UVCCM mwendo wa kuchapana kama CUF enzi hizo... Sasa ni Mara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM mwendo wa kuchapana kama CUF enzi hizo... Sasa ni Mara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nicholas, Oct 8, 2012.

 1. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #1
  Oct 8, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Sasa ni mara UVCCM, kila kikucha wana lao!

  BAADA ya kuripotiwa kupigana kwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), mkoani Dar es Salaam katika uchaguzi ndani ya chama hicho, ngumi zimeripotiwa sasa kutokea mkoani Mara.

  Katika hali isiyokuwa ya kawaida, uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), mkoani Mara, umeingia dosari baada ya kuzuka vurugu kubwa zilizosababisha wajumbe kuchapana makonde mazito, kurushiana viti na mawe ndani na nje ya ukumbi.

  Mapigano hayo makali ya wana CCM yaliyochukuwa takriban muda wa dakika 10 yalisababishwa na wafuasi wa mmoja wa wagombea wa nafasi ya mwenyekiti wa umoja huo, kumvamia Katibu Msaidizi wa CCM wilayani Tarime, Denis Zakaria na kuanza kumshushia kichapo cha ‘mbwa mwizi', kwa madai kuwa alikuwa akiwahonga fedha wajumbe wa mkutano huo.

  Vurugu hizo zimeibuka saa chache zilizopita, katika ukumbi wa CCM mkoa wa Mara, muda mfupi baada ya mgeni rasmi ambaye pia ni Mjumbe wa NEC kuitia wilaya ya Tarime na Kamanda wa Vijana wa CCM mkoa huo, Christopher Mwita Gachuma kufungua mkutano wa uchaguzihuo.

  Baada ya hali hiyo mapigano hayo kuibuka, wajumbe wa mkutano huo kutoka wilayani Tarime walilazimika kutoka nje ya ukumbi, kisha kuanza kupambana na wafuasi hao kwa kurushiana ngumi kavu kavu, mawe na viti huku katibu msaidizi huyo wa CCM wilayani Tarime akitimua mbio na kuingia kwenye ofisi ya Katibu wa CCM wa mkoa kwa ajili ya kunusuru maisha yake.

  Licha ya Katibu huyo wa CCM wilaya ya Tarime kutimua mbio, wajumbe hao walionekana kujawa hasira kali walimfukuza kwa mbio katibu huyo msaidizi, ambaye baadaye alifanikiwa kuingia na kujifungia ndani ya ofisi ya CCM mkoa huo.

  Baada ya Katibu huyo kujificha ndani ya ofisi akikwepa kipigo wa wana CCM wenzake, wajumbe hao walionekana kutaka kumalizia hasira zao kwa mwandishi wa kituo cha Televisheni cha Channel Ten mkoani Mara, Mabere Makubi wakitaka kumnyang'anya kamera yake kwa lengo la kutaka kufuta mkanda wa ghasia hizo, lakini wakashindwa.

  Mmoja wa watu walionusurika kipigo cha vijana hao, Arafat Idd kutoka wilaya ya Musoma mjini alimlalamikia mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mara aliyemaliza muda wake, Marwa Mathayo kwa madai ya kutaka kuhodhi nafasi zote zichukuliwe na wajumbe kutoka wilaya ya Tarime. Uchaguzi unaendelea sasa.

  Katika hatua nyingine, Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Shy-Rose Bhanji amegaragazwa na Agnes Mathew katika nafasi ya ujumbe wa Baraza Kuu la UWT taifa kutoka mkoani Mara.

  Habari hii imeandikwa na Sitta Tumma – FikraPevu, Musoma


  Source: CCM waendelea kuchapana makonde kugombea madaraka | Fikra Pevu | Kisima cha busara!

