama ndio matokeo yake haya sasa, CCM ni hatari kwa Taifa letu
 
Mi napenda kutoa pendekezo tu kwa uongozi wa chadema iwe vijijini au mijini wawe wanautalatibu wa kuonyesha sinema za mikanda ya magamba watu wanavyo gombana kisa rushwa unajua ata uko vijijini hawaoni mambo kama haya yalitokea leo,kwa mfano wawe wanatna linkage toka kikwete alivyo toa lai ya rushwa kwenye chama ushuhuda wa sumaye na huu uliotokea leo,wawe wana waonyesha cnema vijijini ckumoja kabla ya mkutano m4c sasa cku ya mkvano wenyewe ndio wanakandamiza kweli kweli na waiite m4c move show.
 
Kufa ccm na wafuasi wako wooote, kufa milele yoote. Shetani amekupenda wewe na watu wako woote, kufeni na tuwatose baharini kwasababu nyinyi ni wauaji.
 
Wakurya wamejipanga mno wakiongozwa na Vedastus matao tajiri aliekuwa mbunge wa musoma vijijiji na kwa sasa ni MNEC Musoma mjini na anataumia hela yae kuopnga safu VIONGI WA MARA WENGI WAO WAKIWA WAKURYA!

ANAINGILIA KILA WILAYA KUPANGA SAFU HELA YAKE IMEWAWEKA MFUKONI TAKUKURU KWAKE HAWAONI KABISA MFANO KATIKA UCHAGUZI WAKE WA NEC MUOSMA MJINI KIJANA WA KAKA YAKE ANAITWA MARWA ONGOING MWENYEKITI WA VIJANA MKOA ALIKUWA ANAGAWA HELA WAZI WAZI UKUMBINI ELFU 80000 LAKINI TAKUKURU WALIPEWA TAARIFA WAKAKAA KIMYA IKASIHIWA KUANDIKWA TU KATIKA MAGAZETI NA HATIMAYE VEDASTUS AKATANGAZWA KUWA MNEC!


SASA ANA VITA YA KUHAKIKISHA MAKONGORO MZANAKI HAPATI KITI CHA CCM MKOA ANATAKA KUTUMIA FEDHA ZAKE KUWEKA MKURYA WAGOMEA NI WATATU WAWILI WAKURAY MMOJA MZANAKI!


VEDATSUS MATAYO ALIHUSIKA MOJA KWA MOJA KUPANGA SAFU YA WAKURYA KWA KUTUMIA FEDHA ZAKE KATIKA WILYA YA BUTIAMA!


(1) MWENYEKITI VIJANA DARASA LA SABA MKURYA!! PESA ILIMSHINDA KIJANA MSOMI 22 YEARS!
(2) MWENYEKITI AKINA WANAWAKE MKURYA DARASA LA SABA!
(3) MWENYEKITI CCM WILYA MKURYA FORM 4
(4) MNEC MKURYA FORM SIX.

PESA YA MATAYO YA MAFUTA NA IKISAIDIA NA MZEE ............. ITALETA KIAMA CHA CCM KUANGUKA MKOA MZIMA, HASA WAJITA WAMEONEWA SASA TENA WASHINDI WANTAMBA KUWA NI RAHISI KUMUNUA MJITA!!!

Huyu jamaa ni noma kila kitu anataka na sababu ya kumpiga chini ubunge ni kitendo cha kutaka ku-dominate soko kwa kufanya biashara ndogondogo ya kufungua mabucha ya nyama kila sehemu kubwa ya mji wa Musoma na kushusha bei, wadau walivyoona hivyo wakamsubiri kipindi cha uchaguzi na kumpiga chini kwa madai anataka kuwamaliza kwa kuua biashara yao
 
Itv walionesha uvccm morogoro walitaka kususa kikao kwa kukosa chai.
 
ccm imefanya sana vurugu kwa vyama vya upinzani, na sasa wameamua kujifanyia wenyewe, sasa policcm mmeamini kama ni kweli hawa jamaa ni chanzo cha vurugu?
 
unaweza kutusaidia kwa nn mbowe alimzaba kibao mwangalizi wa kiislam ktk uchaguzi mkuu jimbo la hai mwaka 2010?

alimzaba makofi sababu ya ukumbafu wake, sio dini yake! Na kwa taarifa yako, Mbowe alipata kura nyingi sana Bomang'ombe ambapo kuna waislam wengi na wenye siasa kali kuliko wewe!
 
Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoani Mara, jana uliingia dosari baada ya kuzuka vurugu kubwa na wajumbe kurushiana ngumi, viti, mawe na silaha mbalimbali ndani ya ukumbi.

Mapigano hayo makali yaliyochukua takribani dakika 10, yalisababishwa na kilichodaiwa na wafuasi wa mmoja wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa umoja huo kumvamia Katibu Msaidizi wa CCM wilayani Tarime, Denis Zakaria, na kuanza kumshushia kichapo kwa madai kuwa alikuwa akiwahonga fedha wajumbe wa mkutano huo.

Kufuatia madai hayo, wafuasi hao waliendelea kumzonga Katibu huyo huku wakimueleza kuwa kama amekwenda kwenye uchaguzi huo kwa lengo la kugawa fedha nao walikuwa wakizihitaji.

Baada ya hali hiyo, wajumbe wa mkutano huo kutoka wilayani Tarime walilazimika kutoka nje ya ukumbi, kisha kuanza kupambana na wafuasi hao kwa kurushiana ngumi, mawe na viti huku katibu msaidizi huyo wa CCM wilayani Tarime akitimua mbio na kuingia kwenye ofisi ya Katibu wa CCM wa mkoa ili kunusuru maisha yake.

Kutokana na vurugu hizo, wajumbe hao walionekana kujawa na hasira huku wakimkimbiza kwa mbio katibu huyo msaidizi, ambaye baadaye alifanikiwa kuingia na kujifungia ndani ya ofisi ya CCM mkoa huo.

Baada ya Katibu huyo kujificha ndani ya ofisi akikwepa kipigo, wajumbe hao waliokuwa na hasira walimgeukia na kutaka kumnyang’anya kamera mwandishi wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten mkoani Mara, Mabere Makubi, kwa madai kwamba amepiga picha za vurugu hizo.

Baadhi ya wajumbe hao walioonekana kumzonga kwa kutaka kumpokonya kamera mwanahabari huyo, lakini walishindwa kutimiza lengo lao hilo baada ya Makubi kuwakabidhi kamera yake ili watoe mkanda wa picha ya video waliokuwa wakiuhitaji, jambo ambalo walishindwa kisha kuondoka na hasira zao.

Mmoja wa watu walionusurika na kipigo cha vijana hao, Arafat Idd kutoka Wilaya ya Musoma Mjini, alimlalamikia mmoja wa viongozi wa ngazi za juu wa UVCCM Mkoa wa Mara aliyemaliza muda wake, kwa kutaka kuhodhi nafasi zote zichukuliwe na wajumbe wa wilaya ya Tarime.

“Huyu (anamtaja jina) anataka nafasi zote zichukuliwe na watu wa wilaya anayotoka... Makao makuu tunaomba hili suala walione na kulishughulikia, sisi ni vijana wa mjini na tuna uwezo wa kufanya chochote,” alisema kwa jaziba mmoja wa vijana hao.

Baada ya utulivu kurejea, Dito Manko kutoka Tarime alitangazwa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mara kwa kupata kura 274, akifuatiwa na Machumu Manasa kura 245 huku wagombea wengine wakipata kura mbili na mwingine saba.

Source: Nipashe
 
Back
Top Bottom