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. TOWNSEND

  TOWNSEND JF-Expert Member

  #2
  Oct 8, 2012
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,597
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Laana hio baada ya kutumia police na green guard kushambulia cdm sasa imewageukia wenyewe si unakumbuka wakati ule walipiga cdm vita sasa wao wenyewe wamesema hawataki rais wa ccm atoke kasikazini
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  aisee nimeona itv magamba vijana wanatwangana kwa viti si mchezo! Kwishnei magamba
   
 4. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,840
  Trophy Points: 280
  taabu sana hii jumuiya imekua tatizo sana hasa kwa matamko yao yasiyo na tija kwa taifa... ngoja wachapane tuu
   
 5. PPM

  PPM JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 839
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Weka taharifa vizuri, Mara kuna Wilaya nyingi, na majina pia kama unayo yaweka hadharani
   
 6. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Katika kundeleza ule utamaduni wao wa ukabila, udini, rushwa na uchakachuaji, umoja wa vijana mkoa wa Mara wameshindwa kufanya uchaguzi wao watakaowaongoza kwa kipindi kingine cha miaka mitano baada ya kuibuka vurugu kubwa zilizzopelekea kupotea kwa hali ya amani katika ukumbi wa mikutano baada ya vijana hao kuamua kuonyeshana ubabe kwa kutwangana na viti.

  Vurugu hizo zilijiri baada ya baadhi ya vijana kabila la wajita kuwatuhumu viongozi wa ccm waliosimamia uchaguzi huo kuyachakachua majina yao muda mfupi kabla ya uchaguzi na kuacha majina ya vijana wa kabila la wakurya.

  Vijana hao wamedai kwamba mchezo huo wa kuwabagua na kuwatenga vijana wa kijita umekuwa ukifanyika kila mara lakini safari hii wamesema kwamba hawatokubali kufumbia macho mchezo huo wa siasa za kikabila, rushwa na kuchakachuana, hivyo wakaamua kutoa kipigo kwa wanachama wa upande wa pili ili kuvuruiga mkutano huo ili kuhakikisha kwamba uchaguzi haufanyiki hadi majina ya vijana wenzao wa kabila lao la kijita yarejeshwe.

  MY TAKE:
  Chama cha mapinduzi kimekuwa mstari wa mbele kueneza propaganda za udini, ukabila dhidi ya vyama vya upinzani lakini kwa tukio hili la uchaguzi wa vijana mkoa wa Mara imedhihirika kwa mara nyingine tena kwamba ccm ndiye baba na mama wa ukabila na udini.

  Source ITV.

  Nakala; chama, Ritz, zomba, Tume ya Katiba, MAMA POROJO, +255, Kata nyodo, njiwa, almasiomary and all other lumumba staffs.
   
 7. M

  MATATA2011 Member

  #7
  Oct 8, 2012
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  ​Leo saa tisa kamili nimeangalia ITV katika kipindi cha habari za SAA na kuona hali ya hatari kabisa MSOMA mara, nimeshitushwa kuona watu wakipigana kana kwambwa hakuna SERIKALI?. UVCCM Msoma wametwangana kweli kweli na uchugazi umeahirishwa...kwa kweli inasikitisha na kama ingekuwa hali hiyo imetokea kwa vyama vingine sijui ingekuweje..Je ni kugombea madaraka au makundi ndani yao ndo yanakitafuna,au wamefika mwisho wa kufikiri?Source ITV...
   
 8. C

  Chacha Kisiri Senior Member

  #8
  Oct 8, 2012
  Joined: Nov 1, 2008
  Messages: 156
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Dhambi ya ukabila imeanza kuwatafuna wao wenyewe! Thanx God. Malipo ni hapa hapa duniani.
   
 9. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #9
  Oct 8, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hebu tujezeni maana wengine huku ni usiku na ITV Haishiki...Tunaomba msaada wa kuu kujua nini kinajili hapo
  Natanguliza shukurani
   
 10. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #10
  Oct 8, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  nimeona kamanda ccm kwishaaaaaaa, rushwa huko ndo imezaliwa
   
 11. M

  MATATA2011 Member

  #11
  Oct 8, 2012
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Leo saa tisa kamili nimeangalia ITV katika kipindi cha habari za SAA na kuona hali ya hatari kabisa MSOMA mara, nimeshitushwa kuona watu wakipigana kana kwambwa hakuna SERIKALI?. UVCCM Msoma wametwangana kweli kweli na uchugazi umeahirishwa...kwa kweli inasikitisha na kama ingekuwa hali hiyo imetokea kwa vyama vingine sijui ingekuweje..Je ni kugombea madaraka au makundi ndani yao ndo yanakitafuna,au wamefika mwisho wa kufikiri?Source ITV...​
   
 12. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Waache wachapane tuu! chapa ilale!
   
 13. m

  malaka JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Kuna post yangu moja niliwahi kusema mwisho wa Magamba ni 2012 kwenye uchaguzi wao. Naona yanakaribia.

  Natabiri tena. Kuna baadhi ya sehemu iwe mkoa au wilaya CCM itakosa mwanachama hata mmoja hatakuwepo.
   
 14. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mara zote ccm imetumia mbinu hiyo haramu ya kuwagawa watanzania kwa makabila yao na dini zao, sasa inajidhihirisha jinsi invyowatafuna wao wenyewe.
   
 15. M

  MATATA2011 Member

  #15
  Oct 8, 2012
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Dawa ni kuhama chama.....
   
 16. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Wenyewe kwa wenyewe wanatwangana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 17. m

  mamajack JF-Expert Member

  #17
  Oct 8, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Na bado,wakitoka hapo wanaanza kuwatafuta vigogo wao na kuwamaliza,tulieni kimyaaaaa,kama umuni vile.
  With magamba,kila kitu ni maajabu saba ya ulimwengu.
   
 18. A

  Asiyepepesa New Member

  #18
  Oct 8, 2012
  Joined: Oct 8, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ubabaishaji una mwisho Watanzania wameshachoka na tabia ya kuwachochea waumizane wao kwa wao.
   
 19. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #19
  Oct 8, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Anayemnyooshea mwenzake kidole kimoja akumbuke kuwa vinne vinamrudia mwenyewa....nyinyiemu kwa mbinu zao chafu watakufa kibudu.
   
 20. M

  Mkira JF-Expert Member

  #20
  Oct 8, 2012
  Joined: May 10, 2006
  Messages: 425
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wakurya wamejipanga mno wakiongozwa na Vedastus matao tajiri aliekuwa mbunge wa musoma vijijiji na kwa sasa ni MNEC Musoma mjini na anataumia hela yae kuopnga safu VIONGI WA MARA WENGI WAO WAKIWA WAKURYA!

  ANAINGILIA KILA WILAYA KUPANGA SAFU HELA YAKE IMEWAWEKA MFUKONI TAKUKURU KWAKE HAWAONI KABISA MFANO KATIKA UCHAGUZI WAKE WA NEC MUOSMA MJINI KIJANA WA KAKA YAKE ANAITWA MARWA ONGOING MWENYEKITI WA VIJANA MKOA ALIKUWA ANAGAWA HELA WAZI WAZI UKUMBINI ELFU 80000 LAKINI TAKUKURU WALIPEWA TAARIFA WAKAKAA KIMYA IKASIHIWA KUANDIKWA TU KATIKA MAGAZETI NA HATIMAYE VEDASTUS AKATANGAZWA KUWA MNEC!


  SASA ANA VITA YA KUHAKIKISHA MAKONGORO MZANAKI HAPATI KITI CHA CCM MKOA ANATAKA KUTUMIA FEDHA ZAKE KUWEKA MKURYA WAGOMEA NI WATATU WAWILI WAKURAY MMOJA MZANAKI!


  VEDATSUS MATAYO ALIHUSIKA MOJA KWA MOJA KUPANGA SAFU YA WAKURYA KWA KUTUMIA FEDHA ZAKE KATIKA WILYA YA BUTIAMA!


  (1) MWENYEKITI VIJANA DARASA LA SABA MKURYA!! PESA ILIMSHINDA KIJANA MSOMI 22 YEARS!
  (2) MWENYEKITI AKINA WANAWAKE MKURYA DARASA LA SABA!
  (3) MWENYEKITI CCM WILYA MKURYA FORM 4
  (4) MNEC MKURYA FORM SIX.

  PESA YA MATAYO YA MAFUTA NA IKISAIDIA NA MZEE ............. ITALETA KIAMA CHA CCM KUANGUKA MKOA MZIMA, HASA WAJITA WAMEONEWA SASA TENA WASHINDI WANTAMBA KUWA NI RAHISI KUMUNUA MJITA!!!
   
Loading...